Maswali kwa Nape Nnauye na Jaji Warioba!!

Maswali kwa Nape Nnauye na Jaji Warioba!!

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
1,832
Reaction score
566
Baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuuamuwa kutumia Helkopta 2 kuzunguka karibu nchi nzima kukusanya maoni ya Wafuasi na wasio wafuasi wake juu ya aina ya MUUNDO GANI wa KATIBA wanayo hitaji, Chama chama Pinduzi na Mwenyekiti wa Tume ya Katiba wamekuwa wakiweweseka sana na utaratibu huu unaotumiwa na Chama cha CHADEMA.

Huku CHADEMA ikijaribu kuwafikia wananchi wa chini kabisa vijijini kupata maoni yao,CCM imebakia DODOMA makao makuu ya Chama hicho kujifungia ndani na kudai kuwa pale ndipo watakapotoa maoni ya wanachama wao huku katibu wa Uenezi wa chama hicho kilicho zeeka,akiendelea KUWASHWA na CHADEMA na kufikia hatua ya kuikosoa kwa kudai kuwa njia wanayoitumia CDM (ya Helkopta) kukusanya maoni hayo haikubaliki kama kwamba yeye (Nape) ndie mwenyekiti wa Tume au Msemaji wa Tume!!

Swali kwa Jaji Warioba mwenyekiti wa tume ya Katiba!

Naomba kujuwa je Maoni ambayo tume inayataka na itakayo yapokea ni ya watu wachache au taasisi iliyoaamua kujifungia "NDANI" (km wanavyofanya CCM)na kutoa maoni yao then wanaiwasilisha kwa tume, au ni Maoni ya Watu au Taasisi iliyoamua kuzunguka nchi nzima mijini na vijijini haijalishi wanatumia Magari,Helkopta,Miguu au hata usafiri wa UNGO kuwafika walengwa km ambavyo CDM imeamua kutumia usafiri wa Helkopta ili kufanikisha lengo la kupata maoni ya watu mchanganyiko.?

Swali kwa Nape Nauye Katibu wa uenezi CCM taifa;
Je unadhani njia wanayoitumia CDM kupata maoni ya wafuasi wake na watanzania kwa ujumla itaiathirije mchakato mzima wa rasimu ya katiba mpya hadi ifikie hatua ya wewe kuwa msemaji wa Tume??

Swali la 2 kwa Nape;
Je unaweza kutueleza au kutushawishije tuamini kuwa njia mnayoitumia nyie CCM (Kukutana Dodoma) ktk kile kinachosemwa kuwa ni kupata maoni ya wana CCM ni bora zaidi kuliko wanayoitumia CDM(Kuzunguka nchi nzima)?

Swali la 3 kwa Nape;
Ikiwa nyie CCM mlisema mtazunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wanachama wenu na hamkufanya hivyo,unataka kutuambia kwamba DODOMA ndio nchi nzima au ni kweli yametimia yale yasemwayo kuwa CCM kwa sasa haiwezi kuitisha mkutano wa watu 600 na wakajitokeza na badala yake mliona ni heri mjifungie Dodoma ili mlipane Posho then ndio mpeleke maoni ya viongozi kwa niaba ya wana CCM nchi nzima!?

Mwisho. Niombe nijulishwe kuwa kati ya wanachofanya CDM na CCM na CUF ni ipi ambayo ni njia ya wazi ktk kupata maoni ya wafuasi na wasio wafuasi wao kwa uwazi na ukweli!

Na je ktk Muongozo wa Katiba kuna kipengele kinachokataza kutumiwa kwa HELKOPTA kukusanya maoni juu ya Katiba tuitakayo,au ni kwa kuwa tu wanaotumia Helkopta ni CDM na sio CCM?
 
Kwahiyo unategemea Nape aje hapa kujibu maswali magumu namna hii ok Good Luck with that.
 
Kwa mtazamo wangu na kwa ninavyomfahamu Nape, hana uwezo wa kujibu swali hata moja. Badala.yake watakuja washabiki wake na kumwaga pumba. Wait and see.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Ndugu yangu Sokoinei usihangaike kupoteza muda wako na wana CCM waliochoka, serikali iliyochoka wamebakiza kupiga tu mtu ye yote hata kama hana kosa apigwe tu, na kufungua kesi za kijinga mahakamani. Nape ni mtu wa Mungu imani yake ni nzuri sana mbele ya Mwenyezi Mungu lakini kwasababu ya kazi yake hana namna hiyo ndiyo ajira yake na anafanya hivyo makusudi ili amfurahishe aliyemteua, moyoni anajisikia vibaya mno lakini atafanyaje! .... hebu tusubiri kama atakuja kukujibu.... na akija utashangaa hizo pumba atakazo kuja kuzitoa.... stay tuned.
 
Ntakuwa sikuzote narudia kuwa tatizo la Nape sikuzote ni Elimu feki aliyonayo ndo maana anakuwa mtu wa wadhifa mkubwa anaye ongea pumba siku zote. ushauli arudi shule.
 
Mimi namshangaa warioba kuonyesha unazi wake kwa magamba wakati magamba ndo yanapingana naye kuhusu serikali tatu. Cdm ndo wanakubaliana na tume na katika hali halisi magamba hayakuwa na lengo la kuanzisha mchakato wa katiba mpya kwa hiyo hayana moral authority ya kuongea chochote kuhusu mchakato wa katiba
 
magamba hayana lolote zaidi ya kuweweseka,wa tz tunataka maoni yetu from grass root yaheshimiwe na si ya mafisadi Dom
 
Back
Top Bottom