Mbaya zaidi wanaopiga kura ya mapema wataenda tena siku ya pili kupiga kura ya wabunge na Rais wa muungano. Kwanini wasingepiga kura zote tarehe 28 badala ya kupoteza muda wao kwa siku mbili kupiga kura. Dhamira ni nini?Huu ni upuuzi mtupu na mbinu za kuiba kura,Zanzibar ni ndogo na inawatu wachache kuriko Dar,sasa kama Dar haipigi kura kwa siku mbili kwanini Zenj ipige kwa siku mbili,
Hata kama hao wanaopiga ni watu maalum na viongozi,TZ bara inawatu maalum na viongozi wengi kuliko Zenj,na haipigi kura kwa siku mbili.
Wizi mtupu
Je, wakifika wanaonyesha vitambulisho vya kazi zao, je, anonymity (usiri) kwa wapiga kura uko wapi? sio vizuri kujua watumishi wa serikali walipigaje kura zao. La sivyo kura zao zisihesabiwe peke yake zisubiri kuchanganywa na kura za siku ya pili.Je, watu hao ni wangapi
Namba tatu ndio mpango mzima uliobeba dhamira ya kupiga kura siku mbiliZanzibar Wanapiga kura ya mapema kwa watu maalumu na kura ya watu wote siku ya pili.
Maswali kwa ZEC
1. Tume itabandika majina ya watu hao maalumu wanaotakiwa kupiga kura ya mapema kwenye vituo. Je, tume itayajuaje majina ya watu maalumu hadi iyabandike vituoni?
2. Kama tume inayafahamu majina yote ya watu maalumu je usiri katika kupiga kura utahakikishwa vipi? Maana Ni rahisi kufahamu watu maalumu wamepigaje kura zao Kama kura zao zitahesabiwa siku hiyohiyo.
3. Je, waliopiga kura ya mapema watazuiwaje kupiga kura Tena siku ya pili Zanzibar au Bara. Yaani kupiga Mara mbili kwenye uchaguzi.
4. Dhamira kuu ya kupiga kura siku mbili Ni Nini? Mbona Tanganyika ambayo Ina wapiga kura wengi inapiga kura siku moja tu watu wote
?
Hii inanikumbusha uchaguzi wa kura tatu za wakoloni