Mastaa wa ugahibuni waliopata watoto kabla ya kufunga ndoa....!

Mastaa wa ugahibuni waliopata watoto kabla ya kufunga ndoa....!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
celeb-mums-salma-hayek-600x400.jpg


Salma Hayek:

Alijifungua mtoto wa kike Septemba 21, 2007 akampa jina la
Valentina Paloma Pinault akaja kufunga ndoa na mchomba ake Bilionea aitwae Francois Henri Pinault mwaka 2007, lakini muda mfupi baadaye walitengana.
Hata hivyo miaka miwili baadaye tangu watengane, wakatangaza kurudiana tena.

300.ab.portman.102011.jpg


Natalie Portiman:

Mwigizaji wa Holliwood, Likutana na mume wake mwenye asili ya Ufaransa aitwae Benjamin Millipied mwaka 2010 wakati wakitengeneza sinema ya Black Swan, walijaaliwa kumpata mtoto wao wakiume aitwae Aleph mnamo June 2011 na mwaka uliofuata ndio wakafunga ndoa

tamekatinycottle.jpg



ti-family.jpg


TI na Tameka:

Rappa TI amekuwa na mpenzi wake Tameka kwa takriban muongo mmoja kabla hawajafunga ndoa. Ingawa ana watoto watatu kutoka katika mahusiano yake ya nyuma, lakini pia alikuja kuzaa na Tameka mtoto wa kike baada ya kuwa katika uhisiano kwa miaka mitatu, baadaye walikuja kuongeza mtoto mwingine wa kiume ndipo wakafunga ndoa mwaka 2010.

Katie+Holmes+Tom+Cruise+Welcome+Baby+Girl+7ADHS9HWieTl.jpg

Katie Holmes:

Miezi michache baada ya kuachana na mpenzi wake Chris Klein, Katie alikuwa akionekana akiwa na Tom Cruise. Tom alimvika pete ya uchumba Katie mwaka 2005, lakini miezi michahe kabla ya kufunga ndoa walipata mtoto wao wa kwanza ndipo wakafunga ndoa ya kifahari mwishoni mwa mwaka 2006
Hata hivyo mwaka jana Katie alijaza hati ya kumtaliki mumewe huyo

heidi-klum-park-day-with-kids.jpg


Heidi Klum:

Wakati Heidi Klum alipoanza uhusiano na mwanamuziki Seal, alikuwa tayari ana ujauzito aliopewa na mpenzi wake waliyeachana aitwae Flavio Briatore. Mtoto huyo alizaliwa huku Mwanamuziki Seal akishuhudia katika chumba cha kujifungulia (Labour) mnamo mwaka 2004. Baadaye alimuasili mtoto huyo waliyempa jina la Helene. Hawakuchukua muda walioana na kuongeza uzao wa watoto. Walifunga ndoa rasmi mnamo Mei 2005 na mtoto wao aitwae Henry alizaliwa mnamo September 2005. Heidi na Seal waliongeza watoto wengine wawili hadi walipotengana mwaka jana.

Nicole Richie:
Katika maisha ya ujana Nicole Ritchie alianza vibaya kwa kujiunga na kampani ya warembo watukutu kian Paris Hilton na Lindsay Lohan. Baada ya kukua na kujitambua alianza mahusiano na Joel Madden. Walipata mtoto wao wa kwanza mwaka 208, kabla hata ya kuvikwa pete ya uchumba. Hata hivyo walikuja kuoana rasmi mwaka 2010

nicole.jpg


Nicole Richie:
Katika maisha ya ujana Nicole Ritchie alianza vibaya kwa kujiunga na kampani ya warembo watukutu kina Paris Hilton na Lindsay Lohan. Baada ya kukua na kujitambua alianza mahusiano na Joel Madden. Walipata mtoto wao wa kwanza mwaka 208, kabla hata ya kuvikwa pete ya uchumba. Hata hivyo walikuja kuoana rasmi mwaka 2010

angelina-jolie-and-brad-pitt-family-in-new-orleans.jpg


Brad Pitt na Angelina Jolie

Wakati alipomuoa Jennifer Aniston, mcheza filamu wa Hollywood Brad Pit alisema wazi ni kiasi gani alikuwa na hamu ya kuitwa baba. Maombi yake yalijibu baada ya kuachana na Jennifer na kumuoa mwanamke mrembo na mcheza filamu wa Hollywood Angelina Jolie. Akiwa ni mama mwenye mtoto wa kiume aliyemuasili, alianza mahusiano na Brad Pitt, na mpaka sasa wanajivunia kuwa na watoto sita wakiwemo wa kuwazaa wenyewe na wengine wa kuasili (Adopt). Hata hivyo walikula kiapo kwamba hawatafunga ndoa mpaka sheria ndoa ya jinsi moja itajkapopitishwa, lakini walivikana pete za uchumba mwaka 2012. Mpaka sasa sherehe yao ya kufunga ndoa bado haijatangazwa

Michael_Douglas_Catherine_Zeta_Jones_768x0_rozmiar-niestandardowy.jpg


Catherine Zeta-Jones na Michael Douglas:

Mcheza filamu Danny Devito ndiye aliyemtambulisha Michael Douglas kwa Catherine Zeta-Jones mwaka 1998. Lakini wakati huo Michael Douglas alikuwa bado hajaachana na mkewe. Baada ya kuchana na mkewe alimchumbia Catherine Zeta-Jones. Wakiwa bado wako kwenye mipango ya kufunga ndoa, wapenzi hao walipata mtoto wa kiume waliyemuita Dylan Michael Douglas. Walikuja kufunga ndoa miezi kadhaa baadaye ikiwa ni wiki chache baada Michael kukamilisha taratibu za kuachana na mkewe .


Kwa leo naishia hapa.....................
 
ukuje bana kuendelea babu.........huyo anayekushika sharubu akuwache kwanza.....
 
mbona mimi ni msanii huko majuu na idadi ya watoto watatu nje hujaniweka ktk list yako......bila kumsahau Khloe Kadarshian
 
TI mwafrika asilia...amepiga watano....@ Kongosho. Halafu kamweka bidada miaka 13 ndio akatangaza ndoa. Aisee huyu anafanana na hawa ndugu zetu wa humu.

Sasa unatushauri nini na sisi tuendelee kuzaa kabla ya ndoa au ndo kawaida au ndo nini @ Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom