Wordsworth
JF-Expert Member
- Jan 14, 2019
- 1,191
- 3,360
Hivi chuoni kunakuwaje na kunguni? Wanashindwaje kupiga dawa kila baada ya muda fulani? Kuna chuo cha afya hapa Nala Dodoma wanafunzi wanataka kuhama kwasababu kunguni wamezidi. Wakaguzi, wenye mamlaka, mpo wapi? Mnaacha hizi taasisi zijiendeshe na kufuga uchafu? Au mmeshiba rushwa mpaka mnashindwa kutembea?
Kwenye vyoo sasa ndio utakimbia. Kuna vyuo kadhaa vikubwa hapa nchini ukijichanganya ukaenda chooni kule kwa wanafunzi unaweza usile chakula wiki nzima. Ukiuliza sababu unaambiwa eti hamna maji. Maji yanatoka tu vyoo vya chini ukipanda ghorofa moja maji hayatoki. Hivi hadi huu mwaka wa 2022 mnashindwa kupandisha maji ghorofani na mnasomesha watu wa sayansi na uhandisi? Hii ni AIBU.
Ni muhimu sana hizi taasisi zenye kukutanisha watu wengi zisimamie usafi wa hali ya juu. Kwanzia kwenye chakula, chooni, darasani na maeneo yote. Serikali iache uvivu na blah blah, ifanye kazi yake ya kusimamia hizi taasisi.