SoC01 Maskini Tanzania, Taifa kubwa lililo usingizini

Stories of Change - 2021 Competition

Gnyaisa

Member
Joined
Jul 13, 2021
Posts
23
Reaction score
24
Tanzania ni miongoni mwa mataifa makubwa kijiografia katika uso wa dunia hii likiwa linashika nafasi ya 13 kwa ukubwa barani Afrika. Kulingana na kitabu cha rekodi za dunia (World Factbook), Tanzania inachupa hadi nafasi ya 31 kwa ukubwa ulimwenguni kati ya mataifa 257 yaliyoorodheshwa katika kitabu hicho maarufu.

Wakati mataifa ya Rwanda na Burundi kwa pamoja yakiwa na ukubwa wa kilomita za mramba 54,172 na jumla ya watu milioni 22 (sensa 2013), mkoa wa Tabora pekee una ukubwa wa kilomita za mraba 75,264 na jumla ya watu milioni 2 tu (sensa 2012)

Pamoja na ukubwa wa eneo tulionao, Tanzania ni miongoni mwa mataifa masikini kabisa duniani licha ya utitiri wa wasomi wanaozalishwa na vyuo vyetu kila kukicha.

Vijana ambao ndio nguvukazi inayotegemewa na taifa hili ni zaidi ya asilimia 65 ya watu wote lakini ni wazi kuwa nguvukazi hii haijaweza kutumika vyema katika kuharakisha maendeleo ya taifa letu.

Tunaishi katika taifa ambalo wazazi wengi wanaamini kijana akimaliza masomo yake ya elimu ya juu anapaswa kuzunguka maofisini na kutafuta ajira kwa ajili ya kuwasaidia ndugu na wadogo zake aliowaacha nyuma licha ya familia kuwa na uwezo wa kujihudumia.

Ile dhana kwamba msomi ni mali ya umma na kwamba ni dhambi kutumia mafanikio ya elimu yako kujinufaisha wewe mwenyewe na ndugu zako wa karibu pekee tayari imeshatoweka! Siku hizi msomi ni mali ya wazazi pamoja na familia yake

Tunaishi katika taifa ambalo viongozi wengi waandamizi serikalini wamekuwa wahubiri wazuri wa sera ya kujiajiri ilhali mioyoni mwao wanajua wazi kuwa miundombinu ya taifa hili si rafiki mwema wa ajira binafsi hasa kwa vijana.

Vigogo hawa wamekuwa wakiwashawishi vijana kuacha kuzunguka na bahasha mitaani na badala yake waende mashambani kulima ilhali watoto wao tayari wameshapachikwa katika idara na taasisi mbalimbali za umma isivyo halali. Tunaishi katika taifa ambalo watu wakiona changamoto mbalimbali zinazoikumba nchi wanaishia kunung’unika na kuilalamikia Serikali badala ya kutuliza akili na kuchukua hatua.

Watanzania walewale waliokuwa wakiushutumu utawala wa Rais Jakaya Kikwete kwamba haukuwa na makucha na kwamba Rais alikuwa mpole dhidi ya wahujumu uchumi na mafisadi kiasi cha kupelekea ombwe kubwa la uongozi, ni haohao wanaoishutumu serikali ya awamu ya tano iliyokuwa chini ya Rais John Pombe Magufuli kwamba aliendesha nchi kidikteta na kwamba alikiuka haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa kuwashughulikia hadharani wahujumu uchumi na mafisadi

Huu ni wakati ambao vijana tunapaswa kusimama na kulijenga upya taifa letu badala ya kulalamika na kushabikia mambo yasiyo na msingi. Serikali yetu imefanikisha mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka bandari ya Tanga mpaka Uganda.

Vijana tusisubiri mradi uanze ili tujazane kwa walengwa kuomba vibarua. Huu ni muda wa kusaka habari kuhusu maendeleo ya mradi huo kisha kulima matikiti, nyanya, na mchicha kwa wingi kwani ni dhahiri mahitaji ya vyakula yataongezeka.

Vijana tujipange na kuanzisha vikundi rasmi vya upishi kwani ni dhahiri maelfu ya vijana watakaoajiriwa watahitaji chakula kwa wingi katika maeneo yote yatakayopitiwa na bomba hilo. Tunaona jinsi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na mifuko mbalimbali ya hifadhi za jamii inavyojenga kwa wingi nyumba za makazi kwa wananchi hasa mkoani Dodoma.

