SoC04 Masingo maza na masingo father, mayatima wapya wanaohitaji kituo cha taifa cha mahusiano na familia

Tanzania Tuitakayo competition threads

WAPEKEE_

Member
Joined
May 23, 2024
Posts
21
Reaction score
28
'MASINGO MAZA NA MASINGO FATHER', MAYATIMA WAPYA WANAOHITAJI KITUO CHA MALEZI CHA TAIFA.

Ndugu zangu, Idadi ya MASINGO MAZA, inatishia uhai wa KIZAZI KIJACHO. Hivi sasa tunaanda KIZAZI ambacho hakitatambua nafasi ya BABA kwenye familia. Iko haja kama Taifa kwa miaka 25 ijayo, tuje na tiba ya 'Masingo Maza na Masingo Faza'.

'Masingo Maza' , Hawa ni wale Wanawake ambao hawaishi na waume zao ili kulea familia zao na hasa kulea watoto. Hawa walikuwa na mahusiano lakini, yakavunjika kwasababu mbalimbali, na kufanya watengane au waachane na kuishi peke yao bila ya kuwa na Baba katika familia.

Idadi yao imeongezeka na inatishia uwepo wa Taasisi ya familia Tanzania na hata Afrika. Hivi sasa wanawake Wana mitazamo hasi, ikitokea changamoto kidogo tu, wanakimbilina kuachana na waume zao, na kuamua kulea familia zao bila waume zao. Hii imesababisha Watoto MAYATIMA wengi wa hiari ambao baba zao wako hai.

'Masingo Faza', Hawa ni wale wanaume ambao, wamekimbiwa na wake zao, wameachwa na wake zao, na wametengwa na wake zao, kwa vigezo vya wanawake sasa wanaweza kuishi peke yao bila wanaume. MASINGO FAZA hawa wamekubaliana na ukweli, na kwa uchungu wamekata tamaa na maisha ya kuishi na Mke, na wamechagua kuishi maisha ya kubadilisha wanawake bila kuoa, kama visasi kwa Masingo Maza.

KITUO CHA TAIFA CHA MAHUSIANO NA FAMILIA

Kama kwenye jamii tuna vituo vya kulea mayatima, sasa kiwepo KITUO CHA TAIFA CHA MASINGO MAZA NA FAZA. Hiki kiwe kituo maalumu Cha kutoa Usuluhishi wa migogoro ya mahusiano, kuanzia ngazi ya Mpenzi, Uchumba, NDOA na Familia. Ndugu zangu kituo hiki ndio tiba ya kuvunjika kwa taaisisi ya familia.

KITUO hiki kitatoa msaada wa KISHERIA, KIDINI, KIFIKRA, KISAIKOLIJIA, KIHISIA, USHAURI NA MBINU za kuimarisha mahusiano ya kuijenga familia.

KITUO hiki kitakuwa na wataalamu, waliobobea kwenye masuala ya Saikolojia, Afya ya Akili, Mahusiano ya Umma, na wataalamu wa Sheria na Ndoa, pamoja na wataalamu wa masuala ya Dini katika kuijenga familia Bora.

Kuna ongezeko kubwa la Talaka, kwasasa, ikiashiria kuwa Uvumilivu na Ustahimilivu katika jamii umepungua ama kuisha kabisa, watu hawavumiliani kabisa, hawasameheani, hawapendani kwa dhati na hawaamniani tena. Hivyo uwepo wa kituo kikubwa kama hiki Cha msaada wa Kifamilia itasaidia sana kuwa na jamii yenye maendeleo ya KIFIKRA na KIJAMII.

Ndugu zangu watu Wana matatizo makubwa ya KIHISIA na KIAKILI kwasasa, hii inatokana na MABADILIKO makubwa ya KIJAMII katika muingiliano wa watu na tamaduni za nje.

Hivi sasa ngono inapatikana karibu na BURE, na hii imefanya watu kupunguza uzito wa mahusiano ya kuvumiliana mpaka kufa. Na imefanya mahusiano mengi yavunjike na kuzalisha mamilioni ya MAYATIMA WA MAPENZI, yaaani Masingo Maza na Masingo Faza.

Kituo hiki kiendeshwe kwa nguvu ya Serikali, Dini, Mahakama, Taasisi na Wanajamii wenyewe. Ni lazima kabla watu hawajapeleka migogoro yao mahakamani wapewe kwanza USHAURI NASAHA wa kimahusiano na familia.

