Masters of Health System vs Masters of Public Administration

Masters of Health System vs Masters of Public Administration

Zote ni nzuri inatokana na malengo yako,kwa uzoefu wangu katika mambo ya kazi(kama malengo yako ni kuajiri)Masters in Health Systms Management ni nzuri katika NGO's zinazohusika na mambo ya afya,hatari yake ni kuwa unakuwa umejifunga katika eneo moja la Afya.
Kwa upande mwingine MPA ina nafasi kubwa unaweza kufanya kazi kama afisa rasilimali watu/Tawala hususani katika taasisi za serikali.
Sasa ile iwe rahisi kukushauri sema wapi umeajiriwa kwa sasa na malengo yako yakoje!
 
Kozı zote za sosholojia kazi yake mpaka michongo.Public health inaweza kuwa dili kuliko hyo MPA.
 
Malengo yangu ni kwamba baada ya miaka 3,nijiajiri mimi mwenyewe!Kwa sasa mimi ni mwalimu&nimeajiriwa wilayani.
 
sasa mwalimu ukasome MPA kweli ndugu yangu? hapo unaua career bora ukasome Master of Education pale UDSM
 
Asante kwa ushauri.Malengo yangu ni kubadili fani kwanza.SITAKI TENA KUWA MWALIMU.
 
Asante kwa ushauri.Malengo yangu ni kubadili fani kwanza.SITAKI TENA KUWA MWALIMU.

Dada yangu sikiliza,ukienda kusomea Masters ya Education wakati ulishafundisha sio lazima ukashike tena chaki...kuna kuwa mkaguzi,Afisa elimu msingi,A E Sekondary,unaweza kwenda kwny idara ya utungaji na uhakiki wa mitihani(kuna course mpya imeanzishwa na inahitaji skilled personnel kwny mambo hayo,nakushauri ukaisome hiyo) na bado pia kwenye halmashauri kuna kazi nyingi tu away from teaching.

Kwasasahv iwe Bachelor au Masters ya Education kwa nchi hii ni muhimu sana kuliko wanavyodhani watu wengi.
 
sasa mwalimu ukasome MPA kweli ndugu yangu? hapo unaua career bora ukasome Master of Education pale UDSM

We jamaa sijui umekula maharage ya wap wewe! Inamaana mwalimu.hawezi kifanya kaz za management? Mbona kina wakaguz, watu wa tsd, maafisa elimu, wakuu wa shule nk wote hawa wanahusika na sera na management ya watu na raslimali zilizopo kwenye maeneo yao ya kaz, so kwa mwalimu kusoma MPA sioni kama ni dhambi, na haimtoi kwenye field yake.
 
Mbarikiwe kwa ushauri wenu mzuri.Mimi nilitaka kubadili fani moja kwa moja,hata uafisa elimu siutaki.
 
Asante kwa ushauri.Malengo yangu ni kubadili fani kwanza.SITAKI TENA KUWA MWALIMU.

Kuna kitu watu hawakijui,, masters siyo sifa ya kuingilia kazini,, hiyo masters inahitaji kuwa na uzoefu wa hiyo kada,, kwa mfano walimu wengi wamepoteza muda na fedha kwa kusoma masters tofauti,, labda upate mbeleko ya private institutions,, mfano kwa serikali hauwezi kubadili kada kwa masters tu
 
Nenda kapige bachelor degree nyingine tu,
 
Fanya masters ya public administration itakusaidia kuwa na uwanja mpana sana cz tayar una degree ya education kuna jamaa yangu alisoma education udsm bdaye akaenda kusoma masters ya hr mzumbe kwa sasa ni.meneja mzuri wa hr kwenye kampuni kubwa. ..health unakua umejbana sana na serkalin haina ishu sana
 
Hakuna afisa elimu aliyepata hicho cheo kwa kusoma MPA, infact, MPA ni vague balaa utapoteza hela na muda, bora hata uende Zoom polytechnic au VETA
 
Back
Top Bottom