Rashda Zunde
JF-Expert Member
- May 28, 2022
- 204
- 231
Eneo la Loliondo ni eneo pekee Tanzania lenye idadi kubwa ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanazojishughulisha na masuala ya Ardhi na Haki za Binadamu nchini. Kwa sasa kuna jumla NGOs 17 katika eneo hilo. NGOs hizo zimekuwa zikifanya upotoshwaji kwa jamii kuhusu masuala yanayohusu uhifadhi na utalii na hivyo kuchochea vurugu kati ya Serikali na wananchi; na wawekezaji na wananchi. Malengo ya NGOs hizo ni pamoja na:-
1. Kujipatia fedha kutoka kwa wahisani mbalimbali nje ya nchi;
2. Kuendeleza muingiliano wa jamii za kimaasai katika eneo hilo kupitia koo zao (Tanzania Pastoralist Community Forum (TPCF)-Ukoo wa Loita, Pastoral Women Council (PWC)-Ukoo wa Purko. Hii ni kutokana na ukweli kwamba baadhi ya wamiliki wa NGOs hizo ni raia wa Kenya. Aidha, kuna baadhi ya NGOs nyingine (PWC & UCRT) zilizosajiliwa kwa ajili ya kulinda maslahi ya ukoo wa Purko na kulinda maslahi ya Kampuni ya Utalii ya Dorobo Tours Ltd;
3. Kumuondoa mwekezaji wa uwindaji wa kitalii (Ortello Business Corporation-(OBC)) kutoka kwenye eneo la Loliondo; na
4. Kuwaaminisha wananchi kuwa eneo la Pori Tengefu Loliondo ni ardhi ya wananchi hivyo halipaswi kutumiwa kwa shughuli za uhifadhi pekee;
Serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Samia Suluhu ina nia nzuri ya kulinda eneo hilo pamoja na kuwalinda wananchi wake. Tusikubali kudanganywa na watu wachache kwenye maslahi yao binafsi. MamaYukoKazini na Tanzania ipo salama.