Jamal Malinzi
JF-Expert Member
- Feb 9, 2013
- 710
- 650
Jamal
Tunakushukuru kwa kuungana nasi kwenye uzi huu ili tukupe ushauri na maswali.
Swali ;
Kumekuwepo na manung'uniko juu ya kuiendesha TFF kwa misingi ya ukabila, hasa ukipendelea watu wa Kabila lako. Unaweza kulisemea vipi jambo hili ili kuwahakikishia Watanzania soka lisilo na mizengwe?
Tunakushukuru sana kuwa karibu na jamii unayoitumikia. Kwa kweli soka letu linahitaji kuondokana na dhana ya usimba na uyanga
Jamal
Tunakushukuru kwa kuungana nasi kwenye uzi huu ili tukupe ushauri na maswali.
Swali ;
Kumekuwepo na manung'uniko juu ya kuiendesha TFF kwa misingi ya ukabila, hasa ukipendelea watu wa Kabila lako. Unaweza kulisemea vipi jambo hili ili kuwahakikishia Watanzania soka lisilo na mizengwe?
Ni vizuri Jamal Malinzi ajibu hili swali kwani linajirudia mara kwa mara....Linakera!
hsbaky kuna mtu alifungua thread humu jf kuhusu hili jambo nikajibu mpaka nikachoka,naomba utafute hiyo link utaipata.
Kimsingi mimi ninaangalia uwezo wa utendaji,malumbano ya ukabila tukianza kuya entertain kesho yatakuja ya udini matokeo yake tutapoteza mwelekeo,siko tayari kwa hilo.Na kimsingi sitazungumzia tena hili jambo.Nisamehe kwa hilo.
Dark City hakuna haja ya kuhangaika na jambo ambalo halina tija.Mambo ya msingi ya kujadili ni vipi tucheze Afcon Morocco mwakani,ni vipi tunaanda timu zetu za vijana na za wanawake,TFF ipate wapi vyanzo mbadala vya mapato ili yatumike kwenye miradi ya youth,tunazibaje mianya ya wizi wa mapato,tunajengaje mahusiano na vyama vya nchi zilizoendelea,ni mtaala upi utumike kufundisha mpira Tanzania,Academies zetu tunaziongezeaje uwezo wa kukuza na kulea vipaji na kadhalika.Tuachane na mambo ya personality tuhangaike na issues.Anayengang'ania ukabila kwa vyovyote vile ana lake jambo,tusimpuuze,tufuatilie tujue hidden behind kuna ajenda gani.
Kuna kipindi ulizuka mgongano wa kimaslahi kati ya tff na african lyon kuhusu kudhaminiwa na kampuni ya simu na tff waliwakatalia lkn inaonekana hiki kitu kinawatafuna nyinyi leo kwa ticket za electronic sbb huwezi kununua ticket kwa mtandao mwingine zaidi ya vodacom wakati wenye jukumu la kuuza yani crdb wanaweza kuungunisha huduma za kimtandao na mitandao mingine
Kwa nn msipotie hiyo mikataba na kuifanyia maboresho sbb naamini ipo siku matashindwa kuingia mkataba na kampuni za pombe kudhamini ligi sbb kati ya washirika wenu haruhusu pombe kwenye media yake wala uwanja wake
Mkuu JM.
TFF imejipanga vp kuuboresha uwanja wa taifa, kwa maana ya pitch? sababu katika mechi ya juzi uwanja umeanza kuonekana kuwa na vipara, wakati kulikuwa na takribani mwezi mzima wa kushughulikia hilo, kabla mzunguko wa pili haujaanza?
Mimi ningependa nijikite moja kwa moja kukuuliza maswali ya msingi.
1. Baada ya challenge Nairobi ulisema mnachukua maamuzi magumu kwenye benchi la ufundi lakini sijaona hayo maamuzi mpaka sasa wakati muda wa timu kuingia kwenye mashindano (AFCON) unazidi kusogea.
2. Hivi uteuzi wako wa wajumbe wa kamati za TFF unaangalia vigezo gani mbona watu ni wale wale walioshindwa kuufanyia chochote mpira wetu.
3. Mimi ni mfatiliaji mzuri wa Ligi daraja la kwanza (naamini ikiboreshwa italeta tija sana kwenye soka letu) kuna hili sakata la mechi kati ya STAND UNITED na KANEMBWA mbona mikanda ya video iko wazi wachezaji wa timu ya Kanembwa walimpa kisago mwamuzi je ni sahihi mechi hiyo kurudiwa? je sheria ndio inasema hivyo.
Electronic ticketing kusema kweli Ndiye mkombozi wa mapato ya Milangoni.Ila kuna changamoto ambazo inabidi tukabiliane nazo.Tayari tumekaa na washirika wetu CRDB kutafuta namna ya kurekebisha taratibu zake,TFF haiko tayari kuhatarisha Maisha ya watazamaji,tuwe na subra.Imani yetu ni kwamba tutafikia mahali tuondoe kasoro zote kwa faida na usalama wa wadau wote wa mpira nchini mwetu.Jamal Malinzi sijuhi kama lishaulizwa au la.
Ni nini hatma ya Electronic Tiketi ?
mimi naziunga mkono kwani hizi zitasaidia kuhakikisha mapato yanapatikana yote bila kuibiwa pia itasaidia ukusanywaji wa kodi kwa TRA.
Juzi nimeona Tanga manager wa uwanja akilalamika lakini hakika kw akumuangalia usoni anacholalamikia ni ukosefu wa hela za kuiba maana mapato yote yanenda CRDB na hakuna habari ya kupokea hela mkononi.
1.Tuko kwenye mchakato wa kuisuka upya idara ya ufundi.Taarifa zaidi zinakuja.
2.Uzoefu ,uwezo na uadilifu ni vigezo muhimu katika uteuzi wa kamati.Tuliowateua tunaamini watatusaidia.
3.Kamati ya utendaji imeagiza maamuzi kuhusu mechi ya kanembwa vs stand united yapitiwe upya na pia kamati ya nidhamu iwashughulikie wenye tuhuma za utovu wa nidhamu.
hsbaky kuna mtu alifungua thread humu jf kuhusu hili jambo nikajibu mpaka nikachoka,naomba utafute hiyo link utaipata.
Kimsingi mimi ninaangalia uwezo wa utendaji,malumbano ya ukabila tukianza kuya entertain kesho yatakuja ya udini matokeo yake tutapoteza mwelekeo,siko tayari kwa hilo.Na kimsingi sitazungumzia tena hili jambo.Nisamehe kwa hilo.
Mwanzo nilifikiri ni mwanamapinduzi wa soka letu lakini tokea uoneshe makucha yako kwenye swala hili sina imani na wewe na nitaungana na wale wote watakaoamua kukupiga vita.
Hivi unataka kutua ambia katika makabila mengine hakuna watu wenye uwezo katika hizo nafasi?
Usilete siasa katika mpira mkuu, humu sio FB, humu wapo watu wanaojua vitu na uelewa mpana wa mambo, hayo amajibu yako kwenye hoja nzito kama hii ni ya kitoto na uzito wake ni mdogo sana.
Ninachojifunza kupitia majibu yako ni uwezo wako wa kutukana makabila ya wenzio kwamba hayana uwezo wa kuongoza katika soka. Sio siri nime dispear sana na uongozi wako.
Nahisi machungu yangu ya TENGA wala hayajawezi kupoa tena ndio kwanza unazidi kuyaongeza.
Wape hi wahaya wenzio wenye uwezo wa kuongoza soka.