Mashirika ya Umma yanayohujumiwa yafutwe?

Mashirika ya Umma yanayohujumiwa yafutwe?

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
12,096
Reaction score
15,393
Mimi nashauri kwamba serikali isiyoweza kusimamia vyema mali za Watanzania ndiyo inayotakiwa kufutwa.

Maana yake ni kwamba hawa viongozi hawana uwezo wa kuwatumikia waTanzania kwa kuacha mali zao zipotee bure. Kuna sababu gani za wao kuendelea kuwa madarakani?

Shirika ulilokabidhiwa kuliendesha kwa manufaa ya wananchi, linakushinda kuliendesha, suluhisho liwe ni kulifuta shirika?

Nchi inakushinda kuiendesha, TUIFUTE NCHI? Hilo liliwezekana wapi?
 
Tanzania ndio nchi pekee ambayo mwenye anapaswa kuwawajibisha mafisadi wa Mali ya umma nae analalamika juu ya ufisadi ulio wazi kabisa hakika mwafrika hawezi kujitawala.

"Demokrasia hufanya hata wajinga kuwa viongozi"
 
Tanzania ndio nchi pekee ambayo mwenye anapaswa kuwawajibisha mafisadi wa Mali ya umma nae analalamika juu ya ufisadi ulio wazi kabisa hakika mwafrika hawezi kujitawala.

"Demokrasia hufanya hata wajinga kuwa viongozi"
Ninakubaliana na sehemu moja ya andiko lako, kuhusu "mwenye kuwawajibisha mafisadi wa mali ya umma naye analalamika juu ya ufisadi..."

Hii ni wazi yeye mwenyewe ni sehemu ya ufisadi huo; na pengine hana uchungu wowote na mali hiyo ya umma.

Kiongozi huyu tuliye naye sasa hivi hana mapenzi yoyote kuhusu nchi anayoiongoza. Hana kitu kinachomsononesha moyo wake juu ya waTanzania wanapoharibiwa mali.

Yeye yupo kwenye nafasi hiyo ya uongozi kwa bahati tu na bila kutegemea kuwa ingetokea awe kwenye nafasi hiyo, sasa uchungu na nchi utatoka wapi.

Kamwe sikubaliani nawe juu ya hiyo dhana ya kusema "...mwafrika hawezi kujitawala."

Na hili la "Demokrasia kufanya hata wajinga kuwa viongozi"?

Hapana.

Kumbuka vizuri. Ni "Democracy" ipi iliyowaweka hawa madarakani tokea hiyo 2015?

Demokrasi inao udhaifu wake kwa nchi kama hii yetu, lakini hapajawahi kuwepo na demokrasi chini ya CCM.
 
Back
Top Bottom