Maskini, Mnyonge, Mzalendo.

Itoye

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2017
Posts
531
Reaction score
1,023
Wakuu Salam,

Binafsi nikiwa miongoni mwa watanzania milioni 50, sina shaka na UZALENDO wangu kwa taifa langu lakini hizi title mbili za UMASKINI na UNYONGE sizikubali, sijui wewe mwezangu...

Kama na wewe hutaki title ya MASKINI na MNYONGE basi tuungane na tukusanye saini za kutosha halafu tuwaombe waheshimiwa kupitia kwa ZZK ambaye yumo humu jukwaani atufikishie maombi yetu kuwa maneno huumba kuendelea kutuita MASKINI na WANYONGE akili zinalemaa na kama tulivyoanza kukiri kuwa nchi yetu ni tajiri basi na title tuliyopewa ibadilishwe.

Karibuni.
 
Usipokuwa mnyonge na maskini utatawaliwaje mkuu.!!!?
 
Yaani hata me nashangaa. Umasikini sio sifa yetu wala unyonge.
 
Ni Tanzania pekee ambako raia wake ni masikini na wanyonge lakini ni nchi tajiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…