MASWALI KADHAA YA KIDUKUZI KUHUSU SIASA

MASWALI KADHAA YA KIDUKUZI KUHUSU SIASA

Alpha13

Senior Member
Joined
Oct 26, 2015
Posts
141
Reaction score
119
Habari wana jamvi, Asubuhi ya leo itakua vyema tukizungumza kwa mitazamo tofauti hususani siasa zetu hapa nchini na Afrika katika nyezo ya kidukuzi (INTELLIGENCE).

Siasa zetu na mahali pengine afrika mara nyingi zinafungana na vyombo vya ulinzi (serikali) ambapo kimantiki ni misingi ya nchi nyingi zenye chama kimoja. Maswali kadhaa yanaibuka kuhusu mifumo na utendaji wa vyama vya siasa, binafsi nawasilisha kadhaa; wadau mnaruhusiwa kuchangia pia kuongeza maswali mengine ili maarifa yaongezeke na kusambaa kati mwetu.

1. Vyama vya siasa vinaruhusiwa kisheria kumiliki, kuhasisi au kukodi taasisi yoyote ya kijesusi kwa minajiri ya kisiasa?

2. Wanao panga mbinu za vyama huwa ni viongozi wa kamati kuu au watu maalumu wenye taaluma hiyo? matokeo hasi au chanya huwa na tofauti kati ya makundi haya mawili?

3. Taarifa za ndani za vyama huwa zinakusanywa na kuratibiwa kwa mfumo upi, wahusika wadogo na wakuu ni wale tunao wajua kama “katibu uenezezi” “katibu wa chama” au “mwenyekiti” ama kuna jeshi kivuli nyuma ya masuala haya?

4. Kuna tofauti gani mathubuti tukilinganisha vyama vya siasa nchi zilizoendelea na zinazoendelea katika masuala ya kuhadaa na kudanganya umma?

5. a)Makundi ndani ya vyama ni jambo la kawaida, mara nyingi vinahusishwa na kuandaa warithi wa vyeo na ugombea wa hapo mbeleni, je makundi haya huwa yana mizizi katika tabia halisia ya kibinadamu kutamani vyeo vya kiutawala/uongozi au ni kiburi cha pesa?

b) Mara nyingi tumeona yakishindwa kufikia malengo yao mfano; anguko la Zitto Kabwe CDM na Lowassa kuenguliwa CCM, nini mapungufu yao na mbadala wa “intelligence” katika kufanikiwa katika mipango hii au kutokomeza makundi ndani ya vyama?

Naomba niwasilishe, karibuni tujadili.
 
Back
Top Bottom