Maswali kwa wateule wote

Oscar Wissa

Senior Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
108
Reaction score
170
Maswali yafuatayo mteule anapaswa kujiuliza katika siku hizi za mwisho.

Mteule...
1. Kwanini uhangaike na chumvi ya upako wakati wewe ni chumvi ya dunia? (Math. 5:13).
2. Kwanini uhangaike na maji ya upako wakati ndani yako kuna maji yaliyo hai? (Yoh. 4:10; 7:38).
3. Kwanini uhangaike na mafuta ya upako wakati yale mafuta ya Roho Mtakatifu yanakaa ndani yako? (1 Yoh. 2:27).
4. Kwanini utoe sadaka ya kumkomboa mzaliwa wako wa kwanza wakati Yesu ndiye mzaliwa wa kwanza na ndiye anayekomboa (Ufu. 1:5, Kol. 1:15, 18, Rum. 8:29, Ebr. 1:6)

Kila mteule anapaswa kujiuliza hayo maswali, kama wewe si mteule basi hupaswi kujiuliza hayo, hadi uokoke, uwe kwanza mteule,

Kwako mteule, Biblia inasema;

Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; wapate kuwapoteza, kama yamkini, hata walio wateule. (Uwe macho mteule)

Mathayo 24:24
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…