Master over us

Master over us

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Binadamu, Ndege , wadudu na wanyama wa porini wote hufa.

Ni nani mwenye mamlaka dhidi yetu?

Mwenye mamlaka dhidi yetu ni yeye afanyaye viumbe vyote kufa.

Kipindi chetu cha maisha hapa duniani ni kifupi mno. Tunakuja na kuondoka. Kila mtu amepangiwa miaka ya kuishi.

Je ni nguvu gani hiyo ambayo huonyesha mamlaka yake kwa kufanya viumbe vyote kufa?

Kitu ninachojua kwamba tungeishi miaka mingi hata milele tungekuwa viburi. Mungu ameleta kifo ili tujue kwamba yeye ni mkuu na sisi ni wadogo.

Maskini kwa tajiri, wajinga kwa wenye busara, waovu na wema wote hufa. Wote hupotea na miili yao huyayuka na kuwa mavumbi na mifupa.

Nausubiri kwa huu mwili ninaotumia kwa maisha yangu hapa duniani ufe na roho yangu irudi kwa Mungu ambako ilitoka. Kwasababu najua yupo .

Angalia dunia na anagaza. Ukweli upo bayana. Anawapa bure wanyama wa mwituni na hata wanyama wa kufugwa chakula chao.

Mvua inaponyesha majani hukua na mbuzi na ng'ombe na swala wa mwituni husherekea.

Ni yeye atupaye afya na nguvu ya kufanya mambo yetu ya kila siku. Bila ya yeye sisi hatuna kitu.

Kwasababu tunategemea mazao ya ardhi hii kwa maisha yetu. Tumezaliwa tumeikuta ardhi hii ambayo inatulea kwa kutupa chakula.

Kitu kimoja ninachojua Mungu anapenda viumbe vyake vyote. Na hapendi kiumbe chake hata kimoja kiumie. Yanayotokea kwetu ni kwasababu tumemuacha Mungu na kufuata njia zetu wenyewe.

He is the master over us. He rule us and by our death, he show his mastership. No one will ever escape death.
 
Mungu gani huyo? Sijaelewa wala kuamini kuwepo kwa mungu.

Kwanza nieleweshe Mungu unayemuongelea ni mungu gani?

Na kwa nini unahitaji Mungu kuelezea kifo wakati the second law of thermodynamics inaelezea kifo vizuri tu bila kumhitaji Mungu?
 
Back
Top Bottom