Maswali magumu sakata la Messi, Simba

Maswali magumu sakata la Messi, Simba

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,025
Reaction score
1,270
NA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), tayari limemaliza mgogoro wa mkataba uliokuwa ukimhusisha winga, Ramadhan Singano ‘Messi’ na uongozi wa klabu yake ya Simba.
Messi alikuwa akidai mkataba wake umechezewa na Simba kwani awali ulitakiwa kumalizika Julai mwaka huu, lakini uliopo kwa uongozi hivi sasa unaonyesha unamalizika Julai mwakani.
Hivyo katika kikao walichokiandaa TFF juzi kuzikutanisha pande hizo mbili, umetoka uamuzi wa kufuta mikataba yote na sasa wametakiwa kuingia makubaliano mapya kwa ajili ya msimu ujao wa 2015/2016.
Kwenye kikao hicho upande wa Simba uliwakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Collin Frisch, Messi yeye alikuwa pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasoka Tanzania (Sputanza), Mussa Kissoky aliyekuwa akimtetea.
Upande wa TFF alikuwepo Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Celestine Mwesigwa, aliyekuwa akizihoji pande zote mbili kwenye kikao hicho kilichochukua takribani saa mbili (kuanzia saa 6 hadi 8 mchana).
Messi hakuupokea vizuri uamuzi huo kwa kudai kuwa: “Wamesema tukae chini tufanye makubaliano mapya, mikataba yote haipo, lakini kisheria mimi niko huru, bado sijajua kama tukishindwa kuelewana na Simba itakuaje, namuachia Mungu.”
Mara baada ya uamuzi huo wa TFF, yapo maswali magumu ya kujiuliza kutokana na utata ulioghubika suala hilo na namna lilivyomalizwa, baadhi ya hayo ni:
Nani aliyefoji mkataba?
TFF imeamua kulimaliza suala hili kwa staili ya kufunika kombe ili mwanaharamu apite, lakini bado haijaweza kutaja ukweli nani alikuwa ana haki kwenye hilo.
Uamuzi wa TFF bado haujawaingia akilini wadau wa soka, kwani hawajaeleza nani amefoji mkataba huo kati ya Messi au Simba.
TFF inaogopa nini kumtaja aliyefoji?
Hata kama ni Messi ndiye amefoji mkataba aliokuwa nao au Simba imefanya hivyo, kwanini TFF inaogopa kumtaja aliyehusika au inamlinda mtu na kukubali kukumbatia uozo kwenye soka letu?
Katibu TFF alikuwa na uhalali kuwahoji?
Tumeona mambo mbalimbali ya usajili na mikataba ya wachezaji ndani ya TFF yanapitiwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho hilo.
Hili suala la Messi linalohusisha mambo ya kisheria, limekuwa tofauti sana kwani hatujaona chombo hicho kikihusishwa badala yake Katibu wa TFF, Mwesigwa ndiye aliyelimaliza, lipo la kujiuliza je, ilikuwa ni halali kwa bosi huyo kushughulikia suala hilo.
Mikataba ya wachezaji iliyoko TFF ni mapambo?
Kwa kawaida mchezaji anapoingia mkataba na timu, taratibu zinazofuata ni yeye kupewa nakala moja nyingine inabakia kwa timu na ‘copy’ moja hupelekwa TFF kama uthibitisho, huku takwimu zikiingizwa kwenye mfumo wa kielektroniki.
Kutokana na uamuzi huo wenye utata uliofanywa kwenye sakata hilo, je, inamaanisha TFF wameshindwa kufananisha mkataba wa Messi waliokuwa nao na hiyo inayolalamikiwa au mikataba waliyonayo ipo kama mapambo tu?
TFF inatunga sheria kuzikalia au kutumia?
Bado kuna maswali mengi watu wanajiuliza kama TFF inatunga sheria zake kuzikalia au kuzitumia wakati wanaamua masuala mbalimbali yanayokiukwa? Hata wale wanaofoji mikataba au nakala yoyote nao wamewekewa sheria za kuwabana.
Kwa mujibu wa Kanuni za Nidhamu za TFF toleo la mwaka 2012, Sura ya Tano inayozungumzia masuala ya kufoji, Ibara ya 61 (1, 2 na 3) inasema: “Mtu yeyote anayejihusisha na masuala ya soka atakayekutwa na hatia ya kughushi au kutengeneza nyaraka za kisheria kwa lengo za kuzitumia atafungiwa pamoja na kupigwa faini.
“Kama ni mchezaji ambaye amehusika, atakumbana na adhabu ya kufungiwa angalau kutocheza mechi sita. Kama ni kiongozi, wakala wa mchezaji au wakala wa mechi atafungiwa kutojihusisha na shughuli za mpira kwa kipindi cha miezi 12.”
Messi yupo huru au mali ya Simba?
Mikataba yote miwili inayodaiwa kuwa na utata imefutwa kwenye kikao hicho na sasa pande hizo mbili zimeambiwa ziingie makubaliano mapya.
Lakini bado haijajulikana Messi yupo kwenye aina ipi ya usajili hivi sasa, hapa namaanisha yeye bado ni mali ya Simba licha ya mikataba hiyo kufutwa au ni mchezaji huru anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na timu nyingine yoyote?
Kama ni mali ya Simba, je, ni kwa mkataba upi? Huu ni utata mwingine iliyouanzisha TFF kama bado hawajaujua.
Kwanini Simba tu masuala haya?
Sakata hili la Messi si la kwanza kutokea kwenye klabu hiyo, msimu wa 2007/2008, kiungo Athuman Idd ‘Chuji’ naye aliingia kwenye mzozo kama huu na Simba baada ya kumaliza mkataba na kujiunga kwa mahasimu wao Yanga.
Simba ilimng’ang’ania Chuji ikidai bado ina mkataba naye, lakini mkataba aliokuwa nao Chuji ulionyesha umemalizika, jambo hilo lilimuathiri kiungo huyo kwa kukaa nje ya dimba nusu msimu na suala hilo lilipelekwa kwenye vyombo vya dola na kumalizwa kimya kimya. Je, kwanini mambo haya yanajirudia Simba?
Mchezaji gani anafuata baada ya Messi?
Udhaifu wa TFF kushindwa kuyaamua masuala haya ya utata kwenye usajili ambayo yanajirudia kila kukicha, imepelekea wahusika wa mambo hayo kuendelea kuyafanya kila siku unapofika wakati wa usajili.
Kutokana na historia ya masuala hayo kujirudia, lipo la kujiuliza kwenye hilo, je, ni mchezaji gani anayefuata kufanyiwa hilo tena baada ya hili la Messi kumalizwa kienyeji?
Source: Mtanzania-Gazeti la Kiswahili la kila siku
 