KITUO CHA KIDIJITALI.
Kwasasa Dijitali Ina nguvu ya kuwafikia watu kwa haraka sana. KITUO hiki kitaendeshwa kidijitali zaidi ili kutatia migogoro kwa haraka, maana kwasasa watu hawaana kabisa Uvumilivu wa kusubiri taratibu za Usuluhishi. Hivyo Huduma za kidijitali za kimahusiano na familia ziongezwe ili kulinda mustakabari wa JAMII Bora kwa miaka na vizazi vijavyo.

Kuwe na simu ya bure na simu maalumu ya DHARULA ZA KIMAPENZI NA NDOA. Ili kuokoa mahusiano yanayovunjika Kila siku inayokwenda kwa Mungu.

USHAURI NA HUDUMA ZA KIDINI SMART.
Dini Ina nguvu sana ya kufanya watu wajishushe kwa kuogopa na kuheshimu nguvu ya Mungu. Watu Hawa ni Moja ya washauri na matabibu wakubwa wa migogoro Mingi ya KIJAMII ikiwepo Ndoa.
Hivyo katika kituo hiki kuwe na dawati la USHAURI wa KIDINI, kutoka kwa Watumishi wa Mungu, kutoka dini zote kubwa. Hii itasaidia kuponya mioyo ya watu iliyojeruhiwa na kuokoa mahusiano na Ndoa zinazovunjika Kila Leo.


MSAADA WA MALEZI
Hivi sasa Watoto Mayatima Wa Hiari, wako wengi na wanaongezeka kilasiku. Sasa kituo hiki kitoe msaada wa kisaikolojia, kwa familia na hasa watoto na wazazi wao au walezi wao, njia Bora zaidi ya kuwalea watoto kwenye Misingi ya upendo, amani na usalama. Ni lazima tukilinde KIZAZI KIJACHO kwa kutokulisha sumu kuwa kwasasa hakuna Ndoa tena, Wala hakuna kuaminiana tena au hakuna upendo tena. Lazima tuwafundishe na kuwalea watoto kwenye Maadili yanayotambua nafasi ya wazazi wote wawili kwenye USTAWI WA Famia na upendo kwenye jamii.
Hawa watoto ndio wanandoa wajao, hawapaswi kuishi na majeraha ya wazazi wao maishani mwao, ili kutokurithisha chuki kwa KIZAZI KIJACHO.

MSAADA WA KISHERIA.
Mahakama inapaswa kuwa njia ya mwisho ya kunusuru mahusiano na Ndoa. MSAADA wa KISHERIA unapaswa kuwa kwenye Talaka, Mgawanyo wa Mali, Mirathi na Haki za Kibinadamu. KITUO CHA TAIFA CHA MAHUSIANO NA FAMILIA, kitakuwa na jukumu la kuwasaidia wanandoa KISHERIA zaidi ili kulinda maslahi ya Kifamilia na jamii kwa ujumla. KITUO hiki kitakuwa na wataalamu wa kutosha ili kuwahudumia watu wote WENYE changamoto za kimahusiano na familia.

HOSPITALI YA MAHUSIANO NA FAMILIA.
Afya ya Akili ni Moja ya tatizo kubwa zaidi kwa sasa duniani. Lazima watu watibiwe hospitalini na kwenye kliniki maalumu za mahusiano na familia. Kwenye matatizo ya Afya ya Akili, mengi yanasababiswa na Familia na Mahusiano, hivyo ni lazima tuwe na kitengo, kiliniki au HOSPITALI kabisa ya kuhudumia wenza wa Ndoa, wachumba, wapenzi, watoto na jamii kwa ujumla.

HITIMISHO.
Ndugu zangu, Wanandoa waliotengana na kuachana, maarufu kama Masingo Maza na Masingo Faza, ni janga jipya la KITAIFA, tulinde KIZAZI chetu na USTAWI WA familia kwa maslahi ya kuwa na jamii yenye Umoja kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa, kwa maendeleo ya miaka 25 ijayo na vizazi vingi vijavyo.

Naitwa WAPEKEE KEPHAS YOHANA
SIMU NA WHATSAPP: +255 694 024 888.
 
Upvote 3
Bonge la point
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…