A
Anonymous
Guest
Habari wadau,
Upande wangu niko salama naendelea na vizuri na swaumu ya Ramadhan, japo janga la maji ni kubwa hasa kwa wakazi wa maeneo yanayohudumiwa na mto Ruvu juu kwa huduma ya Dawassa.
Tuanzie hapa :
Tarehe 28 Februari 2025, DAWASA kupitia mitandao yake ya jamii walitangaza kuwa kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji kwa maeneo yanayohudumiwa na Mto Ruvu juu. Pamoja na taarifa hiyo ambayo imetoka baada ya angalau siku tatu za tatizo hilo, ila taarifa husika imekuri tu uwepo wa tatizo na kuonyesha kwa uchache sana kua kuna hatua zinaendelea kuchukuliwa.
Kwa nini kupitia makubalianoa na wateja.
Kwanza, kwa uchache nipongeze angalau juhudi hafifu zinazofanywa na shirika la Umeme (TANESCO), pamoja na mapungufu mengi angalau taarifa zao zina uwajibikaji kidogo.
Tuendelee na kwa nini?
1. Bila shaka leo mtandao wako wa simu ukashindwa kutoa huduma kwa masaa mawili, basi inawezekana kabisa kukawa na fidia (kwa wao wenyewe kutoa au kulingana na mtu kutaka yaani kuanzisha shauri la kudai fidia), hali sivyo hivyo kwa mashirika yetu ya umma japo kuwa yanatoa huduma msingi zaidi.
2. Kushindwa kutoa taarifa elezi zinazowezesha mteja kupangilia ratiba zake pamoja na matukio katika kipindi cha ukosefu wa huduma.
3. Hakuna njia ya wazi ya kuziwajibisha taasisi hizi pale huduma inapokosekana, na hali mbaya zaida hata watoa huduma pia ukiwauliza hawajui ukosefu utakuwa mpaka lini.
4. Kutokuwa na takwimu sahihi za matumizi ya wateja wa huduma husika. Kwa mfano ni ngumu sana DAWASA kutoa takwimu ya mahitaji ya wateja wake kimaeneo, kiwakati, na hata kimsimu. Tatizo hili linapelekea kushindwa kupangilia vizuri ratiba za matengenezo na hivyo kuathiri wateja kiujumla. Takwimu zilizopo ni za ujumla na hazina uhalisia kimgawanyo (jambo hili pia lipo mpaka kwa mamlaka ya usimamizi EWURA)
Nini Kifanyike
1. Kuboresha namna ya upimaji kazi wa mashirika haya, mamlaka husika (hususani EWURA) ziweke wazi vigezo vyenye ubora vya upimaji ufanisi, na taasisi zitengeneze na kuonyesha namna wanaweza kuvifikia vigezo hvyo, wabainishe changamoto walizonazo na viashiria hvyo vipangwe mpaka kwa mtumishi mmoja mmoja.
2. Serikali ifanyie kazi changamoto hasa za upungufu za mashirika haya, na sio vibaya ikashirikiana na sekta binafsi ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma.
3. Kuwe na utaratibu bora wa kutoa fidia kwa ukosekenaji wa huduma, kwa mfano kama Mto Ruvu juu unazalisha lita 1000 kwa siku, basi DAWASA wawajibike kutafuta angalau robo ya kiasi cha siku ili kuhakikisha wateja hawakosi huduma moja kwa moja bali ni upungufu tu.
4. Wananchi tushirikiane kwenye kulinda miundombino ya usambazaji wa huduma (mabomba, nyaya za umme, minara ya simu n.k.) Ikiwemo kuripoti pale tunapoona mtu anahujumu miundombinu hiyo.
5. Kuboreshwa kwa mawasiliano hasa kipindi cha ukosefu wa huduma, kama ilivyo kwenye jumbe za ulipaji wa bili basi ziwe jumbe zinazoelezea hali ya utoaji wa huduma na kama kuna changamoto ni vyema kutolewa kwa ushauri wa njia mbadala kwa wateja.
5. Watumishi wa mashirika haya yanayotoa huduma kwa jamii wawekewe malengo kama ilivyo kwenye makampuni ya binafsi, ikiwezekana kulipwa kutokana na malengo waliyowekewa.
6. Kuboresha huduma kwa ujumla ni vyema kupitiwa kwa utaratibu mzima wa manunuzi ya serikali, ili kuboresha thamani ya hela na kuokoa muda kwenye mchakato wa manunuzi.
Naweka nukta hapa.
Maboresho ya huduma za msingi kwa jamii si suala tu la kuuza kisiasa bali ni mjumuiko wa hali ya usalama wa nchi kwa ujumla. Huduma bora huleta utulivu na ustahamilivu wa jamii na kuchochea shughuli za kiuchumii na matokeo yake ni ustawi wa jamii kwa ujumla. Hivyo ni vyema kwa wenye mamlaka kuliangalia jambo hili kwa umuhimu wa hali ya juu.
Nifahamike kama Mdau wa Umma!
Mpaka wakati mwingine, Shukrani