Mr DIY
JF-Expert Member
- Dec 24, 2016
- 1,188
- 2,553
Hili sijui naliona mimi pekee ni shida, kwanini ofisi nyingi za Masijala za halmashauri hazina dawati maalum ndani ya ofisi kwa ajili ya kuhudumia wateja wao ambao wengi wao huwa ni watumishi ila wao hupenda au hulazimisha huduma kufanyika dirishani, tena wenyewe wakiwa wamejifungia kwenye ac?
Imagine unasimama hapa nje tena koridoni unatoa shida zako za kiofisi dirishani kwenye hizo nondo ukitoka kioo kinafungwa, hivi huu utaratibu alianzisha nani.
Pia, hakuna usiri, unapokuwa na shida yako ya privacy, unapanga foleni hapo kama mpo wengi unaeleza shida yako hapohapo kwenye dirisha kila mtu anasikia, kama unawasilisha barua au nyaraka ya siri na unatakiwa kutoa maelezo, kila mtu anasikia unachokisema hapo.
Pia wengi wao wanaohusika na idara hii huku mtaani wanaitwa "Wakata umeme", wakiamua kupotezea nyaraka yako wanafanya hivyo, unajua suala lako linashughulikiwa kumbe wao wamepippiga chini na kuendelea na mambo yao.
Pia soma ~ Watumishi wa MASJALA katika halmashauri kadhaa nchini walalamikiwa kuwa na roho za uuwaji kiutumishi

========================