masikini walimu"waanza tena kujaribu kuibembeleza serikali sikivu"

sugi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
1,392
Reaction score
295
Dar es Salaam. Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kimetaka Bunge na wazazi kuingilia kati uamuzi wa Serikali wa kukataa kukaa katika meza moja, kuzungumzia nyongeza zamishahara na posho.
Chama hicho kimesema, vinginevyo Serikali inakaribisha mgomo mwingine wa walimu.
Mwaka jana walimu nchini waligoma kufanya kazi wakishinikiza nyongeza za mishahara, lakini Serikali ilikimbilia mahakamani.
Kwa upande wake, mahakama ilisitisha mgomo huo kwa maelezo kuwa ulikuwa batili na baadaye, kuziagiza Serikali na CWT kukaa tena kwenye meza yamajadiliano.
Jana Rais wa CWT, Gratian Mukoba, alisema pamoja na chama hicho kuwa tayari kuzungumza, Serikali imekataa kuzungumza nacho kuhusu nyongeza za mishahara na masilahi mengine ya walimu.
¡°Serikali imeeleza msimamo wake wa kutojadili masuala ya mishahara na posho kupitia majadiliano kwenye mabaraza ya kisekta, ikiwa ni pamoja na Baraza la Walimu,¡± alisema Mukoba akinukuu taarifa ya Serikali.
Alisema kwa taarifa hiyo Serikali imepuuza amri ya mahakama inayotaka pande hizo kukaa meza moja kwa sababu inafahamu kwamba haitachukuliwa hatua yoyote.
¡°Serikali haikujifunza chochote katika mgomo wa walimu uliopita na inatamani kuona mgomo mwingine mwaka huu, Bunge na wazazi tunaomba muingilie kati matatizo haya ya walimu,¡± alisema Mukoba.
Alisema walimu wakigoma watasababisha wanafunzi milioni 10 kukosa masomo kwa vile tu Serikali imekataa kutimiza wajibu wake wa kisheria.
Rais huyo alisema walimu hawataki Serikali kuwapangia mishahara bila kujadiliana na CWT.
Alisema mbali na mahakama, hata Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, ilielekeza pande hizo mbili kukaa pamoja na kujadiliana kuhusu matatizo ya walimu.
¡°Sasa ni Serikali gani isiyosikiliza matatizo ya walimu ambayo yameonekana na mahakama kuwa yana maana,¡± alihoji Mukoba.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa walimu, kikao kilichokataa kuzungumzia mishahara na posho kilifanyika Aprili 2 mwakahuu, chini ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue.

Source mwananchi
 
Ni kauli nzuri aliyoisema Bw Mukoba,lakini sidhani kama serokali hii sikivu italichukulia suala hilo kwa uzito unaostahil coz inawezekana kwa sasa sio sikivu bali dhaifu ambayo haiwezi kukusanya kodi na kutatua madai lukuki ya walimu kama mishahara na posho. Ngoja kitaeleweka tu,tumeanza na kufelisha kitakachofuata ni kupotosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…