Mastaa waliopiga mabao yanayozidi 700 kama Ronaldo

Johnny Sins

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
2,537
Reaction score
3,873
JUMATATU iliyopita, Cristiano Ronaldo alifikisha bao lake la 700 katika maisha yake ya soka, wakati alipofunga mara moja akiwa na Ureno kwenye mechi ya kipigo kutoka kwa Ukraine kwenye mikikimikiki ya kuwania Euro 2020.
Mabao hayo 700 amefunga kwenye mechi 973, akifunga kwenye michuano 12 na kuweka rekodi tamu kabisa ya kufikisha idadi hiyo ya mabao kwa haraka.

Ronaldo alifunga mabao matano katika mechi 31 alizochezea Sporting CP, mabao 118 katika mechi 292 alizoichezea Manchester United, mabao 451 katika mechi 438 alizocheza kwenye kikosi cha Real Madrid na mabao 32 amefunga kwenye mechi 51 alizochezea klabu yake ya sasa ya Juventus. Mabao mengine alifunga akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Ureno na hivyo kuingia kwenye kundi la mastaa wachache sana kwenye dunia ya soka waliofikisha mabao 700 katika maisha yao ya soka.
Hawa hapa mastaa watano waliofunga mabao mengi kuliko Ronaldo nao wakifikisha idadi hiyo kwa haraka zaidi.

5. GERD MULLER (mabao 735)
Alifahamika kwa ufundi wake wa kupasia nyavu, Gerd Muller anabaki kuwa mshambuliaji bora kabisa kwenye suala la kusukumia mipira nyavunni. Muller aliichezea Bayern Munich kwa miaka 15 na hadi sasa mabao yake aliyofunga kwenye timu hiyo yanamfanya kuwa kinara wa mabao wa muda wote. Gwiji huyo alifunga pia bao la ushindi wakati Ujerumani Magharibu wanabeba Kombe la Dunia 1974, huku akiwa na wastaani balaa wa mabao, ambapo kwenye timu ya taifa, amefunga mabao 68 katika mechi 62.


4. FERENC PUSKAS (mabao 746)
Wakati akiaminika kuwa mmoja wa wanasoka bora wa muda wote, Puskas, aliyekuwa akifahamika kama ‘Galloping Major’ alitamba na kmikosi cha Hungary na Real Madrid, aliyotamba nayo kwenye michuano kibao ikiwamo ya Kombe la Ulaya mwaka 1960. Umahiri wake wa kufunga mabao makali, yanamfanya jina lake litumike kwenye ile tuzo ya Bao Bora la Mwaka inayotolewa na Fifa, ‘The FIFA Puskas Award’, ambapo imekuwa ikitolewa kila mwaka kwa mchezaji anayefunga bao bora zaidi kwa mwaka husika.


3. PELE (mabao 767)
Mbrazili Pele bado anatambulika kama mmoja wa watu waliohamasisha zaidi soka duniani, huku akiingia kwenye kitabu cha rekodi cha Guiness cha kufunga mabao mengi kwa mechi, baada ya kudaiwa amefunga mabao 1281 katika mechi 1363.
Mshindi huyo mara tatu wa Kombe la Dunia akiwa na Brazili, Mfalme Pele alifunga mabao 767 katika mechi 831 na hivyo kuwa na wastani mzuri wa kufikisha idadi ya mabao 700 na kuendelea ndani ya mechi chache. Bao lake la kichwa alilofunga kwenye Kombe la Dunia 1970 lilikuwa la 100 kwa Brazil.


2. ROMARIO (mabao 772)
Akiwa na mabao 772 katika mechi 994, Romario anatajwa kama mchezaji hodari zaidi kwa kufunga kuwahi kutokea duniani. Kwa sasa akifanya kazi ya siasa huko kwao Brazil, Romario alitajwa kuwa Mchezaji Bora wa Dunia mwaka 1994 na alikuwa sambamba na Pele, alipochaguliwa na raia kwenye timu ya Fifa ya mwaka 2002.
Mbrazili, Ronaldo de Lima, alisema Romario ndiye mwanasoka aliyekuwa akimtazama wakati anakua na kocha wa zamani wa Barcelona, Johann Cruyff aliwahi kumwelezea Romario kuwa ni jiniazi anapoingia kwenye eneo la penalti.


1. JOSEF BICAN (mabao 805)
Gwiji wa Austria, Josef Biscan anaongoza kwenye orodha hiyo akiwa amefunga mabao 805 katika mechi 530 tu. Akijitengenezea umaarufu wa kuwa mchezaji aliyetumia vizuri zaidi miguu yote miwili, Bican alicheza klabu kadhaa huko kwao Austria kabla ya kwenda kukipiga kwenye timu nyingine kadhaa Jamhuri ya Czech, ikiwamo Dynamo Prague. Alicheza pia Bohemia na Moravia.
Wakati ikiaminika kwamba amefunga mabao yapatayo 1470 katika maisha yake ya soka, lakini idadi hiyo ya mabao imedaiwa ikihusisha hata zile mechi zisizotambulika.
 
Magoli anawafunga Lithunia,Kazakstan Cyprus
 
Na wale tuliopiga magoli mengi zaidi ya hayo Ila kwenye miili ya mabinti takwimu zetu mtazitoa lini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…