Story hii inahusu changamoto ya elimu Tanzania(ubora na masomo ya ziada).Nimeambatanisha Nakala ya somo husika
-
MASOMO YA ZIADA NA UBORA WA ELIMU
Katika maisha yangu ya elimu suala la masomo ya ziada ni sehemu ya asilimia 10 tu ya mafanikio yangu ya elimu. Kwani niliwahi kusoma masomo ya ziada katika ngazi yangu ya elimu mwaka mmoja kwajiri ya kufanya mtihani kama mtahiniwa binafsi wa kidato sita kwa sababu sikuwa na kipato cha kutosha kusoma miaka miwili, Naamini kwamba masomo ya ziada ama tuition ni kwajiri ya wanafunzi wenye kipato kidogo na wanaosoma katika baadhi ya shule za serikali zenye walimu wachache.
Binafsi licha ya kusoma katika shule ya serikali yenye walimu wachache na miundombinu mibovu sikuweza kusoma masomo ya ziada kwa sababu niliamini juhudi binafsi na kusoma kwa bidii ningefanikiwa. Licha ya hapo niliamini pia katika kupunzisha akili ni muhimu.Kujifunza na kujishughulisha mambo mengine yasiohusu taaluma ni muhimu na ndio maana ya kuwa na likizo.
Masomo ya ziada ama tuition yamekuwa yakionekana kama kimbilio la wanafunzi wengi huamini kwamba njia hii inatoa fursa na ahuane kwa wanafunzi kufanya vizuri katika masomo na mitihani ya mwisho wanafunzi wengi kufanya vizuri katika masomo yao hasa katika mitihani yao ya mwisho.
Licha ya kufaulu wengi wao wanafundishwa namna ya kujbu mitihihani na si kuelewa, mfumo wetu wa elimu unaamini katika matokeo na sio maarifa. Hii huchangia wanataalumu wengi hasa katika elimu ya juu kutojitambua na kuwa na maarifa kidogo linapokuja suala la utendaji wakiwa wameshaajiriwa ama kufanyiwa usahili, hujikuta hawana uelewa haswa linapokuja swala kuchakata maarifa kwa vitendo. Haya yote pia huchangiwa na mfuno wa elimu yetu ya Tanzania unao amini katika kukalilishwa na mpango wa kuashiria (narking scheme).
Kati ya nchi zenye mfumo bora wa elimu hasa shule za awali na upili na hata elimu ya juu duniani ni Finland. Nchi hii ina viwango bora vya elimu dunia kwa sababu walitambua mambo yafuatatayo kama nchi yetu tungeyafanya elimu yetu ingengua bora :-
Hakuna majaribio ama mtihani wa kitaifa, hawana mtihani wa kitaifa kwa ujumla kwa sababu njia pekee ya kupima wanafunzi wao hasa shule za msingi ni kujaza viputo, kujaza maswali yaliowekwa kwenye makopo hii husaidia kupata umahiri wa mwanafunzi katika somo Fulani pia huwa mtihani wao wa mwisho hutungwa na mwalimu anayemfundisha. Ningependekeza serikali ijaribu kujikita namna hii kwa sababu husaidia kutambua vipawa na mapenzi ya mwananafunzi katika somo Fulani
Uwajibikaji kwa walimu daima hauhitajiki, suala la walimu sio tatizo hata kidogo kwa sababu walimu wote wanatakiwa kuwa na shahada ya uzamili(master’s degree ) kabla ya kuingia katika taaluma hio. Hata hivyo tofauti na nchini Tanzania uchaguzi wa ualimu nchi ya finland ni mgumu sana tofauti na nchini ambako mtahiniwa yeyote akimaliza shule ya upili anaweza kuingia katika taaluma ya ualimu. Finland inaamini kwamba ikiwa mwalimu atakuwa yeyote pasipo kutazama ubora wa mwalimu tutegemee mwanafunzi pia kufanya vibaya. Kwahiyo lawama haziwezi kumfikia mwalimu sababu ya kuwa na mfumo mkali na mchujo wa walimu. Finland inaipa somo ulimwengu kwamba taaluma haipaswi kuchukulia poa. Nchi yetu iwekeze katika kuwatafuta walimu bora pamoja na maslahi bora ili wanafunzi wapate huduma bora ya elimu.
