Masundosundo (genital warts )

Masundosundo (genital warts )

Amoury94

Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
89
Reaction score
37
TIBA YA UGONJWA WA KUOTA KINYAMA SEHEMU ZA SIRI NA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI (GENITAL WARTS & SKIN)

Habari rafiki, natumaini mnaendelea vizuri leo napenda kuzungumzia tatizo la kutokewa vinyama katika sehemu za siri na mwili au Masundosundo au vigwaru kwa kitaalamu tunauita GENITAL WARTS

~GENITAL WARTS ni nini?!!

~ni ugonjwa wa kuota vinyama Laini vidogovidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando Laini unaozunguka maeneo ya sehemu za siri.

~vinyama hivyo vinaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo (urethra), vulva, na shingo ya kizazi au maeneo yanayozunguka haja kubwa, ugonjwa huu huenezwa kwa njia ya kujamiiana (SEXUAL TRANSMITTED INFECTION (STI)

CHANZO CHA TATIZO HILI

Ugonjwa wa Masundosundo husababishwa na virus waitwao HUMAN PAPILLOMA VIRUS (HPV) hata hivyo Kuna Aina 70 tofauti za virus wa HPV hivyo sio wote wanaosababisha tatizo hili kwani Kuna ambao wanasababisha Masundosundo katika mwili sehemu tofauti kama vile mikono, miguu, mgongoni, NK pia wapo wanaosababisha saratani ya shingo ya kizazi (CARCINOMA OF THE CERVIX),saratani ya uume na saratani ya njia ya haja kubwa (ANAL CANCER) kwa jinsia zote mbili

°ugonjwa huu wa Masundosundo umejitokeza kwa kiasi kikubwa baada ya kuwepo kwa janga la UKIMWI hivyo watu wenye wapenzi wengi, wanaofanya mapenzi kwa njia ya haja kubwa, wajawazito, watumiaji wakubwa wa sigara na pombe, watu wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo Wana hatari ya kupata tatizo hili.

DALILI ZA MASUNDOSUNDO

mgonjwa wa tatizo hili hutokewa na vinyama Laini vidogovidogo vinavyojitokeza juu ya ngozi katika maeneo tofauti (MFANO HALISI TIZAMA KATIKA PICHA HIZO) ingawa wakati mwingine huwa ni vidogo kiasi cha kutoweza kuonekana kwa njia ya kawaida

mgonjwa kupata ganzi maeneo yaliyozungukwa na Masundosundo

kutokwa na uchafu sehem za siri na kuwashwa kupita maelezo

kutokwa damu ukeni mara baada ya kufanya tendo la ndoa MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA UGONJWA HUU
 
Back
Top Bottom