Kijana huyu ni hazina kubwa sana kwa taifa hili, tena in a non-partisan way. Kama anazidi kujiongezea elimu, hiyo ni habari njema sana kwa vijana wanaounga mkono jitihada zake za ujenzi wa taifa. Sidhani kama mjadala wa wapi kapata pesa kusoma una tija kwani kuna kusoma online, na degree za namna hiyo kama ni toka chuo reputable, hazina utofauti na degree za kwenda darasani, ili mradi uwe na kichwa kizuri. Kwa mtazamo wangu ambao pengine ni finyu, kwa nafasi yake ya ubunge, Mnyika, muda wa ku attend masomo darasani sidhani kama anao, lakini uezo wa kujilipia masomo online anao kwani sio gharama hivyo. Tusimvunje moyo kijana huyu, ni mmoja wa viongozi ambao masuala mengi wanayosimamia ni ya kizalendo zaidi kuliko kisiasa/kichama.