Ushirikiano sio ushindani, katika nchi yingi ulimwenguni hasa hapa Tanzania tunaamini elimu katika ushindani, tunaamini matokeo ya kitaifa ndo yanayopima ubora wa mwanafunzi kitu ambacho ni tofauti kabisa na nchi ya finlandi. Tunaamini katika nadharia ya “Darwin” ya ushindani, wakati nchi hio inaamini kwamba “washindi halali hawashindani”. Mfumo wa elimu wa finiland hautegemei sifa bali ushirikiano wa kutafuta maarifa . hakuna orodha ya shule au walimu waliofanya vizuri zaidi. Hivyo husaidia kugundua kipawa halisi cha kila mmoja. Yakitengenezwa mazingira ya ushindani watakosa washindi halali ambao hawataki kushindana.
Kuwa na vipaombele vya msingi, usawa ni kitu cha msingi katika utoaji wa elimu katika jamii hivyo kuifanya jamii Fulani ipokee elimu bora kuliko jamii Fulani hio ni moja kikwazo nchini Tanzania. Wanafunzi wanatakiwa wapokee chakula cha bure shuleni pasipo na upendeleo, usawa wa kupokea huduma za afya, ushauri wa afya ya akili ama saikolojia pamoja na mwongozo wa mtu binafsi. Kazi chache za nyumbani na kazi ndogo za nje. Wanafunzi hawapaswi kuwa na kazi nyingi za nyumbani. Hivyo wanatakiwa kuwa na muda wa kutosha wa kupunzisha akili na kufanya mambo mngine yasiohusu taaluma. Nimeshudia wanafunzi wengi kuwa na kazi nyingi za nyumbani hivyo hawapati muda wa kupunzika.
Maelekezo thabiti kutoka kwa walimu walewale, kuna walimu na wanafunzi wachache sana nchini humo wanaobadilishwa. Huwezi kutarajia kuona nyuso zisizoonekana na mafanikio kwao kwa kiwango cha mtu binafsi. Wanafunzi nchini humo huwa na mwalimu sawa kwa hadi miaka sita ya elimu yao, wakati huohuo mwalimu anaweza kuchukua nafasi ya mshauri au hata mwanachama wa familia. Kwa muda huo kuaminiana na mashirikiano hujengwa. Mwanafunzi kuona walimu tofaut itofauti katika kipdindi kifupi si afya ya elimu kwani huathiri uelewa na ufahamu wa mwanafunzi.
Kutoa chaguzi za kitaalamu zaidi ya shahada ya kawaida ya chuo kikuu. Nchini Finland kuna shule ya upili ya juu ambayo ni miaka mitatu ambayo inamwandaa mwanafunzi kuhitimu mtihani ambao hutambua kukubaliwa kujiunga na elimu ya chuo kikuu. Hufanya hivi ili kutambua ujuzi mahususi alioupata wakati akiwa shule ya upili, Tena kuna elimu ya ufundi stadi anbayo ni program ya miaka mitatu inayo wezesha wanafunzi kuwa na taaluma mbalimbali za ufundi. Pia wanafunzi wanachagua kufanya mtihani ikiwa wanataka kujiunga na elimu ya chuo kikuu au kuendelea na elimu ya ufundi.
Binafsi sioni mabadiliko katika elimu ya Tanzania, makosa yanajirudia si mzazi wala mwalimu wala serikali wakipambana kuboresha elimu yetu. Napendekeza kwamba elimu hasa ya awali isiwe ya ushindani bali wanafunzi wawe washindi, matokeo ya mwisho ya mtihani wa taifa isiwe kipimo cha ujuzi na maarifa ya manafunzi bali mwalimu wake anayemfundisha ndo atambue, wanafunzi wapate muda wa kupunzika hasa wakati wa likizo au kujifunza kitu kipya mfano wajifunze elimu ya TEHAMA kama tuition wakati wa likizo kwasababu teknologia inakuwa kwa kasi hivyo basi tusiruhusu itupite na pia vituo elimu ya TEHAMA vijenge vingi, ubora wa walimu na maslahi uzingatiwe sana, maarifa na ujuzi wa mwanafunzi uzingatiwe pia.

Attachments
Upvote
3