Massey Ferguson 290 4WD na FORD 8210

Anithape

Senior Member
Joined
Nov 14, 2018
Posts
131
Reaction score
136
Nina option ya kukopa tractor mojawapo kati ya haya mawili. Yote ni used, yapo Denmark. Wajuzi wa matrekta na wazoefu wa kilimo, naombeni ushauri, kati ya trekta hizo mbili, nichukue ipi ili niweze kulimia bongo?

Tafadhali: Ni kati ya model hizo mbili tuu. Maana watakuja wasukuma utawasikia, oooh, tafuta john deer, wengine ooh, kamata swaraji.

Ni kati ya MF 290 4WD na FORD 8210, nayo pia ni 4WD.
 
Mkuu tractor hizo ,zote mi naona zipo vizuri sana,nami natafuta tu hela nivute massey mwakani,
 
Zote ziko makini shambani ila napendekeza MF 290 maana spare parts zake zinapatikana kwa urahisi sana na ziko imara sana zinavumilia mikiki miki sana,mkuu ukipata unijulishe na Mimi nataka kupata mashine kama hiyo.
 
Mimi sina uzoefu nayo ila rafiki yangu ambaye ni Fundi mzuri tu, kaniambia kuwa
MASSEY ni nzuri zaidi, kwani kwa ubora zote ni nzuri ila advantage ya Massey ni kuwa ina spare nyingi hapa nyumbani kuliko Ford
 
Jamiiforum ukiomba ushauri wa kununua gari, utapeqa ushauri wa spea

Sent using Jamii Forums mobile app
Usichangaje habari; Mtoa mada ametoa choice mbili tu ambazo zote ni nzuri zina nguvu, uimara na pengine niseme Massey alitumia babu hata mjukuu anatumia. Nimeangalia spec zake sijaona cha tofauti sana hivyo nikaona
kinachotoa tofauti kubwa kwa mjasirimali ni upatikanaji wa spare...

Kama unafikiri ushauri wa spare sio muhimu, jaribu ununue gari aina ya Jeep (used) au hata Benz uone moto wake. Spare zake huwezi chonga; Mbona kuna aina nyingi tu za magari hazina spare hapa Tanzania? ukitaka taa yake tu ni hadi uagize ulaya? mtu anaye nunua used ataweza?
Think positive brother acha ushabiki usio kuwa na maana!!!!
 
Wote wanazungumzia spea tu

Sent using Jamii Forums mobile app


Wewe una uzoefu na trekta?

Kama unao au huna, ni kwamba huwezi kuzungumzia ubora wa trekta bila kuzungumzia upatikanaji wa spear zake na uimara wa spear husika. Kuna matrekta yadadumu miaka miwili menngine mmoja au mitatu then ndiyo unabadili spear. Being ya spear, uimara na upatikanaji ni suala muhimu sana.
 
Tractor za Ford na Massey furguson Tuone Tunazo kuanzia kubwa six cylinder heavy duty 42m
Mpaka ndogo 4cylinder heavy duty 17m karibuni 0762612213
 
Mkuu hapo juu MF 390 , 4 WD,75 HP mnauzaje used ? Na zinakuwa kutoka UK ? Tafadhali mwenye uzoefu na hizi trekta ,ni trekta ipi ya MF 390, 4WD kutumia kwa ardhi ya maeneo mengi inatakiwa ya HP ngapi ili km mjasiliamali unayeanza ikupe faida ya kulima mashamba yako na mashamba ya watu wengine kwa malipo ? Mwenye uelewa na hili naomba anifahamishe tafadhali.
 
Kwa ardhi ya kikwetu haijalishi uko kigoma au dar kwa kuanza chukua kuanzia hp75 4wd.
Kingine kwangu kuliko ninunue mtumba cash bora ninunue hata john deere 75hp toka lonagro kwa mkoppo kwa kutanguliza asilimia 35 then inayobaki nalipa kwa miaka mitatu
 
John Deere ya ukweli mpya ya HP75 huwezi kuipata chini ya milioni 80 Tsh.

Hizo John Deere za HP75 za Lonagro za china/ india/pakistani, hata ukipewa kumi mpya, au ukipewa used massey ferguson ya uk ya hp 75 moja, basi chukua massey ferguson.
 
C
John Deere ya ukweli mpya ya HP75 huwezi kuipata chini ya milioni 80 Tsh.

Hizo John Deere za HP75 za Lonagro za china/ india/pakistani, hata ukipewa kumi mpya, au ukipewa used massey ferguson ya uk ya hp 75 moja, basi chukua massey ferguson.
Nakubaliana na weww kuhusu 5075e ambayo ndo yanatangazwa na lonagro. Kwa ujumla zile tractor zimetengezwa kwa ajili ya kushindana na kubota maana hapo zaman john deere alikuwa kawekeza sana kwenye kuanzia hp 80 ambapo kubota alikuja akampiku. Lakin wanamatoleo mengine yanayotengezwa marekani ambalo moja tu linaanzia 56396usd na ujumla kwa sasa hatujawa na uwezo wa kununua tractor original toka ulaya iwe massey,case,valta, deutz na wengine weng, maana hata hao massey ferguson zao za ulaya tu si chini ya usd 40000. Hii ni bei ya dealer ambayo anatakiwa auze.
Nilikuwa naangalia planter tu zinacheza usd50000 kupanda juu.
Hoja yangu ni kuwa kwa sasa ambapo uchumi wa kilimo haujakaa vyema na kama mtu unataman kuja kuwa mkulima mkubwa ni bora utumie hata hizo za india kuliko kutumia used maana ukija piga gharama ya matengenezo ya kuhudumia tractor iliyochoka ni kubwa hata resale value yake inakuwa ndogo.
 
Cheki na New Holland pia iko vizuri. Nililima na Massey vs New Holland, New Holland inafunika mpaka raha jani lotee linazikwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…