Mashujaa wa kweli Tanzania hawakumuogopa Hayati Dkt. Magufuli

Wala hakufanya ushujaa...Kapoteza kazi bure,kichaa huwezi shindana nae wla huwezi kuwa shujaa kwa kushindana na kichaa,tena ana bahati angeuawa kabisa
You are entitled to your opinion, but Likwelile is another hero
 
Prof Assad angeshughulika na mwenye akili timamu ningemuita shujaa sio kupambana na Mwendazake mgonjwa wa akili halafu tukuite shujaa, shujaa kwa kupambana na mgonjwa wa Mirembe?
Nakubaliana na wewe Magufuli alikuwa ni Kichaa kabisa. Kuna waliomugopa kama akina Kabudi, Ndugai au Bashiru na wakabadili misimamo yao kwa sababu ya ukichaa wao.

Prof Assad anakuwa shujaa kwa vile hakumuogopa Kichaa akafanya kazi kwa mujibu wa Katiba
 
Hao ndio mashujaa wetu 2015-2021,na sio Magufuli kama wengine wanavyotaka kutuaminisha
 
Kama hawa ndio mashujaa wako, basi ukapimwe akili.
 
Yule injinia wa magorofa. alimjibu jiwe kisomi mpaka alikaa mzee Jiwe
Huyu Mwamba yupo TBA na sharubu zake kama Jambazi la Kihindi kwenye Movie

Jamaa alikuwa Kavu lakin mwenye busara, na anamajibu kwa maswali yote kama vile alijua ataulizwa hayo maswali
 
1. Freeman Mbowe - Huyu ni mwamba wa mapambano na hanunuliki, japo walimhujumu kiuchumi ( kuivunja Bilcanas, kung'oa mazao katika shamba lake nk) hakuwa tayari kumsujudia shetani Magu aliyeapa kuwa mpaka 2020 upinzani utakuwa umekufa. Alisimama na CHADEMA, na kuivusha Salama
2. Tundu Lissu- Akiwa msemaji mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, alisimama kidete kueleza madhaifu yote ya Magu. Akawa anafunguliwa kesi kila siku na kulala rumande, walivyoona hatetereki wakampiga risasi 16 ili kumuua. Na bado akasavaiv
3. Kigogo 2014 - Huyu alimkosoa vikali Magu, wakaletwa wataalamu wa TEHAMA kutoka Malaysia ili wamtrace akamatwe apotezwe kwa kosa la kutoa siri nyeti za serikali, wakashindwa. Wakaletwa waisrael nao wakashindwa. Serikali ikaenda kumshtaki Twitter,akaunti yake ikafungiwa, akapambana akaifungua tena. Magu akaamua kuifunga Twitter kupitia TCRA ili isipatikane kwa watu ili watu wasimfuatilie Kigogo. Bado akaendelea kupambana kupitia VPN. Magu amekufa akitamani amkamate huyu jamaa amuonyeshe cha mtema kuni. Badala yake yeye ndo amekiona cha mtema kuni.
4. Mdude Nyagali- Huyu alikuwa anamchana hadharani Magu bila woga, alitekwa mara 2 akapigwa na kuteswa sana karibia na kupoteza maisha, lakin mizimu ya kwao ni mikali,hawakuruhusu auawe. Mwisho serikali ikaamua kumfungulia mashtaka kuwa anasafirisha madawa ya kulevya kutoka Pakistan. Mpaka sasa yupo gerezani
5. Wanasheria Fatma Karume - alipambana kuona uongozi wa kufuata misingi ya haki na sheria unafatwa, akachomewa ofisi yake, walipomuona hakomi wakamnyang'anya leseni ya uwakili. Peter Kibatala, huyu mwamba Hana maneno mengi lakin mziki wake serikali wanaujua. Amejitolea kutetea kesi zote za viongozi wa CHADEMA bure, akishirikiana na John Mallya.
6. Wanasiasa God bless Lema, John Heche, Msigwa, Sugu, Ismail Jussa, Nyalandu, January Makamba, Abeid Amani Karume nk- walimkosoa mwendazake bila woga. Wengine hapo Wakafunguliwa kesi na kukaa magereza wakitetea haki za wananchi, wengine walipoteza maslahi mengi. Ila walisimamia wanachokiamini
7. Maaskofu Bagonza, Niwemugizi, Mwamakula, Rua'ichi ,Shoo, Munga hawakumlamba miguu Magu. Siku zote waliongea ukweli wa Mungu
8. Ben Saanane- Alimkosoa vikali Magu na na akahoji hata doctorate ya Magu kuwa ya kimagumashi, Magu alivyoona anaumbuka akaamuru jamaa apotezwe mpaka leo. Damu yake iwe juu ya wote walioshiriki kumteka,kumtesa na kumuua. Damu hiyo iwe pia kwa vizazi vyao vyote,wasije kukaa na amani,kuanzia walioagiza, walioshiriki, hadi waliotekeleza. Pia hapa yupo Alphonse Mawazo ( RIP)
9. Waandishi wa habari- Azory Gwanda, Eric Kabendera, no wengine waliuawa kwa kusema ukweli, wengine waliteseka magerezani.
10. Wanaharakati wa haki za binadamu- Hellen Kijo Bisimba, Maria Sarungi, Eyakuze, Anael Nnkya, Ulimwengu, Prof Assad, Lwaitama, Olengurumwa, Kipanya, Tito Magoti, Sheikh Ponda, Mange Kimambi, Roma Mkatoliki, Tito Magoti, Maxence Melo( Huyu angeamua kutoa true identity zetu wazee wa kujificha nyuma ya key board hapa tungekwisha..much respect to him 💪👏👍nk

Hawa wote na wengine wengi ni mashujaa wa Tanzania katika kipindi kigumu ambacho kila mtu aliufyata, waliokuwa wanaandika kwenye mitandao wanatekwa wanakutwa kwenye viroba.. lakin wao hawakuogopa. Walipaza sauti zao na kupitia misukosuko mingi. Tunawashukuru kwa kuwa sauti ya wengi dhidi ya dikteta katili Magu. Mungu akuadhibu na moto mkali huko uliko.
 
Wasanii usiwasahau
Ney wa mitego
Roma
Kipanya
 
Hata mi ninayo hiyo software
 
Kumwacha Mbowe ni dhambi kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…