Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 4,016
- 6,759
Habari za usiku wanabodi,
Leo nimetafakari sana kuhusu Shujaa wa kizamani na jinsi legacy yake inavyozungumziwa kwa muktadha wa Uzalendo kwa taifa. Lekini kauli au neno la "Shujaa/Hero" maana yake ndogo ni "anaweza kukabili jambo lolote kwa ujasiri, bila kuzuiwa na woga. ".
Katika awamu ya tano tuliona Unafiki mkubwa na kujipendekeza kwa viongozi wa taasisi mbalimbali ili kulinda "ugali wao" kwa kauli mbiu ya uzalendo. Hili lilitokana na uwoga wa kutumbuliwa, kuchukuliwa hatua hivyo kuacha fikra za mwenyekiti zidumu. Lakini katika mazingira yeyote hata ya ukoloni kwa mfano kuna watu waliattempt kutokuwa watumwa au vibaraka japo hawakushinda vita lakini wali-attempt ku-resist kuburuzwa huko ndo maana mpaka leo tunawaimba kina Mtemi Isike, Abushiri wa Pangani, Chifu Mkwawa na kadhalika.
Hivyo basi katika kutambua uwepo wa awamu ya tano iliyojaa element zote za "Authoritarian Leadership", Hatuna budi kuwakumbuka Mashujaa wetu walioamua kutokwa wanafiki japo walikuwa ni watumishi wa tasisi mbalimbali, raia au wafanyabiashara wenye maslahi lakin hawakujali hilo na kuwa na misimamo ya kuattempt kutoburuzwa nwala kuogopa mkono wa Chuma.
Wengine walisacrifice ajira zao, mali zao na hata maisha yao. Hawa ndo Mashujaa wa kweli katika awamu ya 5. Mmi nimewakumbuka hawa.. Tulioweka kumbukumbu tunaweza kuwaleta wengine.
Kazi na iendelee