Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
rage uwe makini siku nyingine mambo muhimu usikimbilie kweye vyombo va habari
kama ulivyomuasa mussa mgosi awe makini tunakushauri na wewe ujipende uwe makini aibu isikukute tena mzee mzima hata hivyo tunakupongeza kuileta timu ya BNGM
Mapokezi ya Asamoah usipime Send to a friend Thursday, 12 May 2011 21:10 0diggsdigg
Mshambuliaji Kenneth Asamoah akiwa amezungungwa na mashabiki wa Yanga baada kuwasili jana asubuhi kwenye Uwanja Ndege wa Kimataifa ya Dar es Salaam (D.I.A) na kuvishwa jezi ya timu hiyo namba 30 yenye jina la Mwenyekiti wa Simba Aden Rage.Picha na Jackson Odoyo
Jackson Odoyo
HAYAWI HAYAWI yamekuwa, hiyo ndiyo ilikuwa kauli ya mashabiki lukuki wa Yanga waliofika kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Ndege jijini Dar es Salaam (D.I.A) kwa ajili ya kumpokea mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Kenneth Asamoah.
Mashabiki hao waliongozwa na Mwenyekiti wa timu hiyo, Lyod Nchunga na Katibu Mkuu wake Mwesigwa Selestine pamoja na msemaji wa timu hiyo Louis Sendeu na viongozi mbalimbali waliokuwa wenye furaha kutokana na ujio wa mchezaji huyo aliyewasili uwanjani hapo saa 3:20 asubuhi.
Furaha ya Wanajangwani hao iliongozeka baada ya kubaini kumpiga bao la kisigino Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage ambaye alikuwa akitangaza kuwa Simba wanamwania mchezaji huyo.
Kwa kukejeri madai hayo ya Rage, msemaji wa Yanga, Sendeu aliamua kumvisha Asamoah jezi ya Yanga namba 30 yenye jina la mwenyekiti wa Simba kifuani ikisomeka A. Rage 30.
Akizungumza na Mwananchi uwanjani hapo Asamoah alisema amekuja kukamilisha taratibu za kujiunga na Yanga.
Kuhusu hatua ya kudaiwa kujiunga na Simba, Asamoah alisema, mimi ni mchezaji wa Yanga isipokuwa nilishindwa kuitumikia timu hiyo msimu uliopita kutokana na taratibu ambazo hazikuwekwa vizuri kwa sababu ya muda kuwa mfupi.
Alisema hana mpango wowote wa kujiunga na Simba kwa sababu yeye ni mchezaji wa Yanga na kwamba hakuna mazungumzo yoyote yaliyokwisha fanyanyika kati yake na viongozi wa Simba mpaka hivi sasa.
Ishu hapa ni Yanga wala sio Simba, mimi viongozi wa Simba siwafahamu kwa sura wala kwa majina sasa iweje useme kuwa ninataka kujiunga na Simba, wewe niulize mambo ya Yanga na sio ya Simba,alifafanua mchezaji huyo wa zamani wa Jogodina ya Serbia.
Kuhusu klabu yake ya Jogodina alisema, maamuzi ya kujiunga na Yanga ni yangu mwenyewe si klabu isipokuwa klabu hizi mbili zinapaswa kuzungumzia suala la mkataba ili ili niweze kuchezea Yanga.
Alisema mazungumzo baina ya Yanga na Jogodina yanaendelea vizuri na safari hii ana imani ataweza kucheza soka Tanzania kwa sababu mambo yameanza mapema tofauti na mwaka jana.
Mghana huyo alisema,mapokezi haya niliyoyapata hapa yamenipa deni kubwa, nina kazi ya kulipa deni kwa mashabiki wa Yanga na hilo nitalitimiza kwa kuifungia magoli mengi na kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu wa ndani na kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika pia.