MUBIKU
JF-Expert Member
- Oct 24, 2014
- 283
- 384
Habari za wakati huu, moja kwa moja niende kwenye mada kama ambavyo kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu.
Nadhani umefika sasa wakati ambapo sisi wananchi na watanzania inabidi tuanzishe mjadala wa kitaifa juu ya maswala yanayogusa uchumi wetu, Rasilimali zetu na maisha kiujumla, na kuachana na propaganda/ matukio na mijadala inayotengeneza ili kutupa upofu na kuacha kuifikirisha Akili zetu kujadili mambo Muhimu ya dhati na ya msingi katika ustawi wa uchumi wetu na vizazi vyetu.
Kuna muda najiuliza kwanini Serikali inauza/binafsisha Bandari yetu ambayo kimsingi ni bora hata iyo imeajiri wazawa kuliko baadhi ya sekta na mashirika yenye uwozo yamekaliwa kimya tu wakati wanajua fika hayana Umuhimu wa msaada kiuchumi.Hayo ndiyo yalitakiwa kubinafsishwa au kuuza ili yatuletee faida kupitia wawekezaji, kwakweli hii inaumiza sana na inasikitisha sana.
Yafuatayo ni baadhi ya Mashirika na sekta ambazo tunapaswa kuishinikiza serikali izi binafsishe kwa wawekezaji ili kukuza uchumi na kuboresha huduma kwa wananchi wake:-
1. TANESCO - Hili ni moja ya shirika linalokusanya pesa nyingi na kuwanyonya watanzania na tangu limeanzishwa limekuwa ni la kususua sua juu ya huduma zake, halina ubunifu na limekuwa likichangia kushusha uchumi kwa raia , ni miaka 59 tangu lilipoanzishwa na kumilikiwa na Serikali lakin kila siku ni vilio na halina tija. Huu ni muda sasa wa kukaribisha WAWEKEZAJI wapewe shirika hili japo kama nchi isiwe na Mashaka juu ya Nishati ya umeme ambayo ndio uti wa mgongo wa uchumi huu wa kisasa.
2.Shirika la Maendeleo ya Petrol (TPDC) - Hili ni shirika lingine ambapo limegeuka kuwa kama kampuni ya watu Binafsi, halina ubunifu lipo tu kiupigaji, nilitegemea katika Miaka 54 ya uhai wake basi hata leo tanzania ingekuwa ina kisima kimoja cha Mafuta ghafi , lakini limekalia tu kuongeza matozo na wimbo wa utafiti usio kuwa na matokeo chanya kila kukicha.
Hayo juu ni machache tu ambayo kwangu yamekuwa kero kubwa, unaweza kuyaongeza mengine na tuyatumie kama agenda ya mjadala.