Mimi namwona mwandishi kama yupo Judgmental hivi. Naona uandishi wake una mapungufu mengi hasa katika analysis ya issue yote.Ni kweli yamesemwa mengi kuhusu mkataba husika ILA je nani kathibitisha utata uliopo? je aliyesema kwamba mikataba ya pande zote mbili ni batili ametoa maamuzi kama nani (Ni TFF authority inayohusu mikataba ya wachezaji)? Je kweli mwandishi ana copy (statement) ya hayo maamuzi? Kwanini au kwa vigezo vipi ameconclude kwamba Simba ni wakosaji? Je tukio moja la miaka nane iliyopita chini ya viongozi tofauti laweza kuthibitisha kwamba SIMBA ni mabingwa wa kuforge? Je ni kwanini mwandishi kaamua kuchafua Image ya SIMBA ambao bado ni watuhumiwa kwa kuwaambia WATU kwamba tutarajie mchezaji mwingine wa SIMBA kukumbwa na matatizo kama yaliyomkuta MESSI? Mimi si mwandishi wa habari hivyo basi nakaribisha ukosoaji toka kwa wale wenye mtizamo tofauti
 
Acha kuongozwa na hisia mkuu. Fact: Simba wamegushi mkataba. Why? Imeamriwa mazungumzo ya mkataba mpya!
Fact: Simba mabingwa wa kugushi. Why? Samatta, Chuji, Kisiga, Kessy, Maftah , Ngassa, Yondani, etc.
 
