Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Rafiki yangu Fredy Nyaluchi kaweka hapa barzani picha ya Lucy Lameck na maelezo kidogo ya maisha yake katika siasa za Tanzania.
Nataka kumuunga mkono kwa kuongeza kidogo katika maisha ya Lucy Lameck ili kujaza nyama katika mifupa ya historia ya TANU na harakati za uhuru.
Lucy Lameck aliibuliwa na Yusuf Olotu lakini akijulikana kwa jina la kazi yake, Yusuf Ngozi kwa kuwa alikuwa mfanyabiashara wa ngozi.
Lucy Lameck akaja kufahamika na kushika nyadhifa kadhaa lakini Yusuf Olotu kafa hakuna amjuaye licha ya mchango wake mkubwa katika kuasisi TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nilikwenda kumuona Mzee Yusuf Olotu nyumbani kwake Moshi nyakati za jioni baada ya L’ Asr.
Nilimkuta Mzee Olotu ndani amelala kwa kuwa hali yake ya afya haikuwa njema sana.
Baada ya ujitambulisha alichangamka kwani nilipomtajia wazazi wangu wote akawa anawafahamu ingawa ni miaka mingi hawajaonana.
Mtoto wa Mzee Olotu Ahmed ni makamo yangu na tulicheza pamoja utotoni kwa kuwa nyumba zetu zilikuwa jirani Moshi Mtaa Chini.
Mzee Olotu alifurahi kusikia naandika kitabu cha historia yao wapigania uhuru wa Tanganyika.
Akanieleza kuwa walipita watu kwake miaka michache iliyopita wakitokea CCM na wakachukua nyaraka zake zote na picha wakidai kuwa wanakusanya nyaraka hizo na picha kwa ajili ya kuandika historia ya TANU na pia kutoa kifuta jasho kwa wale waliokuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kwa masikitiko alinieleza kuwa hakuna kilichofanyika na hata alipokwenda ofisi ya CCM kuomba angalau wamrudishie nyaraka na picha zake aliishia kuzungushwa.
Tukaanza mazungumzo huku kinasa sauti changu kikizunguka taratibu.
Mzee Olotu alikuwa anasumbuliwa na kikohozi lakini alianza kuzungumza kwa utaratibu baada ya kuwaambia vijana wake waliokuwa nje kuwa ana mgeni muhimu na hataki kusumbuliwa.
Hatukufika mbali katika mazungumzo mvua kubwa ikaanza kunyesha ikasindikizwa na radi
Kwa miaka mingi badae kila nilipokuwa namsikiza Mzee Olotu katika kinasa sauti changu na nikisikia vile akinyamaza kuzungumza kwa ajili ya kikohozi kisha akireja kueleza historia ya uhuru sauti yake ikiingiliana na radi nilikuwa najiuliza – ile radi ilikuwa inaashiria nini?
Nilikuwa Arusha baada ya miaka kupita ndipo nilipopata taarifa kuwa Mzee Olotu amefariki na kazikwa jana yake.
Niliondoka siku ya pili yake kwenda Moshi kuhani.
Nasikitika kuwa Mzee Olotu hakukiona kitabu ambacho kimemtaja yeye na wenzake katika kuunda TANU Kilimanjaro, mwaka wa 1955 na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Uchagga ilikuwa chini ya utawala wa machifu waliokuwa wakijulikana kama Mangi.
Baadhi ya machifu hawa walikuwa katika Baraza la Kutunga Sheria na kwa ujumla wao walikuwa karibu na serikali ya kikoloni kuliko walivyokuwa na wananchi wanaowaongoza.
Hali ya siasa Jimbo la Kaskazini ilikuwa ngumu na ya kukatisha tamaa.
Wakati TANU inakabiliwa na Kura Tatu mgogoro wa ardhi ya Wameru ulikuwa umekwisha kwa wananchi kudhulumiwa haki yao.
Japhet Kirilo alikuwa amerudi kutoka Umoja wa Mataifa alikopeleka madai ya Wameru mikono mitupu.
Kirilo hakuwa na chochote cha kuwaonyesha Watanganyika.
Ilikuwa Yusuf Ngozi ndiye aliyeweza kuifanya TANU iingie kwanza Moshi mjini kwa vishindo na kutoka hapo mjini akaieneza vijijini.
Kupitia kumbukumbu za Mzee Yusuf ngozi ndipo unapokutana na historia za awali kabisa za wanasiasa maarufu waliopata majina na vyeo; na wengine kuwa mawaziri katika Tanganyika huru, kama Lucy Lameck, Enesmo Eliufoo na wengineo.
Ilikuwa Yusuf Ngozi ndiye pamoja na wazalendo wengine waliifanya TANU ishinde uchaguzi wa Kura Tatu mwaka 1958.
Kupitia kumbukumbu zake halikadhalika ndipo kwa huzuni kubwa utakapokutana na mashujaa waliosahaulika kama yeye mwenyewe, mashujaa wa kike na wa kiume, wazalendo kama marehemu Mama Bint Maalim, Amina bint Kinabo, Halima bint Selengia, Juma Ngoma, Melkezedek Simon, Gabrieli Malaika na wengineo.
Hawa ndiyo mashujaa ambao kwa muda waliamua wasahau nguvu na utawala wa machifu wao na kujiweka chini ya TANU kupigania uhuru wa Tanganyika.