Mason Greenwood aondolewa kwenye bidhaa za FIFA

Mason Greenwood aondolewa kwenye bidhaa za FIFA

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mchezaji wa soka wa Manchester United Mason Greenwood ameongzewa mda zaidi wa kushikiliwa kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono na kutoa vitisho vya kuua.

Mchezaji huyo mwenye miaka 20 alikamatwa kwa tuhuma za ubakaji na shambulio siku ya jumapili.

Polisi wa Greater Manchester Police (GMP) walisema wamepewa muda zaidi wa kumhoji baada ya kuongezewa muda hapo awali hadi Jumatatu.

Manchester United imesema hatachezea klabu hiyo hadi itakapotangazwa tena.

GMP ilisema mchezaji huyo alikamatwa siku ya Jumapili baada ya kikosi hicho "kufahamu kuhusu picha na video za mitandao ya kijamii zilizotshirikishwa na mwanamke akiripoti matukio ya kushambuliwa kimwili".

Ilisema hakimu aliwaongezea muda kwa mara ya pili kuendelea kumzuia hadi Jumatano.

Manchester United ilisema klabu hiyo "haikukubali vurugu za aina yoyote"Image caption: Manchester United ilisema klabu hiyo "haikukubali vurugu za aina yoyote"

Msemaji wa jeshi alisema uchunguzi unaendelea na mwanamke mmoja "anapewa usaidizi wa kitaalam".

Waundaji wa mchezo wa video EA Sports walisema Mshambuliaji huyo ameondolewa kwenye bidhaa za FIFA.
 
Kubaka ni kosa kisheria. Aende jela tu kama atapatikana na hatia. Kama huko uingereza kuna timu ya magereza aichezee. Maana tayari wameshamsajili Mendy beki wa city.
 
Back
Top Bottom