Wadau nauliza hii kutokana na kuendelea kufa au kuzorota kwa miradi ya kibiashara ya wasanii wetu mastaa nje ya fani zao zilizowapa majina.
Biashara ya Lady Jaydee mgawaha wa Nyumbani Lounge , bar ya marehemu Ngwea ilikufa kabla ya yeye mwenyewe kufariki, duka la pamba la AY, Diamond na Ray C yote yalikufa kifo cha kawaida . Mo Faya ya King Kiba hii ilikufa kabla ya kuanza na mhanga mwingine ni Chibu Pefrume na Diamond Karanga nayo chali pia. Huku lotion ya Mwana Fa ikiwa inahemea pua moja.
Je, hawa jamaa wanakosea wapi?