Naomba usome upya nilichoandika halafu uangalie hoja zangu.Unajua hapa JF ni sehemu ya kujifunzia kwa watu wa kada mbalimbali sasa mimi nilichoandika si kile kilichopo chini ya carpet bali ni jinsi mwandishi alivyoandika. Hiivi mwandishi huyu akipelekwa mahakamani anaweza kushinda kesi? Sasa kwavile hili jambo linaweza kwenda kwenye vyombo vya sheria kujua mbivu na mbich, je ni sahihi kwa mwandishi kutoa conclusion ya yale ambayo hawezi kuyathibitisha mahakamani. Kinachonisumbua hapa si context ya uandishi husika bali ile art ya uandishi. Ahsante.

Mzalendo Mkweli uko sahihi. Waandishi wetu ni mashabiki lakini hawajui kuwa kazi zao zinawataka kusimama katikati na kuripoti kile kilicho sahihi au kilichofanyiwa utafiti. Maswali mengi anayouliza mwandishi ni elekezi lakini pia yanaonyesha mapungufu katika uelewa wa jumla wa jambo hili.

TFF walichofanya (namaanisha sekretarieti) ni kuzikutanisha pande mbili kuona kama KWANZA zinaweza kuzungumza kuondoa tatizo lililopo la kutokuelewana. Pande zote zimesema inawezekana basi imeamriwa wafanye hivyo na ktkt kipindi wazungumzaji wakuu wawe ni wapatanishi kwa maana ya TFF. Sasa hapa tatizo ni nini? Au watu hawataki wapatane? Na ni kwa faida ya nani?

Pili, Katibu Mkuu hana mamlaka ya kisheria kuamua mkataba uko sahihi au umechakachuliwa, mwenye nafasi hiyo ni Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji. Ila katibu mkuu alichofanya ni kusuluhisha ili pawe na win -win situation. Hata makamani au kwenye vyombo vya kutoa uamuzi wahusika wanaweza kupewa fursa ya kupatana kabla ya kesi yao ya msingi kusikilizwa. Sasa sijui kwa nini watu wanabeza hatua hii.

Mimi ninavyofahamu kama Singano na Simba hawatapatana, na kama kila upande utashikilia msimamo lazima suala hili litarudi moja kwa moja kwenye kamati husika na hicho ambacho wengi wanataka kukisikia kwamba kuna mtu kafoji kitajulikana tu. Kwa hiyo watu wasianze kucheza ngoma ambayo bado haijapigwa. Mkondo wa sheria ni mrefu
 
Nashukuru kwa ufafanuzi, nadhani kama kuna mwandishi wa habari yupo ktk jukwaa hili anachakujifunza kupitia hoja zikazotolewa hapa.

Mwandishi hana makosa ameripoti kutokana na anavyoliona swala kwa mtazamo wake, kwanini TFF wataka simba na Singano wazungumze wakati tayari wameshashindwa kuelewana toka mwanzo, sasa wazungumze kitu gani tena? Kama Singano bado yuko na mkataba simba kwanini Hans wakati anahojiwa E fm alisema kuwa wamempa mkataba mwingine ulioboreshwa ila mwnyw ndo anazunguka nao hajawapa feedback,TFF ndo walitakiwa wakate mzizi wa fitina waseme nani mkataba wake sio halali na kwa misingi ipi, pande isiyoridhika ikate rufaa sio danadana sijui mkae mkubaliane mkataba mpya
 
