Masoki ya madini yapaisha mapato mkoa wa Geita

Masoki ya madini yapaisha mapato mkoa wa Geita

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
461
Reaction score
295
1577602391165.png

TANGU kuanzishwa kwa masoko ya madini nchini, mkoa wa Geita umeongeza ukusanyaji wa mapato kwenye sekta ya madini kutoka chini ya Sh bilioni moja kwa mwaka mpaka kufikia zaidi ya Sh bilioni 3.5 kwa mwaka.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko, alipokuwa akifungua Soko Kuu la Madini ya dhahabu Chato lililopo Buseresere Mkoani Geita.

Kwamba, soko hilo limefikisha idadi ya masoko 29 nchini na masoko nane yaliyofunguliwa mkoani Geita, ambalo kwa sasa lina ofisi 10 za madalali wanaonunua madini hayo.

Aidha, Waziri Biteko aliwataka maofisa wa serikali kutowasumbua wachimbaji na wafanyabiashara wa madini, wanapopeleka madini yao sokoni.

Pia, alisema mchimbaji au mfanyabiashara yoyote wa madini, haruhusiwi kukaa na madini nyumbani kwake, bila ya kuwa na nyaraka kutoka serikalini.

“Kipindi cha nyuma serikali ilikuwa inatoa leseni kwa wafanyabiashara bila kujua wananunua wapi wala wanauza wapi, ila leo wanunuzi wanajua wakanunue wapi na wakauze wapi. Haya ni mafanikio makubwa sana kwenye Sekta ya Madini na anayestahili pongezi si Wizara ya Madini wala si Doto Biteko, bali ni Rais Magufuli mwenyewe na wadau wa madini kwa kukubali kufuata sheria,” alisema Biteko.

Wakati huo huo, Waziri Biteko aliwataka wachimbaji na wafanyabiashara wa mkoa wa Geita, kufanya shughuli ya madini, kwa kufuata sheria, kue- pukaukwepajiwakodinaku- tunza kumbukumbu ili kuepuka usumbufu usio wa lazima.

“Wilaya ya Chato ina jumla ya leseni za uchimbaji mdogo 276 na ni ya tatu, baada ya wila- ya ya Geita yenye jumla ya leseni 630 na ya pili ni Bukombe yenye jumla ya leseni 376 za uchimbaji mdogo wa madini,” alisema.

Mwaka 2017 yalifanyika Marekebisho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, ikiwa ni jitihada ya serikali kudhibiti utoroshwaji wa madini nchini.

Kifungu 27C (1 na 2) cha Marekebisho ya Sheria hiyo ya Madini, kinaelekeza uanzishwaji wa masoko ya madini ambayo yana faida kubwa kwa wachimbaji, wafanyabiashara wa madini na Serikali kwa ujumla.

Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani alimpongeza Waziri Biteko kwa kazi nzuri anazozifanya.

Alieleza kuwa pamoja na maelekezo mazuri wanayoyapata kutoka kwa Rais, Wizara ya Madini imejipanga kuhakikisha inasimamia sekta ya madini kikamilifu na imeongeza pato la nchi kwa kiwango kikubwa.

“Tulilia sana soko la madini Chato, lakini leo tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kilio chetu kimepata majibu,” alisema Dk Kalemani.

Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Nchini (FEMATA), John Bina alimuomba Waziri Biteko kuendelea kuwapa wachimbaji wadogo maeneo ya kuchimba.

Aliipongeza serikali kwa kugawa transfoma saba kwa wachimbaji wadogo kila mkoa.
 
Kwa hiyo Dreamliner mpya ya Taslim yaja?
 
Back
Top Bottom