Masoud Sura Mbaya

Keykey

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2006
Posts
3,251
Reaction score
747
Mwanaume Alivyotumia Sura Mbaya Kupata Umaarufu, Marafiki

Imeandikwa na Kaanaeli Kaale; Tarehe: 14th September 2009




Masoud Sura Mbaya kama anavyojulikana sasa ni msanii ambaye alivuma miaka ya 90 baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya mwanamume mwenye sura mbaya.

Kwa mara ya kwanza alishiriki katika mashindano ya wanaume wenye sura mbaya yaliyofanyika Buguruni Dar es Salaam na kuibuka mshindi wa kwanza ambapo alipata zawadi ya redio.

Mashindano hayo ya kusisimua yalifanyika kwa mara ya pili katika Wilaya ya Kinondoni ambapo, Masoud aliwashinda wasanii wengine maarufu wakiwamo mwanamuziki wa siku nyingi Remmy Ongala na msanii maarufu wa vichekesho Khalid John, maarufu kama Mzee Jangala.

Masoud anasema anaamini kuwa hakuna mwanamume mwenye uwezo wa kumnyanganya nafasi hiyo nchini Tanzania kwa kuwa ana uwezo wa kubadilisha sura yake kwa kutumia hisia mbalimbali. Mimi ni sura mbaya nambari wani Tanzaniawa kunishinda hajapatikana.

Wapo waliojaribu kukata rufaa kupinga ushindi wangu lakini niliwashinda hata kwenye rufaanajivunia ushindi wangu na kila ninapojiangalia kwenye kioo naona wazi kuwa nina haki ya kushinda, anasema Masoud.

Ingawa hivi sasa anajivunia sura yake, maisha yake ya utotoni hayakuwa ya furaha kwa kuwa alichukizwa na tabia ya vijana wenzake waliopenda kumtania kwa kumuita sura mbaya. Kitendo hicho kilimsababishia hasira za mara kwa mara na kujiona mpweke.

Masoud alishiriki pia katika mashindano ya pili ya kumtafuta mwanamume mwenye sura mbaya ambayo yalifanyika Kinondoni na kupata zawadi ya TV baada ya kuibuka mshindi wa kwanza.

Baada ya ushindi huo, Ongala alikata rufaa na kudai kuwa Masoud alipendelewa. Hata hivyo Masoud alishinda katika rufaa hiyo jambo lililomuongezea umaarufu.

Kuanzia kipindi hicho amekuwa akishiriki katika matamasha ya wasanii mbalimbali na sherehe ambapo watu humkodisha ili atoe burudani.


SOURCE: HabariLeo
 
Last edited:
Jamaa hakika amebeba sura! Ee bwana, Mungu hamnyimi mtu vyote. Hatakupa hiki lakini atakupa kile!

Jamaa hakupewa sura nzuri lakini kapewa vipaji tele vya kufurahisha wengine. "Usura mbaya" wake umekuwa chanzo cha furaha kwa wengine. That's great.
 
Kaanaeli naye yaani kakosa vitu vya kuandika kweli huu mwaka anaturudishia story za miaka kibao ya nyuma!!
 
amani acha aandike sisi wengi hatujasikia bado
 
nakumbuka Dr Remmy alidhani angeshinda mpambano ule,ila mtoto wa Bonga Bar akamuonyesha kuwa Remmy alikuwa bonge la handsome:hand:
 
huyu kweli alichakachua ushindi marehemu remy ilikuwa nafasi yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…