Mimi namwona mwandishi kama yupo Judgmental hivi. Naona uandishi wake una mapungufu mengi hasa katika analysis ya issue yote.Ni kweli yamesemwa mengi kuhusu mkataba husika ILA je nani kathibitisha utata uliopo? je aliyesema kwamba mikataba ya pande zote mbili ni batili ametoa maamuzi kama nani (Ni TFF authority inayohusu mikataba ya wachezaji)? Je kweli mwandishi ana copy (statement) ya hayo maamuzi? Kwanini au kwa vigezo vipi ameconclude kwamba Simba ni wakosaji? Je tukio moja la miaka nane iliyopita chini ya viongozi tofauti laweza kuthibitisha kwamba SIMBA ni mabingwa wa kuforge? Je ni kwanini mwandishi kaamua kuchafua Image ya SIMBA ambao bado ni watuhumiwa kwa kuwaambia WATU kwamba tutarajie mchezaji mwingine wa SIMBA kukumbwa na matatizo kama yaliyomkuta MESSI? Mimi si mwandishi wa habari hivyo basi nakaribisha ukosoaji toka kwa wale wenye mtizamo tofauti

Hebu rudia kusoma tena ladba utamuelewa mwandishi alicho kiandika.
 
Tanzania bana, kamati ya usuluhishi, kamati ya wachezaji, kamati ya maharage, kamati ya maandazi, yaani ni longolongo tupu. Na mpira hautaendelea popote kwasababu ya majungu ya hizi timu mbili hapakila kitu kinaendeshwa kwa mapenzi hakuna haki.

Acheni ushabiki wenu hapa tuongee ukweli. Kwa ufahamu wangu iliyofanyinka hapa ni forgery. Hii ni fraud kwasababu kuna upande, SSC au huyu Singano umewakilisha mkataba feki na hii kisheria ni kosa la jinai. Moja kwa moja hapa hakuna kama kamati itayohusika na hii issue bali ni jeshi la polisi tu. Hakuna cha kuangalia mkataba mpya, polisi wafanye uchunguzi atakayebainika amefoji huu mkataba akamatwe na sheria ichukue mkondo wake, period.
 
Mzalendo Mkweli uko sahihi. Waandishi wetu ni mashabiki lakini hawajui kuwa kazi zao zinawataka kusimama katikati na kuripoti kile kilicho sahihi au kilichofanyiwa utafiti. Maswali mengi anayouliza mwandishi ni elekezi lakini pia yanaonyesha mapungufu katika uelewa wa jumla wa jambo hili.

TFF walichofanya (namaanisha sekretarieti) ni kuzikutanisha pande mbili kuona kama KWANZA zinaweza kuzungumza kuondoa tatizo lililopo la kutokuelewana. Pande zote zimesema inawezekana basi imeamriwa wafanye hivyo na ktkt kipindi wazungumzaji wakuu wawe ni wapatanishi kwa maana ya TFF. Sasa hapa tatizo ni nini? Au watu hawataki wapatane? Na ni kwa faida ya nani?

Pili, Katibu Mkuu hana mamlaka ya kisheria kuamua mkataba uko sahihi au umechakachuliwa, mwenye nafasi hiyo ni Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji. Ila katibu mkuu alichofanya ni kusuluhisha ili pawe na win -win situation. Hata makamani au kwenye vyombo vya kutoa uamuzi wahusika wanaweza kupewa fursa ya kupatana kabla ya kesi yao ya msingi kusikilizwa. Sasa sijui kwa nini watu wanabeza hatua hii.

Mimi ninavyofahamu kama Singano na Simba hawatapatana, na kama kila upande utashikilia msimamo lazima suala hili litarudi moja kwa moja kwenye kamati husika na hicho ambacho wengi wanataka kukisikia kwamba kuna mtu kafoji kitajulikana tu. Kwa hiyo watu wasianze kucheza ngoma ambayo bado haijapigwa. Mkondo wa sheria ni mrefu

Tanzania imefika hapa ilipo kwa mitazamo potofu ya namna hii. Mambo mengine yako wazi mno, hakuna haja ya kubishana. Singano ana nakala ya mkataba wa miaka miwili WENYE SAHIHI YAKE. Simba wana nakala ya mkataba wa MIAKA MITATU ukiwa na sahihi ya Singano.

