Mastaa wa filamu waliolazimishwa kuingia kwenye fani

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Tofauti na akina Johari,Ray,marehemu Kanumba (RIP), Cathy,Mainda na wengine kibao ambao waliingia kwenye fani ya uigizaji kwa mapenzi yao, hali hiyo ipo tofauti kwa baadhi ya mastaa ambao wapo kwenye fani hiyo kwa kulazimishwa.

1. JB
Huyu kwa sasa ni msanii mkubwa wa filamu , ila wengi hawajui kuwa aliingia kwenye fani baada ya kulazimishwa na swahiba wake wa kitambo hicho Single Mtambalike (Richie), JB mwenyewe aliwahi kukiri alikuwa akifanya mazoezi ya kuigiza miaka ya 98 ili kumridhisha swahiba wake, ila hakuwa na mapenzi na fani hiyo.Anamiliki tunzo ya muigizaji bora wa kiume.

2. Irene Uwoya
Mbali na kushinda tuzo ya muigizaji bora wa kike mwaka Jana, hakuwahi hata kuota kama ipo siku atakuja kuwa muigizaji, kipaji chake kiligunduliwa na muigizaji mwenzake Lucy Komba(Lona) , baada ya kukutana nae njiani na kumuomba aigize kwenye filamu yake. Sasa hivi ni tishio kwenye ulimwengu wa filamu.

3. Rose Ndauka
Star wa movie ya Swahiba , ambaye alilazimishwa kuingia kwenye fani hiyo na msanii mwenzie Richie, ambaye hapo awali alikuwa akimtumia kwenye movie zake kadhaa kabla ya kuamua kusimama mwenyewe, sasa ivi ni bonge la star.

4. Wema Sepetu.
Ni miss Tanzania 2006, ambaye aliingia kwenye ulimwengu wa filamu kwa shinikizo la marehemu Kanumba, pengine hii haikuwa fani yake maana toka Kanumba amefariki hajawahi kuonekana kwenye movie kama hapo awali, japokuwa amekuwa akifanya vizuri kwenye filamu.

5. Patcho Mwamba
Huyu jamaa alitokea FM academy, alikuwa rafiki wa marehemu Kanumba, ambaye ndiye aliyemuingiza kwenye fani ya uigizaji, japokuwa hakuwa na ndoto hizo, naye pia anafanya vizuri kwenye Game.

6. Jackline Wolper
Ni star anayefanya vizuri kwenye soko la filamu apa bongo, naye huyu hakuwa na ndoto za kuwa muigizaji, marehemu Kanumba aligundua kipaji chake ambapo alimchezesha movie kwa Mara ya kwanza , movie inaitwa Red Valentine, ambayo ilimpa umaarufu hadi Leo.

7. Rammy Gallis
Huyu jamaa aliingizwa kwenye fani Mara ya baada ya kufananishwa na marehemu Kanumba, yupo kwenye kampuni ya the great ya marehemu Kanumba, naye pia anafanya vizuri sokoni, naye hakuwa na ndoto za kuwa muigizaji.

8. Nargis Mohammed
Huyu aliwahi kuwa miss Tanzania, naye hakuwahi kuwa na ndoto za kuwa muigizaji, Ray alimforce akaingia ulingoni, hata hivyo hakudumu sana kwenye game kwani hadi sasa amewahi cheza movie tatu tu, naona ameona uigizaji sio fani wala ndoto zake hivyo kaamua kujiweka pembeni.

9. Lulu Michael
Huyu alishawahi kukiri kwenye Moja ya interview zake kuwa hakuwahi kufikiri wala kuota kuwa muigizaji, kipaji chake kiligunduliwa na dokta Cheni toka akiwa na umri dogo, sasa hivi anamiliki tunzo ya Ziff kama muigizaji bora wa kike.
 
Hivi King Majuto aligundua kipaji chake mwenyewe au alilazimishwa pia
 
Umesahau na Kajala pia kaingizwa na Marehemu the great.

Kulwa Kikumba naye a.k.a Dude naye anahadithia mara nyingi alipenda kuwa baunsa wa milangoni ila akina Dr. Cheni walimfosi kucheza scene mojs na kumpa elfu kumi akanogewa.
 
siku hizi ukishakuwa star tu na wewe unaweza kuigiza filamu ya kibongo hitaji kipaji wa la kuwa na uwezo wa kuigiza
 
Irene Paul, Zimwi, Jengua, Chikoka, Rado, Matovolwa, Shija, et al hao wote wanalazimisha kuigiza tu
 
mkuu, fuatilia vizuri historia ya ray.. alishakiri kwenyewe kuwa hakuwa na wazo lolote kuhusu filamu..

yeye pia alilazimishwa na richie richie enzi hizo.. tena akapewa jina la ray ray ili liwiane na la richie richie...

bongo movie ukiwa na pesa, halafu ukawa na sura inayokubali make ups, wanakubeba tu tofauti na nollywood!

cc. warumi
 
Last edited by a moderator:

OK , najua watakuwa wengi but mm nimeandika ambao Nina ushahid nao , sikufutilia ray kaingiAje, thanks kwa hilo Excel
 
Last edited by a moderator:
Huyu dada huwa sivutiwi na uigizaji wake,kweli analazimisha fani halafu km ana utoto flan hivi

Huyu anapendeza akiigiza kubwa jinga au tahira kuna jamaa anaitwa rammy galis kila siku anachambwa location kuwa hajui kuigiza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…