Mashirika ya ujasusi na utata wa kifo cha Diana na Dodi

Mashirika ya ujasusi na utata wa kifo cha Diana na Dodi

Keylogger

Member
Joined
Oct 13, 2016
Posts
13
Reaction score
14
Duniani especially Tanzania ujue kunafulsa nyingi sana jamani tufanyeni
hata kazia ya kuandika vitu vyetu watanzania kwenye mitandao, tusisubiri
tufanyiwe na wazungu et hata ukigugo "jinsi ya kupika ugali" unakuta
article kaandika mzungu??? mbongo anaekula nguna kila siku hata kujisumbua???
nilikua najaribu kumbe keyboard yangu nzima haya.......

Diana,Princess of Wales, ni mmoja kati ya wanafamilia wa British royal
family alikua mke wa kwanza wa Charles,prince of Wales, mama wa prince
william na Prince Harry.

Emad El-Din Mohamed Abdel Mena'em El-Fayed alijulikana kama Dodi Fayed
mtoto wa Bilionea wa Egypt Mohamed El-Fayed anaemiliki biashara nyingi
ikiwemo hoteli kubwa iliopo Paris, ufaransa.

Maurice ni Katsa,yani kwa lugha nyingine ni Mossad field agent,
anaingia ufaransa June 1997 akiwa na kazi moja tu ya kumrecruiter informer
ambaye ni Henri Paul, ambaye cheo chake ni assistant chief wa Ritz Hotel
pia huwa anakaimu cheo cha Chauffeur kwa wageni mashughuri pale hotelini
lengo kubwa la kumrecruit Henri paul ni kuwa na mtu ambaye atakua anatoa
taarifa muhimu za kila siku, unajua tena sehemu kama hotelini ni sehemu
ambayo watu wengi wanaingia kwa shughuri mbali mbali.

Hadi kumpata Henri paul Mossad waliapitia hatua mbali mbali ila ya kwanza
ilikua kupata taarifa za wafanyakazi wote wa hoteli, hili lilifanyika kwa
kuhack kwenye computer system ya Ritz, ikabakia kutafuta mfanyakazi mwenye
kuweza kuingia sehemu yeyote ya hoteli ikiwemo vyumbani,pia anaweza pata
taarifa za wageni muda wowote akihitaji au akihitaji kupata bill za hoteli
na simu zilizopigwa na wageni, kati ya wafanyakazi wote walimpate Henri paul
pia kama chauffeur kwa watu mashughuli anaweza kusikiliza wanachozungumza
wageni na akaona wanachofanya hadi watu wanaoonana nao kwa kua yeye kazi
zake anazifanya karibu nao.
Hatua nyingine muhimu ilikua kuchunguza tabia za Henri ambayo ilichukua
wiki kadhaa hii ilichunguzwa na katsa(Mossad field agent) wakazi wa ufaransa
kwa kujifanya wafanyakazi wa bima mala wauza simu pia wafanya biashara.
Taarifa za tabia zikatumwa kwa Mossad plsychologist(sijui kiswahili chake)
na akatoa maoni yake kuwa kwa tabia ya Henri paul anaweza akarubunika na
kuwa informer wa Mossaid ikiwa mkazo utawekwa na akaaidiwa donge nzuri la
pesa baada ya kupata riport hiyo Maurice hakufanya makosa kwa Henri.
Kati ya mwezi wa nane pale Ritz hotel anategemewa kuwasili Diana na
mpenzi wake mpya Dodi Al-Fayed kumbuka huyu ni mtoto wa mmiliki wa hoteli
ya Ritz, Mohamed Al-Fayed.
Wafanyakazi wote pale hotelini waliambiwa watunze siri kuhusu ujio huo mkubwa
na endapo mfanyakazi atatoa tarifa juu ya ujio huo basi atapoteza ajira

Simu inatoa mwanga kuashilia kua kuna simu inaingia ambayo inamwamsha Maurice
toka uzingizini, ilikua 1:58 A.M siku ya jumapili,tarehe 31 mwezi wa nane
1997, aliepiga ni anafanya kazi paris kitengo cha ajari alikua recruited na
Mossad miaka kadhaa iliyopita, alipiga simu kumtaarifu Maurice kuhusu ajari
iliyotokea ikihusisha msafara wa Dodi na Diana, ambapo waliofariki ni Dodi
,Diana na Henri paul.

Miezi mitano baadae British netword ITV, inatoa documentary inayodaikua
Henri paul alikua mshilika wa karibu na French intelligence.

