MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Nawasalimu kwa jina la Chama Cha Mapinduzi.
Naandika nikiwa na huzuni zilizochanganyikana na hasira kali. Jana hata leo kinacho-trend mitandaoni ni matangazo ya mkutano mkubwa wa injili. Ni kwamba kinachofanya hili jambo liwe kubwa ni baada ya watangazaji kuweka matangazo mji mzima bila kuacha sehemu yoyote. Nawapongeza mno waandaaji kwa ubunifu uliopitiliza.
Watu mitandaoni kama kawaida wakaanza kupost memes kuhusiana na hayo matangazo. Wengi ilikuwa ni katika hali ya mizaha. Kilichonihuzunisha ni kuona baadhi ya watu maarufu wakiwemo wasanii wakiingia mkumbo wa kupost hizo meme ambazo zina hilo tangazo.
Walichofanya ni ukosefu wa akili na kutojua thamani yao kibiashara. Ni kwamba wamewatangazia bure waandaaji wa mkutano bila wao kujua.
Hii inaonyesha bado nchi ina rundo la wasanii vilaza ambao wameshindwa kwenda sawa na ulimwengu wa kibepari.
Wasipojirekebisha tutegemee wasanii mamilionea kuendelea kubaki wachache ambao ni kina Diamond, Shilole, Young Lunya, Nuhu Mziwanda, Ali Kiba, Jux, Moni Centrozone, Malkia Karen, Official Nai pamoja na Ray Kigosi.