Masikini gari yangu niliyoagiza, uchakavu kodi mpya!

Safi sana, muwache kuleta magari yaliokwisha tupwa na wenzetu.

Tena wangefanya miaka 5 tu kwa magari yote. Hii ya miaka minane bado ina walakin.

wangefanya kama kenya, no uchakavu ni kwamba haiingia kabisa ikizidi miaka 8
 
Mwongo mkubwa wewe ajuza, assessment atafanyia nyumbani kwako ili kuwahi July 1?

We kula kulala mambo ya kuagiza magari na wewe wapi na wapi...

Wewe ni punguani wahed, leo tarehe ngapi? na huu uzi umeletwa lini? na yeye kaagiza lini?

Kusoma hujui basi hata picha huoni?
 
wangefanya kama kenya, no uchakavu ni kwamba haiingia kabisa ikizidi miaka 8

Uzee wa mashine haupimwi kama uzee wa kiumbe hai. Kama nia ni kupunguza magari chakavu watumie vyote, umri na umbali iliotembea. Gari nyingine zimekaa muda mrefu lakini ni mpya, na nyingine (hasa zilizotumika kama taxi) ni za mwaka jana lakini zimezeeka vya kutosha.
 
Mwongo mkubwa wewe ajuza, assessment atafanyia nyumbani kwako ili kuwahi July 1?

We kula kulala mambo ya kuagiza magari na wewe wapi na wapi...

As long as manifest imetoka na kwakilishwa TRA na shiping line, ataweza kufanya assessment na kulipia hata kabala meli haijafika/shusha. hakuna cha ajabu hapo.
 
Safi sana, muwache kuleta magari yaliokwisha tupwa na wenzetu.

Tena wangefanya miaka 5 tu kwa magari yote. Hii ya miaka minane bado ina walakin.

Sister Faiza mbona unawabagua wenye kipato kidogo ? Miaka mitano huoni kama utawakosesha wengi haki ya kumiliki chombo ? Tuna maendeleo gani ya kujivunia hadi tuweke benchmark ya juu hivo ? Watu wanunue gari ya ghali kwa kuendeshea barabara zipi tulizonazo ? I can guarantee you FF gari mpya iliyonunuliwa Tz kwa wakala ikatembea 50,000 km kwa miaka 2 hali ilokuwa nayo ni imechoka kuliko gari ya miaka 8 iloenda 140,000 km in Japan, hata hiyo miaka 10 ilowekwa awali haikustahili, kwa uduni wa barabara zetu, mafuta ya kuchakachuwa, spare parts feki, hatuna vifaa vya kisasa vya kutengeneza magari ya kisasa, nadhani hata magari ya miaka 25 yakiagizwa ndio sawa, M/Benz ya mwaka 2008 tu Dar nzima watu wanashindwa ku diagnose tatizo dogo tu...eti mpaka lipelekwe Nairobi..oil filter ya Lexus 2011 eti mpaka iagizwe toka Dubai !! Jamaa ana VX-R ya 2012 anashindwa kuendesha, kisa gari ina ping, diagnostic machine inamwambia fuel used too low quality..
 

Hapana sijawabagua.

Unajuwa mipango ya kwetu hapa iko kinyume nyume. Ikiwa mtu anaweza kulimbikiza mwaka au miaka miwili akanunuwa gari chakavu, basi huyo huyo anaweza kulimbikiza miaka 10 akanunuwa gari mpya.

Ni wakati muafaka sasa, tukaja na financing companies au bank inayojali wenye kipato kidogo. Unaenda wakala unanunuwa gari mpya unakatwa kidogokidogo kwenye mshahara, mradi iwe na comprehensive, na dhamana ni hiyo hiyo gari. Na makato yako yawe sawa na "depreciation" ya gari. Kila mmoja ataibuka mshindi. Gari likifika miaka 12 au 15 ni lazima liwe scrap au vintage.

Ni mipango tu na wenzetu ndivyo wafanyavyo na sasa wamepata soko la scrap zao (magari ya mitumba) kutuuzia sisi kwa bei poa.

Tukifanya hivyo utaona baada ya muda si mrefu tunafunguwa viwanda vya magari japo kuanzia kwa kuunganisha, bila hivyo hatuendelei ng'oo. Tuwe na mtazamo mpana zaidi ya hapa tulipo.

Chuma tunacho, ni wakati muafaka kianze kutumika kuunda magari badala ya kuagiza mitumba kutoka nje kuwanufaisha wengine.

