SoC04 Mashine za EFD Zitolewe BURE kwa Wafanyabiashara Ili Iongeze Wigo wa Walipa Kodi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Tukuza hospitality

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
321
Reaction score
691
Utangulizi
Kwa mujibu wa Powercomputers Telecommunication Ltd, ''Electronic Fiscal Device (EFD)'', ni mashine iliyoundwa kwa ajili ya matumizi ya biashara ili kudhibiti ubora wa usimamizi katika maeneo ya uchambuzi wa mauzo na mfumo wa udhibiti wa bidhaa na ambayo inakidhi mahitaji yaliyoainishwa na sheria. PowerComputers imeidhinishwa Kuwa Wasambazaji wa EFD na Mamlaka ya Mapato Tanzania Tangu 2013.

Mashine hizi huuzwa kwa Wafanyabiashara waliosajiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (''TRA''); muuzaji na msambazaji pekee wa Mashine hizi ni kampuni ya Powercomputers kwa kiasi cha shilingi 600,000.00 na kuendelea, kutegemea na aina na ukubwa wa Mashine.

Dhamira ya Serikali
Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania, inafanya kampeni kubwa kupitia majukwaa mbalimbali, hususan vyombo vya habari, kuhamasisha Wafanyabiashara kutoa risiti za kielektroniki kwa kila bidhaa wanayouza. Na kwa upande mwingine, wananchi wanahamasishwa na kuhimizwa kudai risiti (ya kielektroniki) kwa kila bidhaa au huduma inayonunuliwa. Lengo kuu la kampeni hii, ni kuhakikisha bidhaa na huduma zote zinazouzwa zinalipiwa Kodi stahiki ili Mapato ya serikali yapatikane kikamilifu. Hii ni dhamira nzuri kabisa, kwani bila Mapato ya kutosha, serikali haitaweza kutoa huduma kwa wananchi wake, kama Afya, Elimu, Miundombinu muhimu (barabara, reli, vivuko, viwanja vya ndege, nk.).

Wafanyabiashara Wenye Mashine za ''EFD'' ni Wachache
Pamoja na dhamira nzuri ya serikali ya kuhakikisha Wafanyabiashara wengi wanatoa risiti (za ''EFD''), bado ni wachache sana wana hizi mashine za kielektroniki, kutokana na vigezo vilivyowekwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, ikiwa ni pamoja na kulazimika kununua Mashine, inayouzwa kwa kiasi kisichopungua shilingi 600,000.00. Inasemekana kwamba Mashine hizi huharibika mara kwa mara, ambapo mfanyabiashara hulazimika kulipa kiasi kisichopungua sh 250,000.00 kila inapofanyiwa matengenezo.

Wafanyabiashara wengi ni wa kima cha kati na cha chini. Wafanyabiashara wengi wanazungusha biashara zao kwa mitaji midogo, kati ya shilingi 50,000 na 1,000,000.00. Tuchukulie huyu mwenye sh. Milioni moja anatamani kuwa na Mashine; ambapo atapaswa alipe sh 600,000. Kumbuka, bado kuna gharama nyingine, kama leseni ya biashara, Kodi ya Mapato, na kadhalika. Kumbe, mfanyabiashara huyu, ili akidhi matakwa ya kumiliki Mashine ya ''EFD'', atatakiwa kuwa na zaidi ya sh milioni moja. Hii ndio maana wafanyabiashara wengi wa kati na wadogo kote nchini hawana uwezo wa kutoa risiti za kielektroniki, kama inavyoelekezwa na serikali.

Ukweli Usiotambuliwa na Serikali
Ni ukweli usiopingika kwamba Wafanyabiashara wadodo, wa kati na wale wakubwa, wanategemeana kwa kiasi kikubwa. Mfano mzuri ni kipindi wafanyabiashara katika soko la Kariakoo (jijini Dar es Salaam) wanagoma kutoa huduma kwa kufunga maduka, kwa ajili ya kuishinikiza serikali kusikiliza malalamiko yao; kama ilivyotokea tarehe 24/06/2024. Wailokuwa wakilalamika zaidi ni wale wafanyabiashara wadogo, kwani wanasema wameshindwa kufanya biashara zao kwa sababu, bidhaa wanazoziuza hununua kwenye maduka ya wafanyabiashara wakubwa. Hii ina maana gani? Wafanyabiashara wa kati na wadogo, wananunua bidhaa ambazo zimeshalipiwa Kodi; pili, hawa wafanyabiashara wakubwa wakiendelea kufunga biashara, mbali na wananchi kukosa bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku, kundi kubwa la watu waliojiajiri katika biashara za kati na ndogondogo, watakosa ajira.

Wafanyabiashara ndogondogo wengi hupata mahitaji yao ya kila siku kutokana na biashara zao za kila siku. Hii ndio maana kundi hili linaathirika zaidi pale wafanyabiashara wakubwa wanapogoma. Mfanyabiashara mkubwa anaweza kuishi na familia yake kwa mwaka mmoja au zaidi, bila kufanya biashara, kwa kutumia akiba aliyojiwekea; hii ni tofauti sana kwa huyu mfanyabiashara ndogondogo, ambapo kama hatafanya biashara kwa siku moja, yeye pamoja familia yake hawatapata chakula cha siku inayofuata.

