Mashirika 26 ya Kenya mbioni kuuzwa kwa Wachina ili kulipia madeni. Zimo Bandari zote, Benki na Viwanda vya saruji.

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
2,869
Reaction score
3,187

Bandari ya Mombasa

Hofu imetanda nchini Kenya kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa, Serikali ya Kenya iko mbioni kuuza Mashirika na Makampuni yapatayo 26 nchini humo kwa Wachina ili kupata fedha za kulipia madeni yanayoielemea Nchi hiyo.

Tume ya Ubinafsishaji imeridhia Mashirika ya Serikali 26 kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia bajeti ya Serikali. Miongoni mwao kuna: Benki ya Taifa ya Kenya; Mamlaka ya Bandari ya Kenya; Viwanda vya sukari, nyama na saruji

Hivi karibuni, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta alikuwa nchini China kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara, ambapo China ilitangaza kufungua soko lake kwa ajili ya bidhaa za Kenya. Sasa Wakenya wanahoji, iweje Kenya aruhusiwe pekee huko China, kuna nini Kenyatta alicho-offer kwa Wachina?

Baadhi tayari waneanza kuona ya Zambia yakiingia nchini Kenya, kutokana na mzigo wa madeni hasa kutoka kwa Wachina.

Haya, nyie wanaojidai kuisifia Kenya kwa diplomasia njooni hapa muone faida ya kusafiri kila mara kwenda nje halafu unarudi na mzigo wa madeni.

Kwa haya yanayotokea nchini Kenya, yanathibitisha wazi kuwa, maendeleo huwa hayaletwi kwa sababu Rais ana diplomasia nzuri na anajipendekeza nje. Maendeleo huletwa na usimamizi madhubuti wa mipango mliyojiwekea.

Nafikiria ingekuwa Hali hii ndiyo iko Tanzania, hii taarifa wale waliozaliwa kujua mabaya pekee ya Serikali wangekesha wanashangilia wakidhani anayeumia ni Rais Magufuli na siyo wao. Cha ajabu, kwa hili la Wakenya baadhi ya watu humu nchini wanaumia sana kuiona Kenya katika hali hiyo.
Halafu hawa ndio wanataka waishauri Serikali, never!!!

State to sell 26 companies to finance current budget
 
Hebu fikiria kuwa, Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) inayosimamia Bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, zimechukuliwa na Mchina, itakuwaje hapo?
 
Sasa Magufuli mbona anakopa kila siku. mbona yupo anaipeleka nchi hukohuko kwenye madeni
 
Hawa wachina ndio marafiki pendwa wa awamu ya 5!
Ni marafiki wa Awamu ya Tano lakini wanamuogopa sana Omuzilankende Muyago kutokana na kwamba jamaa hapendi kumpigia mtu magoti. Utawala wa sasa sio kama uliopita ambao haukujitokeza kipindi ulipohitajika.

Baada ya kuturingia kutupa mkopo wa kujenga SGR, walishangaa baada ya ku-secure fund huko Uturuki na kwa leo wao ndio wanajileta tena kutaka kushirikiana na Tanzania katika ujenzi wa SGR, tena kwa bei tunayotaka sisi.
Itafahamika tu.
 
Unajua mikataba 16 ya siri aliyoingia na JK na wachina? Unajua kwanini Magu hahangaiki na gas? Subir siku unakabidhiwa kwa basha wa kichina utajua mkufunge ndoa kwa Bashite au chattle.
 
Ukiona mwenzio ananyolewa, tia maji...na sisi Tanzania tunaelekea huko huko, kwa taarifa yako. tatizo siyo kutoka toka sana nje. tatizo ni mipango mibovu. kwa hilo la madeni na sisi tuko njia hiyo hiyo
 
Sasa Magufuli mbona anakopa kila siku. mbona yupo anaipeleka nchi hukohuko kwenye madeni
Serikali ya sasa haikopi kwa pupa bali ni kwa mipango inayoonekana. Na uzuri haikopi kwa mtu mmoja tu bali wengi hivyo kufanya tatizo na Mchina lisiwepo.
 
Unajua mikataba 16 ya siri aliyoingia na JK na wachina? Unajua kwanini Magu hahangaiki na gas? Subir siku unakabidhiwa kwa basha wa kichina utajua mkufunge ndoa kwa Bashite au chattle.
Kama ni Kikwete litabaki kosa lake lakini siyo la Magufuli. Huyu anasimamia masuala na kweli unayaona hayo masuala yakienda na kuyashuhudia jinsi yanavyoenda.
 
Hilo likitokea hapa kwetu nivigumu kujua, tunadhibiti sana uhuru wa habari na takwimu...uenda jambo kama hilo limesha tokea kwenye gesi yetu na mka wa nawe kwasababu serikali iko kimya kuhusu uchumi wa gesi na coal....lkn nani aliazishe asio ogopa kutekwa .
 
Sasa Magufuli mbona anakopa kila siku. mbona yupo anaipeleka nchi hukohuko kwenye madeni

Hawa Mataga watu wa ajabu sana. Hawawezi kuona kuwa sisi tukakoendani worse kuliko jirani zetu? Ni vigumu sana kukopa kwa miradi ya maendeleo kwa commercial loan ikalipa kirahisi.
 
Kama ni Kikwete litabaki kosa lake lakini siyo la Magufuli. Huyu anasimamia masuala na kweli unayaona hayo masuala yakienda na kuyashuhudia jinsi yanavyoenda.

Mtu anayetegemea mikopo hana ujanja. Tofauti ya huyu na JK ni uwazi. JK aliruhusu kwa kiwango fulani mambo kuwa wazi. Huyu hakubali mambo yawe wazi na ni bingwa wa kupika data za mafanikio. Ila naona waziri wa uchumi kajilipua jana na kuweka hali halisi hadharani.
 
Sisi si washachukua gesi? Magu hana cha kujisifu
 
Wanakucheki tu,milango ya kukopa iko wazi!Ila ukishakopa ndio utajua wanakuogopa au la!!!
 
Ukiona mwenzio ananyolewa, tia maji...na sisi Tanzania tunaelekea huko huko, kwa taarifa yako. tatizo siyo kutoka toka sana nje. tatizo ni mipango mibovu. kwa hilo la madeni na sisi tuko njia hiyo hiyo
Mkuu tumeshamalizana nao kwenye gas!Yaani wajichotea tu!
 
Hehehe!! Huu upupu huwa mnaokota wapi, eti hofu imetanda Kenya yote kwamba bandari zote zinauzwa, nyie nchi yenu ndio maana mna mkoa unaitwa Mbeya, maana ndio zenu, umbea usiokua na kipimo, halafu utakuta huu umbea sasa hivi mnaujadili nchi yote.
 
Bado mtauzwa na nyinyi,wakati si milele

Wewe bandari iko sokoni unachekacheka tu hapa kama malay kaona bia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…