Nasema ningekuwa mimi, mwisho kuagiza gari chakavu ni miaka mitano. Sasa amuwa, unagiza nje au unanunuwa jipya lililoundwa Tanzania. Ni mipangilio ya kukuza uchumi, kuongeza ajira na kuanza kujitegemea na sio kutegemea.

Tusiwe na ujamaa wa kijinga kama wa Nyerere, kufunga kiwanda cha kuunda matrekta akafunguwa kiwanda cha majembe ya mkono.

Sasa sisi tuuze chuma nje, wenzetu wakatengenezee magari na sisi tuendelee kununuwa mitumba yao? Fikiri!
 

You have made my day mkuu! Mambo ya kuiga na kukariri tu
 
Tungegoma kuagiza magari tuone hawa watu watapata wapi kodi
 
There is no way atathibitisha unless apate assessment before 1st July ambayo kama ina arrive 14th july haiwezekan kupatikana so kiukweli hana jinsi ni kujipanga tu kuumia na kodi mpya


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

BILL OF LADING date!!
 
BILL OF LADING date!!
Sheria za customs hazizungumzii BL date bali the day assessed I mean the day goods were arrived. Cahecking the BL date and what if the vessel did not reach at the destination for instance it sank utasemaje kwa hilo.

What matters ni date of arrival au kwa urahis ni Manifest Submission.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
daah pole sana mkuu.
Ila kwa mtu yeyote ambaye anahitaji kuagiza gari nje. Tafadhali tuwasiliane. Iwe ngo au private. Its better ukakutana na mtu akakupa maelekezo mazuri na namna ya kuingiza gari na shipping line gani uzitumie.
Mimi nahitaj ist toka japan nina m8 nitapata?
 
Mkuu ngoja tusubiri majadiliano kuanzia kesho, sijui kama hii kitu itapita tena! Hata mwaka jana ilikwamishwa na wabunge machachari! Ngoja tuwasikilize tena! Ni ujinga mtupu hii serikali!



Mbaya zaidi wanasahau kuwa miaka si issue bali matumizi. Kuna magari ya 2014 yametembea hadi kilometre 200000 au zaidi na kuna magari ya miaka yaa 90 au 2000 yana kilometre chini ya 50000. Kwa picha hiyo ni lipi chakavu? Au shida ni kodi kwa njia yeyote? MAJANGA
 
Safi sana, muwache kuleta magari yaliokwisha tupwa na wenzetu.

Tena wangefanya miaka 5 tu kwa magari yote. Hii ya miaka minane bado ina walakin.

.....5years ni very tight kwa uchumi wetu mdogo unaokuwa....hili suala linafanyika in phases......nashangaa wamesema 8years.....ilikuwa iwe 7years.......naipongeza serikali kwa maamuzi hayo though.....
 
Mkuu ngoja tusubiri majadiliano kuanzia kesho, sijui kama hii kitu itapita tena! Hata mwaka jana ilikwamishwa na wabunge machachari! Ngoja tuwasikilize tena! Ni ujinga mtupu hii serikali!

......magari mabovu (tena hayafanyiwi service za uhakika) yamezidi sana kuharibu mazingira yetu, maisha na afya zetu.....
...stringent measures are also necessary kufuatilia mambo ya services za magari.....GoT can make a lot of revenue out of this measure......hii mambo ya kununua tiketi siku ya nenda kwa usalama barabarani....inatuua....na tunapoteza pesa nyingi kutokana na madhara yake......
 
Nadhani ndio njia pekee alonayo kwa sasa. Nje ya hapo asikilizie maumivu maana Tz walalahoi ndo walipa kodi wakubwa.

Sorry hivi anaweza kuassess bila manifest ya shipping line sio???

.....Yes, hiyo ndio hali halisi.....wale wenye pesa zao wanapata exemptions za ajabu ajabu......
 

....Good observation points......lakini usisahau hata kule mikoani kuna bin-adam......hakuna double standard kwenye hili........tuzipende afya zetu na maisha yetu jamani.........kinachoniuma hapa ni wale matajiri wanaleta magari yao ya kifahari halafu wanapewa misamaha ya kodi.......wakati sisi tukileta yaliyo over 10 years tunapigwa adhabu + Kodi + milolongo ya rushwa (ambayo huwezi kukwepa) ili uipate gari yako......
 

....AND THIS SHOULD BE THE WAY FORWARD......Kudos FF!!..... Game Theory alisema tukitaka kupona hatuna budi kumeza dawa hata kama ni chungu kiasi gani.......
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…