marcoveratti
JF-Expert Member
- Sep 21, 2017
- 1,019
- 1,824
KWA wanasoka wa kizazi hiki cha sasa, kuonyeshwa kadi kwenye mechi ni jambo la kawaida sana. Kutokana na waamuzi wa mechi kuwa wakali sana hasa kwenye Ligi Kuu England, ndio maana kimekuwa kitu cha kushangaza kama itatokea mechi yote inachezwa bila ya kuwapo na kadi hata moja kuonyeshwa.
Lakini, kuna wachezaji hao, wamecheza mechi kibao kwenye soka, lakini hawajawahi kuonyeshwa kadi nyekundu hata mara moja, ambapo wengine wamestaafu na baadhi yao bado wanakipiga hadi sasa.
1.RAUL GONZALEZ
-Staa wa Kihispaniola, Raul Gonzalez alikuwa matata sana kwenye enzi zake za uchezaji. Staa huyo amedumu kwenye soka kwa miaka 18, lakini nidhami yake ilikuwa kubwa sana kwa sababu hajawahi kuonyeshwa kadi yoyote nyekundu. Raul alifunga mabao 388 katika mechi 932 alizocheza kwenye ngazi ya klabu, huku mabao yake mengine 44 akifunga kwenye timu ya taifa. Alibeba mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mara kadhaa pia huku akiwa na mataji mengine ya ubingwa wa Hispania. Lakini, kitu kikubwa hajawahi kuonyeshwa kadi nyekundu.
2.PHILIPP LAHM
-Usishangae. Philipp Lahm alikuwa beki wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani. Kwa sasa amestaafu. Lakini, kwenye kipindi chake cha uchezaji, huko Bayern Munich alitumika kama beki wa pembeni na wakati mwingine aliwekwa kwenye kiungo ya kukaba. Kitu kinachovutia ni kwamba kwa mechi zote alizocheza 652 kwenye klabu yake na 113 kwenye soka la kimataifa, Lahm hajawahi kuonyeshwa kadi nyekundu licha ya kwamba, amekuwa akicheza kwenye eneo ambalo kimsingi kuonyeshwa kadi ni kitu rahisi kutokana na kuwakabili washambuliaji, ambao wengine ni wasumbufu kweli kweli uwanjani.
3.KARIM BENZEMA
-Mshambuliaji Karim Benzema ameonyesha kuwa na nidhamu kubwa sana ndani ya uwanja na ndio maana kwa muda ambao amedumu kwenye kikosi cha Real Madrid kwa sababu hajawahi kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mechi yoyote. Benzema amecheza mechi kibao kwenye kikosi hicho cha wakali wa Santiago Bernabeu ameonyeshwa kadi tano tu za njano na hajawahi kuonyeshwa kadi yoyote nyekundu na hivyo kuwa na rekodi bora kabisa katika maisha yake ya soka. Benzema ndiye Mfaransa anayeongoza kwa mabaoa kwenye kikosi cha Real Madrid na ameitumikia timu hiyo kwenye mechi zaidi ya 200.
4.RYAN GIGGS
-Amecheza mechi 963 kwenye kikosi cha Manchester United na kwenye idadi hiyo mechi 672 za Ligi Kuu England na 157 za michuano ya Ulaya. Staa huyo amedumu kwenye kikosi cha Man United kwa miaka 24 na kitu kinachovutia zaidi ni kwamba hajawahi kuonyeshwa kadi nyekundu. Kwenye soka la klabu, Giggs hajawahi kuonyeshwa kadi nyekundu, mara moja tu alionyeshwa kadi nyekundu ilikuwa kwenye timu ya taifa ya Wales, tena kadi hiyo ilikuja baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwenye mechi dhidi ya Norway kuwania kufuzu Kombe la Dunia.
5.ANDREAS INIESTA
-Fundi wa mpira wa Kihispaniola, Andres Iniesta ambaye kwa sasa ameamua kuachana na klabu yake ya Barcelona na kutimkia huko Asia. Iniesta amebeba mataji mengi sana kwenye soka lake la ngazi ya klabu na timu ya taifa. Staa huyo amecheza zaidi ya 850, lakini kitu cha kuvutia ni kwamba hajawahi kutolewa kwa kadi nyekundu.
[Source www.instagram.com/mwanaspotiapp]
Sent using Jamii Forums mobile app