Swali kwako: Siingano alisaini mikataba miwili kwa ajira ile ile? Je, TFF wanathibitisha mkataba upi wanautambua?

Hii hoja haikwenda TFF kutafuta suluhu, bali lengo kuu ilikuwa ni kutaka kufahamu kjataba upi ni halali kisheria. Jibu lilikuwa ni ama Singano, ama Simba. Hakuna neutrality hapa. Laiti kama issue ingalikuwa ni kukiuka vipengere vya mmkataba msuluhishi angekuwa na nafasi. Lakini hapa tangu kkuibuka kwa sakata hili hadharani hoja ya pande zote mbili ilikuwa ni kugushiwa kwa mkataba.

Inachukiza sana pale hata mambo yaliyowazi kisheria yanapelekwa kibongo bongo tu. Tumegeuka taifa la ajabu sana. Kila kitu kutafuta mapatano ya kihuni huni tu. Hivi tuna jenga misingi ya soka letu ama tunabomoa????? Kifupi hii ni serious offense, hakuna siasa itakayobadili ukweli huo. Pole sana
 
Naomba usome upya nilichoandika halafu uangalie hoja zangu.Unajua hapa JF ni sehemu ya kujifunzia kwa watu wa kada mbalimbali sasa mimi nilichoandika si kile kilichopo chini ya carpet bali ni jinsi mwandishi alivyoandika. Hiivi mwandishi huyu akipelekwa mahakamani anaweza kushinda kesi? Sasa kwavile hili jambo linaweza kwenda kwenye vyombo vya sheria kujua mbivu na mbich, je ni sahihi kwa mwandishi kutoa conclusion ya yale ambayo hawezi kuyathibitisha mahakamani. Kinachonisumbua hapa si context ya uandishi husika bali ile art ya uandishi. Ahsante.

Hebu onesha mwandishi atapelekwa mahakamani kwa kosa lipi.
Hoja ipi ambayo atashindwa kuithibitisha
 
Tanzania imefika hapa ilipo kwa mitazamo potofu ya namna hii. Mambo mengine yako wazi mno, hakuna haja ya kubishana. Singano ana nakala ya mkataba wa miaka miwili WENYE SAHIHI YAKE. Simba wana nakala ya mkataba wa MIAKA MITATU ukiwa na sahihi ya Singano.

Swali kwako: Siingano alisaini mikataba miwili kwa ajira ile ile? Je, TFF wanathibitisha mkataba upi wanautambua?

Hii hoja haikwenda TFF kutafuta suluhu, bali lengo kuu ilikuwa ni kutaka kufahamu kjataba upi ni halali kisheria. Jibu lilikuwa ni ama Singano, ama Simba. Hakuna neutrality hapa. Laiti kama issue ingalikuwa ni kukiuka vipengere vya mmkataba msuluhishi angekuwa na nafasi. Lakini hapa tangu kkuibuka kwa sakata hili hadharani hoja ya pande zote mbili ilikuwa ni kugushiwa kwa mkataba.

Inachukiza sana pale hata mambo yaliyowazi kisheria yanapelekwa kibongo bongo tu. Tumegeuka taifa la ajabu sana. Kila kitu kutafuta mapatano ya kihuni huni tu. Hivi tuna jenga misingi ya soka letu ama tunabomoa????? Kifupi hii ni serious offense, hakuna siasa itakayobadili ukweli huo. Pole sana

Huu ni muono wako wewe na unaweza kuwa potofu vilevile.

Kisheria ambayo wewe unaipgia kelele narudia kusema tena katibu mkuu wa TFF hawezi kuamua upi ni mkataba halali na upi umechakachukuliwa. Yenye kufanya hivyo ni Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji.

