Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MASOUD MASOUD: NIMEMKOPESHA PIMA KANILIPA SHUBIRI
Nimetembelewa na Bi. Mboni wa "Mboni Show," kuna historia alikuwa anataka kuisikia kutoka kwangu kuhusu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nje ya jukwaa la siasa.
Bi. Mboni ana hamu ya kunisikia nikumuhadithia Mwalimu akiwa mitaa ya Kariakoo ya 1950 mathalan Mtaa wa Mvita nje ya ofisi ya TANU usiku akiwasikiliza Egyptian wakipiga taarab kuwaburudisha WanaTANU.
Basi tukawa katika mazungumzo haya ndipo nikamtaja Bi. Nuru bint Sudi mwimbaji maarufu wa nyakati hizo.
Bi. Nuru alipata kuimba na Al Watan na Egyptian vikundi viwili maarufu na mahasimu lakini si maadui.
Ushindani wao upo katika utunzi wa nyimbo, uimbaji na upigaji wa ala.
Lakini nani leo anamjua Bi. Nuru?
Hapo ndipo nikamtaja Manju Masoud Masoud.
Bingwa asiye na mpinzani.
Nikamshauri Bi. Mboni akamuone Manju Masoud Masoud atapata historia ya Bi. Nuru bint Sudi na historia ya Al Watan na Egyptian.
Sikujua kuwa nimechokoza sege la nyuki.
Sikujua kuwa nimekopesha pima nitalipwa shubiri.
Nilipeleka kadha nimelipwa kadha wa kadha na nyongeza juu iliyopambwa na kisunzu chenye ushungi.
In Shaa Allah Msome Masoud Masoud hapo chini tena kwa tahadhari:
"I feel very much humbled.
Mohamed Said ni kati ya watu wachache nchini humu ninayeona fahari kuishi zama ambazo yupo hai.
Pamoja na kuwa na Darja kubwa Kiuandishi na Kihistoria ni Malenga mbobezi aliyetamalaki katika kazi zake zote.
Ni wazi hakuwa na "choice" bila shaka ni Allah mwenyewe alimpendelea na kumpa Neema ya fahamu alizompa.
Unamuona kila akizungumzia taarikh ya jambo lolote limjialo analichambua kwa "passion."
Na ukimsikiliza utagundua anayaona mambo kwenye jambo alisemalo wengine sisi hatuyaoni.
"He is an epitome of absolute genius living amidst a people of paralysing stupidity and cheerleaders of mass imbecility.
May God grant him more wisdom and a noble life."
Masoud Masoud