Maswahibu yanayomkuta Halima Mdee yalinikuta na Mimi, tofauti tu yeye ni Senior Mimi nilikuwa Junior

Akaendelea kutuambia kwamba pamoja na asante hiyo tumevunja itifaki ya kampuni kwa kupeleka deal moja kwa moja kwa CEO badala ya kupitia kwake OM ambaye ndiye line manage wetu.. hii tuliambiwa mapema wakati wa orientation yetu, kwa hiyo ni lazima tuchukuliwe hatua za kinidhamu huku akitoa ka kitabu hako ka Policies & Procedures na kutuambia tusome ukurasa wa kumi ambapo ulieleza endapo mfanyakazi ambaye si wa idara ya mauzo akipata mteja ama biashara je afanyaje?.

Wakati huo Sales Manager alikuwa kimya akituangalia kwa makini, tuliambiwa kama tuna utetezi wowote tuuseme muda huo kabla hatujapewa adhabu yetu ingawa aligusia kwamba adhabu inaweza kufikia hata kufukuzwa kazi..

Sikuamini... sikuamini; Yaani kumbe kujiongeza kwangu kote kule nilidhani naisaidie kampuni yangu kumbe ndiyo nimeharibu kabisa.. sikuamini.. Chumba kilikuwa na AC kali ila tulianza kutoka jasho jembamba... kabla ya utetezi nilianza kulia huku nampigia magoti OP wangu, mwenzangu kichwa kikaangukia meza kimyaaaa.....

...inaendelea....
 
Duuuh kweli hii nchi ngumu!!

Inaezekana huyo jamaa aliona mmebania ulaji maana kama mngepeleka kwake maana yake ingeonekana yeye ndiye kaleta mteja na sio nyie!!
 
Nikasikia kwa mbali OP akisema you need to see the company secretary immediate after this...wakatoka wakatuacha - tulibakia pale conference kwa muda kama nusu saa, nikazinduka nikamshtua mwenzangu nikamwambia kaka jikaze huu ndiyo ukubwa, tayari tushaingia cha kike - wamesema tukamwone secretary pale chini hatuna namna... Kosa letu kubwa tunatuhumiwa nalo kujaribu kujipatia commission bila kufuata utaratibu... tume pindisha deal kwa makusudi ili tujipatie fedha huku tukijua kufanya hivyo ni kosa kubwa.

Tulitoka huko, baadhi ya staff wakitushangaa mno kulikoni?? maana hatuwashirikisha kwa lolote kwa hiyo hawakujua what is going on...
Tulifika pale reception, tukakuta barua tayari zilishachapwa na kusainiwa tayari kwamba kwa kosa tulilofanya hatuwezi kuvumilika hivyo sisi si wafanyakazi tena wa kampuni kuanzia muda huo - tutapewa mshahara wa mwezi mmoja kama sheria inavyotaka na tunatakiwa kukabidhi vitu vya office siku hiyo hiyo na kuondoka.

Aisee nilitamani nife kabisa, niliona maisha yangu hayana maana tena - nilifikiria je ntalipaje pango, nitakula nini? maisha magumu.. kikakabidhi vitu vyao nikachukua barua yangu ya kufukuzwa nikasepa - mshikaji wangu pia hivyo hivyo tukaondoka - kabla ya kuagana kituo cha basi tukapanga tukutane kesho getoni kwangu tupange nini cha kufanya......

....inaendeea usiondoke
 
Kuwa uyaone ya dunia..
Origami za kizamani, hapo wangeweka utaratibu ukileta deal mtu wa nje ya sales unapewa commission ndogo kuliko sales.

Ukiritimba kama huu wa watu wa sales umeathiri sana kampuni flani.
 
Duuuh!

Kwa sababu mna ujuzi hilo ndio la maana.

Ningemrudia yule jamaa aliye toa dili no way!!
 
pole sanaa Mkuu ila kwa mzee halima ni usaliti uliofanywa kwa kushirikiana na mfumo
 
Nendeni mkaajiriwe na huyo CEO mpya maana amejua how potential mlivyo lakini kampuni yenu inataka kuwadhulumu.


Poleni samaki wenzangu
 
Operations Manager alitumia msahafu kuwafukuza kazi vijana waliyeleta mteja kwenye kampuni yake bila kuangalia aina ya kosa na athari zake kwa kampuni; hakujali wala kuangalia uzoefu wa wakosaji wahusika, hakujali historia yao ya kufanya makosa, umuhimu wao kwenye biashara, athari zinazoweza kutokana na kufukuzwa kwao kazi kwa kampuni na kwa wateja na mambo mengine

Wapo managers wengi sana wa aina hii. FUSO endelea na haka kahadithi tujue iliishaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…