Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 373
- 829
Migogoro Wa Ardhi unaoendelea Ngorongoro umekuwa ukijengewa dhana kadhaa ili ikubalike na wengi.
Mara ni Mpango wa kuokoa uhifadhi, mara kulinda masalia ya wanyama, mara kulinda vyanzo vya maji, mara kulinda malikale (labda Wamasai wasikanyage fuvu la kale au nyayo labda wanadhani Wamasai ni so reckless) Wanasahau kabla ya wao kuona hizo nyayo Wamasai walikuwepo for centuries.
Hata hivyo ukweli ni kuwa, kuna makundi ndani na nje yana maslahi ya kifedha kwenye eneo la Ngorongoro- Loliondo.
Maslahi ya kifedha ya makundi hayo yamebatizwa kuwa ni maslahi ya taifa na rasilimali za taifa zinatumika kulinda maslahi ya makundi haya.
Hili swala la ardhi ya Ngorongoro tusilipe tafsiri isiyostahili. Tatizo sio mgogoro wa wahifadhi na wafugaji, mgogoro upo kati ya wafugaji na mawakala (mercenaries) wa taasisi za kibiashara katika sekta ya utalii.
Wala serikali ya Tanzania haina sera yeyote ya uhifadhi Tanzania. Nani anajua sera yeyote ya kupanda miti Tanzania ambayo ni endelevu? Prof Wangari alipanda mamilioni ya miti kule Kenya. Alikuwa na vision ya uhifadhi. Tanzania hatuna. Sisi Tanzania tunatunza na kuhifadhi mazingira na wanyamapori kama tutapata fedha. Bila fedha, hakuna lolote litafanyika. Kosa letu kubwa Wamasai tunatunza uoto wa asili na wanyamapori bila kuipa price tags 🏷️ .
Ndani ya miaka 14, Wizara ya Maliasili imekuwa na mawaziri wengi kuliko Wizara yeyote Tanzania na hakuna Waziri hata mmoja ambaye hakujifanya amezaliwa upya Kwa mapenzi na Ngorongoro baada tu ya kuteuliwa. Kwa sisi tuaofuatilia shughuli za hii wizara, utadhani waziri wa Maliasili ni Waziri maalum Kwa ajili ya Ngorongoro. Waziri akiteuliwa tu, kituo cha kwanza baada ya uapisho ni Ngorongoro na hakutani na wananchi. Anakutana na waratibu deal za fedha. Na wakija tu ni kuanzisha mgogoro wa ardhi. Ngoja niwaseme wachache