Wanaijeria ni wajanja sana. Nyimbo zao nyingi ni za furaha furaha. Ndicho watu wanapenda. Kingine kikubwa ni wajanja sana katika vionjo hasa melody kwenye chorus na bridge. Hapo ataweka %90 kuhakikisha anabamba. Wasikilize wote wanaovuma. Hatujui hata wanaimba nini pamoja na pidgin yao ila tunajikuta tunarukaruka tu. Wasanii wetu wawekeze huko pia. Ila nawakumbusha, soko la muziki limeshikwa sana na vijana. Wakumbuke kuna watu wazima pia ambao hawana burudani. Wanabakia kusikiza kwaya na zilipendwa. Vijana hao wajitahidi kwenye natumizi sahihi ya lugha na ujumbe