Wafanyabiashara wa Kati na Wadogo-wadogo Wanaweza Kutumia Mashine za Kielektroniki

Mazingira wezeshi na rafiki yakiwekwa na serikali, wafanyabiashara hawa ambapo ni wengi sana, wataweza kuuza bidhaa zao na kutoa risiti za kielektroniki. Kuna faida ya kuwa na Mashine ya kutoa risiti, mojawapo ikiwa ni kuongeza mauzo, kupitia kuuza bidhaa kwa taasisi mbalimbali (za serikali na za kiraia) ambazo huitaji risiti kwa malipo yoyote. Kwa upande mwingine, serikali itaongeza wigo wa walipa Kodi (''Tax base'').

Mazingira wezeshi ni yapi? Hapa namaanisha, Kodi ndogo inayolipika bila kuumiza biashara husika; na Mashine ya ''EFD'' kutolewa BURE, na ikiharibika itengenezwe kwa gharama za Mamlaka ya Mapato (''TRA'').

Kwa mini Mashine zinapaswa kugharamiwa na TRA? Kimantiki, kazi ya kukusanya Kodi ya serikali, ni ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (''TRA''), na Mashine hizi ni vitendea kazi vya kukusanya Mapato haya! Sasa, kwa nini mfanyabiashara alazimishwe kununua Mashine na kuitengeneza pale inapoharibika kwa gharama zake?

Ni Muhimu Serikali Kufanya Mageuzi Makubwa
Ni ukweli usiopingika kwamba hakuna urafiki kati ya walipa Kodi na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Hii ni kwa sababu TRA hujifungia na kutunga sera na sheria za kukusanya Kodi, jambo ambalo husababisha ugumu kwa walipa Kodi; hii ina maana kuwa wanapanga namna ya kukusanya Kodi bila kufahamu kwa kina hali halisi ya wafanyabiashara (walipa Kodi). Ndio maana wafanyabiashara wengi hutumia mbinu mbalimbali kuwakwepa maafisa wa TRA; na pale inaposhindikana, wanagoma kutoa huduma, kama inavyojitojeza mara kwa mara katika solo la Kariakoo na majiji mengine kama Mbeya na Mwanza.

Mageuzi haya ni pamoja na serikali kukaa na wafanyabiashara na kuangalia upya vipengele vya sheria ambavyo vinasababisha migogoro ya kila mara na kuleta ugumu wa kukusanya Kodi. Pia serikali ipanue wigo wa walipa Kodi kwa kutoza Kodi zinazolipika, na kutoa Mashine za ''EFD'' kwa wafanyabiashara wote BURE. Haya pamoja na mengine yakifanyika, wigo wa walipa Kodi utaongezeka, na itafika wakati walipa Kodi watalipa Kodi kwa hiari popote pale walipo. Na jambo lingine muhimu ni kwa serikali kupunguza matumizi yanaipelekea kulazimika kukopa fedha katika taasisi za fefha za kimataifa, zenye riba kubwa na masharti mbalimbali. Pamoja na mengine, hili hufanya serikali kuongeza Kodi kwa walipa kodi, ili iweze kugharamia matumizi yake, ikiwa ni pamoja na kulipa madeni.

HITIMISHO
Wananchi na/au wafanyabiashara sii wagumu kulipa Kodi; sambamba na elimu juu ya umuhimu wa kulipa Kodi, serikali inapaswa kuweka mazingira rafiki yatakayovutia wengi kulipa Kodi stahiki bila shuruti.

Rejea
powercomputers.co.tz
www.mof.go.tz
 
Upvote 8

Technically zinatolewa bure kwani pesa unayo nunulia huwa inapunguzwa/inakatwa kwenye Kodi yamfanya biashara inayofuata
 
hujifungia na kutunga sera na sheria za kukusanya Kodi, jambo ambalo husababisha ugumu kwa walipa Kodi; hii ina maana kuwa wanapanga namna ya kukusanya Kodi bila kufahamu kwa kina hali halisi ya wafanyabiashara (walipa Kodi).

Hapo ndiyo wanapokosea.

Shida inaanza hapa, binafsi nina mwaka wa 3 kwenye biashara.Miaka 2 iyopolita nilifanikiwa kukusanya faida ya chini ya 15% kwenye biashara.

Swali, Kwa kikokoto hiki wewe unazani kusambaza mashine bure itasaidia.
 
Attachments

  • downloadfile.jpg
    downloadfile.jpg
    63.3 KB · Views: 8
Uko sahihi, ninachosema, machine zipatikane bure, sambamba na kutoza kodi rafiki, ambayo kila mtu ataweza kulipa bila kuumia kibiashara. Ndio maana, badala TRA kujifungia na kutupangia kodi, wakae Mara kwa Mara na walipa kodi (wawakilishi) ili kujua uhalisia wa kinachoendelea kwenye biashara. Hii inawezekana!
 
Kwa hapo umetisha 👏
 
Pia, serikali iweke utaratibu wa kulipa Kodi, ikiwezekana kila wiki. Kwa mfano, ukiniambia nilipe sh. 250,000 kwa mwaka, hata kama mauzo yangu yanakidhi kigezo, ni vigumu kulipa mara moja; lakini kama nitalipa, japo kila wiki, nitatakiwa kulipa sh. 5,000.. Viwango hivi vinalipika hata kwa wamachinga.
 
Mamlaka ya mapato iangalie upya mfumo wa Kodi pamoja na matumizi ya mashine za EFD, ili kupunguza kama sii kumaliza kabisa kero zinazojitokeza kila uchwao.
 
Mfumo wa kodi Tanzania unapaswa kufanyiwa mageuzi makubwa sana, kuwezesha kila anayestahili kulipa Kodi, afanye hivyo kwa hiari!
 
Back
Top Bottom