Vijana tusibweteke na kushinda kwenye mitandao ya kijamii tukipiga soga na badala yake tuanzishe vikundi vya ufyatuaji matofali kisha tuisukume serikali iyabane mashirika haya kukubali kuingia mikataba ya kibiashara na vikundi vyetu.

Hivi karibuni taifa la Sudani Kusini limekaribishwa rasmi kuwa mwanachama mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa sasa jumuiya hii inakadiriwa kuwa na zaidi ya watu milioni 180.

Vijana tuache lawama kwamba hakuna masoko ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini, tuamke kwa pamoja na tulikabili kwa ujasiri soko la bidhaa la jumuiya hii yenye jumla ya mataifa sita sasa.

Shime watanzania, tujivunie amani na ukubwa wa taifa letu kwa vitendo. Tuache manung’uniko na tuyatazame matatizo ya taifa letu kama changamoto.

Taifa lenye changamoto nyingi na zisizoisha kila kukicha ni ishara ya fursa nyingi na zisizotumika kila zinapojitokeza.
 
Upvote 5
Wa Africa sijui vipi??tafuteni hela sasa ukubwa wa Tanzania una tija gani?mara cjui Mtu wa kwanza fuvu lake lilipatikana olduvai mara Adam na hawa walikuwa waafrica sasa haya yote yana faida gani??
 
Walimu na wasomi ambao wangeweza kuwaandaa vijana kukabiliana na maisha na mabadiliko ya uchumi na teknolojia wamekimbilia siasa.
Viongozi wanapoteza mitazamo ya kulinusuru taifa katika changamoto ya uhaba wa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi,kwa kushindwa kutenga fedha na kuwapeleka vijana wetu waende kusoma nje ya nchi ili kupata elimu itakiwayo kwa ajili ya kizazi kipya kitakachobadili Tanzania tuliyonayo sasa.
Viongozi wakiacha ubinafsi tunaweza kuitazama mipango yenye kunyanyua uchumi na maisha ya mtu mmoja mmoja:
1.Viongozi muda mwingi wapo katika kutafuta kiki badala ya kuwa wabunifu na kusimamia maendeleo ya nchi.
2.Bado viongozi hawajiulizi na hawapo tayari kujifunza kwa wenzetu kwa nini sisi kodi ipo juu,lakini wenzetu wanapitisha bidhaa hapa kwetu na kodi yao ipo chini, na wanaendesha uchumi.
 
kwa hiyo unamaanisha kubwa jinga?
 
2.Bado viongozi hawajiulizi na hawapo tayari kujifunza kwa wenzetu kwa nini sisi kodi ipo juu,lakini wenzetu wanapitisha bidhaa hapa kwetu na kodi yao ipo chini, na wanaendesha uchumi.
Hii ni moja ya maajabu ya Tanzania..
Mganda anaagiza bidhaa toka China, anazipokea bandari ya Dar es Salaam, anasafirisha kwa gharama kubwa umbali wa zaidi ya km 1000 hadi Uganda.

Mfanyabiashara wa Kariakoo anasafiri hadi Uganda ananunua hizo bidhaa anasafirisha kurejesha Dar es Salaam anauza na kupata faida!!!

Yaani badala ya waganda kuja kununua bidhaa Kariakoo kwa kuwa tuna advantage ya bandari, watu wetu ndo wanateseka kwenda kununua bidhaa Uganda kusiko na bandari🙄
 
Walimu na wasomi ambao wangeweza kuwaandaa vijana kukabiliana na maisha na mabadiliko ya uchumi na teknolojia wamekimbilia siasa.
Viongozi wanapoteza mitazamo ya kulinusuru taifa katika changamoto ya uhaba wa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi,kwa kushindwa kutenga fedha na kuwapeleka vijana wetu waende kusoma nje ya nchi ili kupata elimu itakiwayo kwa ajili ya kizazi kipya kitakachobadili Tanzania tuliyonayo sasa.
Viongozi wakiacha ubinafsi tunaweza kuitazama mipango yenye kunyanyua uchumi na maisha ya mtu mmoja mmoja:
1.Viongozi muda mwingi wapo katika kutafuta kiki badala ya kuwa wabunifu na kusimamia maendeleo ya nchi.
2.Bado viongozi hawajiulizi na hawapo tayari kujifunza kwa wenzetu kwa nini sisi kodi ipo juu,lakini wenzetu wanapitisha bidhaa hapa kwetu na kodi yao ipo chini, na wanaendesha uchumi.
Bora wanapata vibuyu vya asali hayo mengine hawana kazi nayo.
 
Back
Top Bottom