Mashine za kutotolesha mayai (Incubators): Upatikanaji wake, aina zake, matumizi na ushauri

day 24

Member
Joined
Dec 21, 2010
Posts
13
Reaction score
9
Habari zenu wanajamvini,

Mimi ni mfugaji mdogo wa kuku, sasa kidogo biashara yangu imepanuka, nahitaji mashine ndogo ya kutotoleshea vifaranga.

Naomba mnisaidie bei na mahali zinapopatikana, nitashukuru kwa msaada wenu.


--------------------





Wakuu kama una mashine za kuangulia mayai unaweza pata kutoka kwangu.

1. Spare parts zote za incubators


2. Trays za kuwekea mayai kwenye mashine




3. Tray za kutotoleshea


4. Kufanya repair za mashine mbovu/iliyo haribika

 
Cheki na SIDO makao makuu pale Upanga watakupa ushauri mzuri tu. Pia kwenye maduka ya kuuza vyakula vya mifugo. Pale Mbezi Luis mwisho niliziona.. kila la kheri!
 
hiyo ya mayai miamoja ni shilingi ngapi?maana huyu bwana kanigusa mimi pia nimufugaji wa bata.
 
Mdau hizo made in tanzania zina guarantee ya mda gan? Mimi nahitaji za mayai 1000 na pia sehemu ambayo naweza kupata hayo mayai please jibu bajeti kuanzia 2m/
 
Natamani kufuga kuku wa kienyeji, shida yangu ni mashine ya kutotoleshea vifaranga itumiayo mafuta ya taa. Zinapatikana wapi na kwa bei gani? Wadau nisaidieni ili nami nijaribu kwenda sambamba na hii KASI ZAIDI
 
naomba mni PM bei za hizo incubator,kwa sabab siwezi kujichinja mwenyewe kwenye bei,ni vizuri nikafaham bei ili niweze kujipanga,
 
Habari zenu wanajamvini, Mimi ni mfugaji mdogo wa kuku, sasa kidogo biashara yangu imepanuka, nahitaji mashine ndogo ya kutotoleshea vifaranga. Naomba mnisaidie bei na mahali zinapopatikana, nitashukuru kwa msaada wenu.
pale morocco kinondoni yanakopaki malori ya mchanga kuna askari jeshi mstaafu anauza hata za kutumia mafuta ya taa. Zinaangua kuanzia mayai 100 na unaweza kupata ya kuanzia laki 5
 
we nenda tu SIDO bei zinatofautiana zana kulingana na size ya incubator yenyewe
 
Habari zenu wanajamvini,

Mimi ni mfugaji mdogo wa kuku, sasa kidogo biashara yangu imepanuka, nahitaji mashine ndogo ya kutotoleshea vifaranga.

Naomba mnisaidie bei na mahali zinapopatikana, nitashukuru kwa msaada wenu.

unataka ya mafuta ya taa ( Manual ) au unataka ya umeme? uwezo wa kutoto vifaranga vingapi?
 
Natamani kufuga kuku wa kienyeji, shida yangu ni mashine ya kutotoleshea vifaranga itumiayo mafuta ya taa. Zinapatikana wapi na kwa bei gani? Wadau nisaidieni ili nami nijaribu kwenda sambamba na hii KASI ZAIDI
Wasiliana na Nenda ofisi za ScienceScope zilizoko pale mataa ya Morocco, kituo cha kuelekea Buguruni, nyuma ya magari ya mchanga. Eneo hili lipo nyuma ya ofisi za Airtel.
 
Wana JF, Naomba msaada wenu natafuta incubator yenye uwezo wa kutotoa vifaranga kuanzia idadi ya vifaranga 500 au zaidi, ni wapi naweza kupata mashine nzuri kwa bei nzuri?
 
Nenda Magomeni mapipa mtaa wa Kizingo upande wa Butiama (wa kwenda ubungo kama unatoka jangwani) kuna jamaa wanatengeneza, zinasifika ila sijawahi kuzitumia au kumjua anayetumia, niliwahi kuona TBC wanawahoji.
 
Hta mie napenda sana lakini sijui hta bei na zinakopatikana
 
Kuna jamaa yangu alinunua magomeni, incubator na inayoweza kuhatch mayai elfu tisa (9,000) hapo magomeni, cost ilikuwa arround milioni 20 za kitz, inafanya kazi mpaka leo. Yeye biashara yake ni kutotolesha vifaranga tu, unaenda na mayai yako anakucharge 300 kwa kila yai. Yakitoka yasitoke that's the cost.

Nikavutiwa na biashara nikatafuta vendor china nikapata kwa dola 2900 kila kitu, hiyo iliikuwa ni hatcher ya mayai 5000 na incubator ya mayai 6000, bei ya hatcher ilikuwa dola 700, na incubator 1100, na hizo 1100 zilikuwa ni contena la futi ishirini kuja tz. Sasa hizi habari ni za mwaka 2010 mwanzoni, sijui sasa zikoje.pia kumbuka kuna tra na customs mzigo ukishafika, fanya utafiti wa gharama za kutoa mzigo.

Kama uko interested ingia alibaba.com, jiridhishe mwenyewe na wauzaji kwa kusearch kama unavyofanya google. Halaf malizana nao. Ila kuwa makini, matapeli wengi. Ingekuwa vema ukawatumia watz wanaoenda kununua bidhaa zao huko japo wakachungulie kama jamaa wana kiwanda na wahakikishe usalama wa pesa zako kwa kuthibitisha mzigo unapakiwa melini.

Nb: hata hao watz usiwaamini sana, sanaa zimezidi nchini hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…