Nitajibu kwa uelewa wangu mdogo wa darasa LA saba
Mashirika ya kijasusi ktk nchi tofauti huwa chini ya Raid (mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama)
Sambamba na hapo huwa chini ya Mkurugenzi wa Idara hiyo. Pia kama ilivyo ktk mashirika au taasisi zingine, hawa nao huwa na vitengo mbalimbali na vina wakubwa/wasimamizi/ viongozi wa vitengo hivyo ambapo huwa na team za watu wanao report kwao.
MAJUKUMU
Idara hizi huwa na majukumu mengi mno kiasi kwamba kuelezea yote ni ngumu..
Ila baadhi ya majukumu ni kukusanya taarifa ndani na nje ya nchi, taarifa za kiuchumi, kiteknolojia, kisiasa, kijamii na nyanja zote.
Pia jukumu lao kubwa ni kuhakikisha Ulinzi na usalama wa Taifa upo sawasawa kwa kufanyakazi kwa uadilifu/ufanisi/weledi wa hali ya juu sana. Na ndomana kwetu wanaitwa USALAMA WA TAIFA. Hapa wanajukumu la kung'amua jambo lolote linalotaka kutishia hali ya usalama wa RAIA na Taifa, kuzuia jambo hilo na endapo linakuwa limeshatokea basi wanahakikisha wanajua limefanywa na nani au limefanyikaje na kuchukua hatua zaidi.
Hizi Idara ni Idara nyeti mno na wakati mwingine inagharimu maisha yao kwa maslahi ya Taifa (mimi, wewe na yule) Japo ni wachache wanaoweza kuelewa hilo.