Mwaka 1999, Mohamed al-Fayed babayake Dodi anadai wahusika wa ajari ile ni
MI5, MI6 na French Intelligence pamoja na Mossad alienda mbali zaid akasema
hiyo ilitokea kwa kua waingeleza hawakutaka Diana aolewe na muislam maana
mtoto wao ilibidi awe mfalme wa uingeleza,mohamed aliwashutumu kuwa waingeleza
hawakutaka mfalme wao awe na damu ya kialabu.
Ila ilikuja kugundulika kua pia Diana na Dodi walikua chini ya uangalizia
na ufuatiliwaji wa hali ya juu na National Security Agency(NSA) ya Marekani
Mwanzoni wa mwezi wa tano 1999 alitokea mtu wa kuitwa Richard Tomlison
aliekua mfanyakazi wa MI6, stori yake ni kubwa kidogo sababu alifukuzwa
akadai ameonewa wakashtakiana akafungwa jela kama miaka 2 alivyotoka akakimbia
wingeleza akanza toa taalifa kibao za siri za MI6 Mbaka majina ya wafanyakazi
hadi MI6 wakasema amesababisha janga kubwa ambalo hawajawahi pata tangu
vita kuu ya dunia yaani kuna mambo kibao ila me nataka hapa ambapo alitoa
siri kuhusiana kifo cha Diana na Dodi, yeye alidai kuwa maagents MI6 walifika
Paris wiki mbili kabla ya kifo cha Diana na Dodi na walikaa vikao kadha na
Henri paul ambae walimlipa kua informer wa MI6 lakini pia Tomlison alidai
kua Henri paul ambae alikua deleva kwenye ile ajari MI6 Walimfanya kua
kipofu kwa kutumia miare mikali ya mwanga (high-powered flash) pia ni njia
maarufu sana kwa MI6 wakitaka kufanya assasination.Tomlison alienda mbali
akadai kuwa anaushaidi wa Henri Paul kuweka vinasia sauti kwenye chumba walicho
kitumia Diana na dodi kwenye Hoteli ya Ritz.

kwenye ripoti ya Mossad kupitia uchunguzi walioufanya wiki mbili kabla ya
ajari inaonesha timu ya watu 4 toka MI6, wiki ya kwanza walikua mabase kwenye
ubalozi wao lakin baadae walihamia kwenye nyumba ya kupangisha(MI6 safe house)
karibu na Ritz hotel pia kuna timu moja ilichukua vyumba pale pale Ritz hotel
siku 4 kabla ya kifo cha Diana na Dodi

Ripoti ya mossad inaonesha pia kua kati ya tarehe 14 na 15 mwezi wa nane
1997 timu ya CIA pia iliwasili paris hiyo timu ilikua ikimfuatilia Diana
kwa muda mrefu.
pia MOhamed al-Fayed anasema kua Diana alikua mjamzito...

JAMANI TUTAENDELEA MANAKE NIKO BUSY BOSS WANGU ANAJUA NAFANYA KAZI KUMBE...
YAANI WE ACHA TU KISA CHOTE NITAMALIZIA WAUNGWANA
 
Nitarudi kuisoma tar 27/04 maana ni ndefu sana hii habari


Tupo bize na maandamano ya 26/04
 
Stori Nzuri. Hongera sana ila kuna vitu unatakiwa kuviboresha katika uandishi wako mfano. Matumizi ya 'r' na 'l', pia majina ya watu kuanza na herufi kubwa. Mwisho kabisa jitahidi kututafutia tafasili za maneno ya kiingereza unayotumia (hata kama sio tafsiri rasmi) ili hata sisi tusiojua kiingereza usituache nyuma.
 
Stori Nzuri. Hongera sana ila kuna vitu unatakiwa kuviboresha katika uandishi wako mfano. Matumizi ya 'r' na 'l', pia majina ya watu kuanza na herufi kubwa. Mwisho kabisa jitahidi kututafutia tafasili za maneno ya kiingereza unayotumia (hata kama sio tafsiri rasmi) ili hata sisi tusiojua kiingereza usituache nyuma.
asante mkuu nayafanyia kazi hayo
 
mkuu ukiendelea hakikisha wanitembelezea tag
nilikuwa nampenda mnooo Diana ....kwakweli hapa umenikonga moyo ""


ama kweli mambo ya ulimwengu ni zaidi ya vile uyajuavyo
 
Princess Diana.

Sijawai kuchoka kusoma au kufatilia makala zinazomuhusu huyu dada, alikuwa ni mtu safi sana, mpole na mwenye huruma,

Kuna documentary moja niliiona aliwai kusema hapendi maisha ya ufahari na ya kifalme....alikua hana amani kabisa kwenye maisha ya kifalme,

Walimkatili sana kukatisha uhai wake mapema...na yeye alijua kuhusu mipango yote ya kumuua.

Dunia hii ina maSiri mengi sana asee.
 
Wazungu ni watu wabaya na sna hatari ulimwenguni...
 
Stori ni nzuri sana, lakini mkuu hariri stori yako kabla ya kupost. Ina makosa mengi sana ya kiuandishi.
 
Gideon spies ....kuna matukio ya kufurahisha kwenye hiyo Novel hasa nikikumbuka visa vya a gentleman spy -David Kimche
 
waingereza[m16,m15]kwa ushirikiano na MOSSAD pia CIA kwa lengo la kuhofia uislam kushamiri ulaya hii ni baada ya dod al-fayed kuwa na mpango wa kumuoa PRINCESS DIANA,kisa kinaanzia tangu enzi za british &usa miaka ya 1950's kujaribu kuangusha utawala wa iran kwa lengo la kuchota mafuta kiulain i compare iraq na libya,wazungu ni wazungu tujiandae
 
Back
Top Bottom