Sasa nikuulize swali: Pande husika ziliitishwa na Kamati inayoshughulikia mambo ya sheria au na sekretariati? Najua jibu unalo, sasa ulitegemea chombo ambacho hakiwezi kutoa uamuzi kama katibu mkuu atoe uamuzi ambao ni binding? Kwa mamlaka ipi? Sheria haimuliwi kwa hisia za kishabiki bali facts na sio kirahisi kama mnavyorahisisha.

Na madai yanabaki kuwa madai hadi yanapothibitika kuwa ukweli. Na mamlaka hiyo sio katibu mkuu.

Halafu kuna kitu katibu mkuu alisema kuwa pande husika zote ZIMEBAINI uwepo wa kasoro zilizopo ktk mikataba yote miwili, na huu ndio msingi wa kuona kama zinaweza kukaa pamoja na kuelwana. Sasa ungekuwa na hoja za msingi kama pande husika hasa Singano na Sputanza wangepinga hilo la kasoro kwenye mikataba yao halafu TFF ing'ang'anize kwamba lazima wapatane. Hapo tungesema TFF imekwenda kuhuni kihuni lakini kabla ya hapo ni hisia na unazi tu ndio unaosumbua na sio issue ya sheria.
 
Kuna swali moja ambalo wachangiaji wenye ushabiki hawataki kabisa kulisikia na kulijibu. Nalo ni hili;
Ukiondoa mapungufu ya kiuandishi yaliyo ktk mikataba iliyo kwa Simba na Messi, mkataba upi kati ya hiyo ndio upo TFF na katika TMS? Naombeni majibu tuanzie hapo.
 
Mzalendo Mkweli uko sahihi. Waandishi wetu ni mashabiki lakini hawajui kuwa kazi zao zinawataka kusimama katikati na kuripoti kile kilicho sahihi au kilichofanyiwa utafiti. Maswali mengi anayouliza mwandishi ni elekezi lakini pia yanaonyesha mapungufu katika uelewa wa jumla wa jambo hili.

TFF walichofanya (namaanisha sekretarieti) ni kuzikutanisha pande mbili kuona kama KWANZA zinaweza kuzungumza kuondoa tatizo lililopo la kutokuelewana. Pande zote zimesema inawezekana basi imeamriwa wafanye hivyo na ktkt kipindi wazungumzaji wakuu wawe ni wapatanishi kwa maana ya TFF. Sasa hapa tatizo ni nini? Au watu hawataki wapatane? Na ni kwa faida ya nani?

Pili, Katibu Mkuu hana mamlaka ya kisheria kuamua mkataba uko sahihi au umechakachuliwa, mwenye nafasi hiyo ni Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji. Ila katibu mkuu alichofanya ni kusuluhisha ili pawe na win -win situation. Hata makamani au kwenye vyombo vya kutoa uamuzi wahusika wanaweza kupewa fursa ya kupatana kabla ya kesi yao ya msingi kusikilizwa. Sasa sijui kwa nini watu wanabeza hatua hii.

Mimi ninavyofahamu kama Singano na Simba hawatapatana, na kama kila upande utashikilia msimamo lazima suala hili litarudi moja kwa moja kwenye kamati husika na hicho ambacho wengi wanataka kukisikia kwamba kuna mtu kafoji kitajulikana tu. Kwa hiyo watu wasianze kucheza ngoma ambayo bado haijapigwa. Mkondo wa sheria ni mrefu
ila ana mamlaka ya kubatilisha miikataba!
 
Kuna swali moja ambalo wachangiaji wenye ushabiki hawataki kabisa kulisikia na kulijibu. Nalo ni hili;
Ukiondoa mapungufu ya kiuandishi yaliyo ktk mikataba iliyo kwa Simba na Messi, mkataba upi kati ya hiyo ndio upo TFF na katika TMS? Naombeni majibu tuanzie hapo.
hiyo inategemea na aliyepeleka mkatabaa TFF, je ni Simba au Messi.
 
FUATILIA VIDEO HII ILI KUJUA UKWELI WA KILA KITU.

