NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,402
- 4,532
Jumatatu iliyopita ilikuwa nitoke Mwanza kwenda dar kwa ndege ya shirika flani X saa sita mchana tukaambiwa kuna shida tukapelekwa hotelini tukaambiwa inaweza ondoka jioni. Jioni haikuwa hivyo tukaambiwa labda saa nne usiku, haikuwa hivyo tukalala hadi asubuhi.
Asubuhi tukaambiwa labda saa sita mchana aikuwa hivyo matokeo yake tukakaa hadi saa nne usiku ndio tukaondoka kumbuka hiyo ni jumanne yaani siku zaidi ya moja imepita.
Baadhi ya abira walilalamika yuko mmoja alikuwa anakwenda kwenye interview dar ilikuwa inafanyika jumanne asubuhi automatically aliikosa. Yupo mmoja alikuwa anakwenda kwenye kesi dar hakufika na alikuwa mlalamikaji hatujui kesi ilifutwa au vipi kwa mlalamikaji kutokufika mahakamani.
Yupo aliyekuwa anafanya connection na ndege ya shirika la ndege la Ethiopia sijui ilikuwaje kwakweli. Yuko mmoja alipata kaupenyo kazini kwake kwenda msibani dar maana katika siku zake za mapumziko alibakiza siku mbili tu hivyo angekwenda dar na kugeuza kesho yake matokeo yake sijui kazini kwake watamchukulia mtoro? na kitengo chake yuko peke yake hivyo kuna emergency ilitokea kazini wakampa severe reprimand.
Yote haya yasingetokea kusingekuwa na ndege kuchelewa. Sina ubishi na mashirika ya ndege kuhusu usalama wa abiria na ndege ni namba one hata wewe kungekuwa na ndege ipo uwanjani ukaambiwa hii ndege ina hitilafu lakini kama mnataka kupanda pandeni tu tuombe mungu hakika hakuna atakaye panda.
Nawapa heko kwa hili na ndio maana sikutaka kuweka wazi ni shirika gani kuharibiana biashara maana pia mlifanya hivyo ajili ya usalama wa abira na ndege.
Shida yangu na ushauri wangu ni kwamba mjaribu kuwa na maelewano ya ushirikiano kati ya shirika na shirika ili kulinda majina yenu. Mfano kama hilo shirika X liliona halitaweza basi wangewasiliana na shirika lingine B kufaulisha ku save aibu mateso na aibu kwa shirika kwa kufaulisha abiria.Kitendo cha kuwapangia hotel abiria siku mbili hiyo gharama ingejifidia kwenye kuchukua hiyo ndege nyingine.
Kwa nchi za wenzetu weupe hakuna kitu kama hiki cha kizembe.Miezi mitatu nyuma train ya Japan ilichelewa kufika kwa sekunde kadhaa abiria waliombwa radhi na kufidiwa hapa kwetu hili ni kizungumkuti.
Hiyo picha hapo ni ya abiria aliyekwama airport akijua amekosa interview na ametumia gharama zake hii kwa kweli ni very pathetic
ZINGATIENI USHAURI WANGU itafika mahali itakuwa aheri kupanda SGR.