Mastaa wa kike wa Tanzania na mwisho mbaya katika mahusiano!

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Kidogo wandugu tuchemshe bongo kwa hili ambalo limenitatiza bila kujua nini hasa shida.

Hebu chukua Mdada Mtanzania ambaye bado hajawa star,Celebrity Ktk Muziki,bongo movie ,utangazaji na hata U-Miss.Hapo kabla huwa na maisha ya kawaida tena akiwa na juhudi ya mafanikio lakini anapokuja 'Hit'na kujulikana nchini na hata nchi jirani cha kwanza tunachoanza sikia au kitakachofuata ni kutafuta kuingia kwenye mahusiano kwa nguvu kubwa na kutangaza kuwa sasa 'ana mtu'. Zile juhudi zake zooote za mwanzo na weledi pamoja na nyota aliyokuwa nayo huanza fifia hapo na ndio basi dada huyu huenda akitoweka na kupotea kabisa.

Na kibaya nilichojifunza wengi wao wanakuwa warembo kweli lakini huwa nasikitika kuona wanaenda kuangukia kwenye uhusiano na mtu asiyelingana nae ki hadhi,umri au hata tabia.

Wengine huangukia kwenye penzi na mtu wa shoga yake na kuleta 'bifu'.Wengine wanaangukia kwa ma zungu wa unga,wapigaji nk.

Mahusiano yoote hayo humfanya dada huyu kuishia kuzalishwa na ndoa au uhusiano kuvunjika!Na hii ni 95% yao huishia hivi..hili.

Inanisumbua sana kuona safari yao yaisha mapema bila kufikia level ya kimataifa kama walivyo nyota wengine wa mataifa mengine!

Sina haja ya kuwataja majina hapa ila tu nitapenda kuwapa baadhi yao pongezi kubwa kwa kuonyesha kuwa ni wapiganaji na wametulia japokuwa walivuma lakini 'hawaja pasuka na kulewa sifa na wengi wametulia na familia na wanaperfom vizuri ktk nafasi zao. Miongoni mwao ni Happiness Magese,Jaquline Ntiyubaliwe,Fatma Nyangasa,Besta,Luiza Mbutu,Hoyce Temu nk.

Mwisho ningeombea huyu mwimbaji chipukizi Ruby basi asibugudhiwe afike mbali na asiangukie upande mbaya hasa asitangulize suala la mahusiano ya kimapenzi awajibike kwanza bado ana umri mdogo, ni vema tumuone akifika mbali katika game.

Midume yenye tamaa ikae mbali nae nasi tupate wa kujivunia Tanzania kama ilivyo kwa akina Yvonne Chakachaka,Anjeric Kidjo,Sade nk.
 
"... nasikitika kuona wanaenda kuangukia kwenye uhusiano na mtu asiyelingana nae ki hadhi,umri au hata tabia..."

Kwa point hizi nashangaa kwanini umemuweka Jaqline Ntuyabaliwe kundi unalolisifia
 
Hujajua kwa jini kamuweka????



"... nasikitika kuona
wanaenda kuangukia
kwenye uhusiano na mtu
asiyelingana nae ki
hadhi,umri au hata tabia..."

Kwa point hizi nashangaa kwanini umemuweka Jaqline Ntuyabaliwe kundi unalolisifia
 
Sawa mkuu natumaini wamekusikia na kukuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…