Masoud Kipanya alimaanisha nini kwenye mchoro huu?

To me: Hilo skeleton ni MZEE(r.i.p)
Draft ni serikali
Kete ni utawala
Mwanamke ni huyu([emoji1780])
Hilo jipu mkononi mwa Mwanamke
NI MATATIZO YA KIUTAWALA
GLASS ya wine(damu zilizomwagika
Kuna mzee hapa jirani yangu ananikata jicho na anamwonekano wa kikauzu ngoja niishie hapa kwanza....
 
Umesema kweli mkuu, huyu jamaa amepoteza mwelekeo, kazi iliyo baki ni kukashifu na kudhihaki, nadhani hii yote ni njaa, anaona bila kuchora katuni za kukashifu na kudhihaki hawezi kupata mafao ya kutosha.
sasa atajimaliza mwenyewe
mbona mnachachamaa vipi?
 
Kweli Kipanya ni akili kubwa sana! Hapa ni kuwa Rais Samia amewafufua wanyonya damu (wapigaji) walikuwa wameshakufa na kuoza (baki mifupa) na sasa kupitia kofia ya CCM wameanza kula maisha (vuta sigara na kunywa nao jasho la Watanzania/ damu kwenye glass) ! Rejea teuzi za January Makamba na Bodi ya ajabu ya TANESCO ambayo January amejaza " wapigaji" ambao Rais Magufuli alishawamaliza kabisa!
 
Wengi hamjaiona hiyo bangi kwenye draft upande wa huyo mwenye "SILAHA"

Hii picha ni kubwa sana, ukimsikiliza Gentamycine hapo juu "UNAPOTEA"

MUNGU Mwenyezi na ATUSAMEHE.
 
Hapo Yanga na simba wanashindania makombe na pia hilo skeleton ni ile kesi iko CAS wakati wowote kinalipuka .
 
Hii ni katuni bora kabisa so far kutoka kwa Kipanya.

Natumaini kuna mahali anaandika na kutunza tafsiri zake za katuni anazochora. - Na anafuatilia juhudi za wadau wanaojitahidi kutoa tafsiri za kazi zake.
 
Kuna wanywa damu zaidi ya ccm ya 2015-2021?
 
Naungana na wewe..nimetafsiri hivi pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama anacheza panga, pangua kuitokomeza Kambi ya marehemu mwendazake wakati hiyo Kambi haipo tena, ilibadirika na kuwa kitu kingine....
Chama kipya cha siasa chenye kumuenzi mbabe wa fitina za Tanzania soon kinakuja!

Chama kipya? Kitachukuaje mamlaka ya dola (polisi, jw, tiss, magereza, uhamiaji, Hazina/BOT) toka kwa CCM? Kitapindua nchi?

Bila hivyo kitaishia kuwa kama TLP au UDP.

Jeuri ya mbabe wa fitna iliwezeshwa na nyenzo za dola zinazomilikiwa na CCM. Bila hizo, nje ya CCM, angekuwa kama Mrema au Cheyo.
 
Nimtishe namuelekeza,kama ana ndugu wanampenda wamwambie,asije sema hakuambiwa,uhuru usitumike kuvuka mipaka

Ungekuwa unamfahamu kipanya, usingepoteza muda kumtolea kitisho cha aina yoyote. Ukiona katuni zake hazikufurahishi, just ignore him.
 
Ilo skeretoni ni rahisi kulihusisha na JPM cos alishafariki laiki ukitoa ilo hakuna kitu kingine ambacho unaweza kukihusisha na JPM hapo! Binafsi naona Mama yuko na Mafia fulani ndani ya chama chao.
Ni uyo uyo Jiwe.
 
Ungekuwa unamfahamu kipanya, usingepoteza muda kumtolea kitisho cha aina yoyote. Ukiona katuni zake hazikufurahishi, just ignore him.
Sawa,ila anachofanya sio poa kwa afya yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…