VIDEO :-

:teeth::teeth::teeth::teeth::t eeth::teeth::teeth::teeth::tee th::teeth::teeth::teeth::teeth ::teeth::teeth::teeth::teeth:: teeth::teeth::teeth::teeth::te eth::teeth:
 
Last edited by a moderator:
Huu ni muono wako wewe na unaweza kuwa potofu vilevile.

Kisheria ambayo wewe unaipgia kelele narudia kusema tena katibu mkuu wa TFF hawezi kuamua upi ni mkataba halali na upi umechakachukuliwa. Yenye kufanya hivyo ni Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji.

Sasa nikuulize swali: Pande husika ziliitishwa na Kamati inayoshughulikia mambo ya sheria au na sekretariati? Najua jibu unalo, sasa ulitegemea chombo ambacho hakiwezi kutoa uamuzi kama katibu mkuu atoe uamuzi ambao ni binding? Kwa mamlaka ipi? Sheria haimuliwi kwa hisia za kishabiki bali facts na sio kirahisi kama mnavyorahisisha.

Na madai yanabaki kuwa madai hadi yanapothibitika kuwa ukweli. Na mamlaka hiyo sio katibu mkuu.

Halafu kuna kitu katibu mkuu alisema kuwa pande husika zote ZIMEBAINI uwepo wa kasoro zilizopo ktk mikataba yote miwili, na huu ndio msingi wa kuona kama zinaweza kukaa pamoja na kuelwana. Sasa ungekuwa na hoja za msingi kama pande husika hasa Singano na Sputanza wangepinga hilo la kasoro kwenye mikataba yao halafu TFF ing'ang'anize kwamba lazima wapatane. Hapo tungesema TFF imekwenda kuhuni kihuni lakini kabla ya hapo ni hisia na unazi tu ndio unaosumbua na sio issue ya sheria.

Funny. Hiyo kamati unayoipigia upatu iko chini ya nani? Je hizi pande mbili ziliomba kusuluhishwa ama kupatiwa maamuzi ya uhalali wa mkataba? Huyo katibu kaingiaje hapo? TFF walitakiwa kuproduce nakala ya mkataba wanaoutambua kuwa ni halali. Upande usioridhika ungekata rufaa mahali husika. Badala yake wakakaa kama wapatanishi ili kulea ujinga.

Hili suala limeshavuka ngazi ya TFF hata kama hutaki kuelewa. Linahitaji vyombo maalum kwa kazi hiyo ili kubaini ukweli. Ila kama kawaida ya wabongo.....
 
huu ni muono wako wewe na unaweza kuwa potofu vilevile.

Kisheria ambayo wewe unaipgia kelele narudia kusema tena katibu mkuu wa tff hawezi kuamua upi ni mkataba halali na upi umechakachukuliwa. Yenye kufanya hivyo ni kamati ya sheria na hadhi za wachezaji.

Sasa nikuulize swali: Pande husika ziliitishwa na kamati inayoshughulikia mambo ya sheria au na sekretariati? Najua jibu unalo, sasa ulitegemea chombo ambacho hakiwezi kutoa uamuzi kama katibu mkuu atoe uamuzi ambao ni binding? Kwa mamlaka ipi? Sheria haimuliwi kwa hisia za kishabiki bali facts na sio kirahisi kama mnavyorahisisha.

Na madai yanabaki kuwa madai hadi yanapothibitika kuwa ukweli. Na mamlaka hiyo sio katibu mkuu.

Halafu kuna kitu katibu mkuu alisema kuwa pande husika zote zimebaini uwepo wa kasoro zilizopo ktk mikataba yote miwili, na huu ndio msingi wa kuona kama zinaweza kukaa pamoja na kuelwana. Sasa ungekuwa na hoja za msingi kama pande husika hasa singano na sputanza wangepinga hilo la kasoro kwenye mikataba yao halafu tff ing'ang'anize kwamba lazima wapatane. Hapo tungesema tff imekwenda kuhuni kihuni lakini kabla ya hapo ni hisia na unazi tu ndio unaosumbua na sio issue ya sheria.

sputanza!!!
 
Back
Top Bottom