Mashujaa FC wamenikumbusha enzi za RTC Kigoma

Huo mkoa umejaaliwa kwenye vipaji tele vya michezo na sanaa mbalimbali kama uimbaji, uchekeshaji et al.

Changamoto kuu inayowaathiri ni mazingira yasiyo rafiki (duni) ya watu kuwekeza kule.

Huenda kwa vile hii timu inamilikiwa na jeshi isiwe na maajabu mengi maana mifano tunayo ya timu zote zinazo/zilizo milikiwa na hawa mabakabaka hazijawa na mwendelezo bora.

Mfano ni Ruvu Jkt, Mgambo na Ruvu shooting.

Inaonesha ndani ya utaratibu wa kitaasisi kuna nyakati ni kama kuna wachezaji huacha kujumuika na timu na kwenda kulitumikia jeshi kwa kipindi flani(endapo siko sahihi naomba mnirekebishe) hivyo warudipo huikuta timu yao inawaza namna itakavyopambana huko champinship badala ya Premier league.

Tunawatakia kila la heri.

Ile mbinu ya kimedani waliyoitumia kuwaondosha Mbeya City na Pamba basi wasiitegemee maana huku wako akina mzee Mpili na wenzao wa kutegua mabomu yote na risasi mnyunyizo zisifanye kazi.
 
Leo nimeona uchawi live pale sokoine nilikuwa jukwaa kuu pale nyuma ya ma RC nimeona watu wanawanga mbele yangu
 
Tumepanda NBC premier league msimu ujao.
Mkoa ambao Hatoki Farasi
 
Vijana wa Mashujaa FC wamepanda daraja msimu ujao.

Wamenikumbusha enzi za RTC Kigoma wakati huo ikiwa na golikipa Patrick Mwangata ambaye baadae alienda Simba, winga Sanifu Lazaro Tingisha na mshambuliaji Makumbi Juma Homa ya jiji.
Hongereni sana Mashujaa, big up pia kwa Tabora Utd.
 
karibuni sana naombeni sisi yanga mtuachie point 6 msimu ujao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…