Maswali na ushauri kwa Malinzi

Kuna uzi humu kuwa Wambura ameshinda. This is great! Haki imetendeka. Sishabikii Wambura, ila ujinga wa mashabiki wa Simba na Yanga ukomeshwe!
CHUAKACHARA kikao cha kamati ya rufaa ya uchaguzi kinaendelea,maamuzi hayajatolewa mpaka sasa.
 
Last edited by a moderator:
Mheshimiwa Rais, swali langu ni soka la watoto wadogo, kumekuwa na upungufu mkubwa wa makocha wenye sifa za kufundisha watoto wadogo U14 pamoja na vifaa hasa mipira ya size ya watoto matokeo yake watoto wanatumia mipira mikubwa jambo ambalo kitaalamu halimjengei msingi mzuri. TFF ina mpango gani kwa kushirikiana na wadau kwanza kuagiza vifaa hivyo, na pili kutoa mafunzo kwa makocha wa kufundisha watoto?
 
Magehema kwa swali lako sina shaka wewe ni mtaalam wa mpira wa awali (grassroot),grassroot ni mpira unaochezwa katika umri wa miaka 6-12.Katika ngazi hii msisitizo ni kumfanya mtoto ajenge mapenzi ya kucheza mpira,hapa ushindi hautiliwi mkazo. Katika ngazi hii watoto wanatakiwa wachezee mipira midogo (size 3/4,mipira ya wakubwa ni size 5).Mipira hii inatakiwa ipatikane kwa wingi na kwa bei nafuu,tatizo kodi inasababisha bei yake iwe kubwa.Tanzania tuna shule za msingi yapata 19,600,unapozungumzia makocha wa grassroot unazungumzia kila shule ya msingi iwe na Mwalimu kocha aliyesomea na kupata leseni ya kufundisha grassroot football,ni jukumu la wamiliki wa shule hizi ambao ni ofisi ya Waziri Mkuu kupitia TAMISEMI kuhakikisha walimu hawa wanapatikana,TFF iko tayari kutoa ushirikiano wa kiufundi katika hili.Vyuo vya michezo kama Malya na Murutunguru na hata idara ya michezo ya UDSM vinatakiwa viweke umuhimu wa kipekee kwa kushirikiana na TFF kuhakikisha hizi kozi zinatolewa. Sasa hivi TFF inaandaa mpango wa miaka kumi wa maendeleo ya mpira wa vijana,yote haya yatafafanuliwa kwenye program hii na bajeti yake itaelezwa.Wadau wote tukiongozwa na Serikali,TFF,mashirika ya umma/binafsi,NGO,Media,watu binafsi itabidi tushirikiane kutekeleza mpango huu.Bila program makini ya maendeleo ya mpira wa vijana tutabakia kuota kushiriki fainali za kombe la dunia.Wenzetu afrika magharibi na kaskazini walithubutu wameweza (nchini Misri youth development programme yao ilianza mwaka 1957!).
 
Nina swali jingine, hili linahusu TFF kusaidia vilabu vyetu; kumekuwa na ushirikiano baina ya vilabu vya soka duniani katika kubadilishana uzoefu na ujuzi. Kama sijakosea (nikosoe pls) Ajax Amsterdam ina ushirikiano wa karibu na Ajax Capetown, hii imewezesha kusaidia hata baadhi ya wachezaji wa Ajax Capetown kufanya majaribio Amsterdam kwa urahisi. TFF kina mpango gani katika kuratibu hayo mahusiano ya vilabu vyetu na wenzetu waliotuzidi?
 
Heshima kwako Mkuu..umenijibu Vizuri sana..yaani nimeelewa...Tuombe mungu tupewe UENYEJI huo..
 
Swali langu ndugu Malinzi kwanini TFF iliamua kubadili muonekano wa jezi ya timu ya taifa? Lakini pia Heri rangi ingekuwa nzuri, mmechagua rangi nyeusi isiyo hata na mvuto, mlipata ushauri wa kitaalamu kweli? Na je serikali ilishirikishwa? Maana tunaona rangi ya juu ukiacha nyeusi sio rangi ya bebdera ya taifa letu.

Ushauri: ni bora mngeweka blue yenye michirizi ya njano, hapo tungekubali wadau wa soka. Rangi hii nyeusi si njema kwa mafanikio ya soka na haina mvuto.
Pia, ndugu Malinzi uongozi mpya unapoingia madarakani si lazima ubadili kila kitu, ulifanya hivyo kwenye secretariat, kamati za TFF etc, sasa hata jezi kweli?
 

mahangu nimeingia madarakani nikakuta mkataba wa jezi kati ya TFF na CAF na adidas ulikwisha sainiwa na kontena la jezi lilikwisha letwa,jukumu langu lilikuwa ni kuvalisha timu.Jezi mpya inaandaliwa tukijaliwa tutaanza kuzitumia muda sio mrefu.
 
Last edited by a moderator:

Nakuunga mkono Jamal Malinzi 100% kwa hili sababu hao Simba walianza kutoa shutuma kwa TFF na specific kwa Rais Malinzi kabra na baada ya kamati ya Rufaa ya TFF kukaa na kutoa maamuzi wakadiliki hadi kusema Wambura anarudishwa sababu ni rafiki wa Malinzi (utetezi wa kipuuzi kabisa) lakini wakashindwa kutambua wao kwenye club yao ndio walishindwa kuuunda vyombo hivyo vya maamuzi wakaamua kukasimisha hiyo kazi kwa TFF, alichofanya Malinzi ni sahihi tena alichelewa ni bora wakafanya mambo yao wenyewe kwa kuunda kamati zao wakishindwana ndio waje TFF halafu hao Friends of Simba kama wanadhani mgombea wao ndio chaguo la wanachama wa simba si waache wanachama waamue mbona kama wamejikita kutaka kupata ushindi wa mezani hovyo kabisa tena kuna wengine wana heshima zao wanajidhalilisha kila kukicha.
 
Salute kwako mh rais Malinzi! ili kuleta maendeleo ya soka, nadhani kuna mkakati wa mda mfupi na wa mda mrefu. Umelezea ktk huu uzi wako kuhusu walimu kuwa na ujuzi wa masuala ya soka ili wawafundishe hawa vijana wadogo/wanafunzi. Huu ni mkakati wa mda mrefu. Naomba utujuze mkakati wa mda mfupi wa TFF kuboresha soka letu kwa sasa? je, kuna utafiti wote uliofanyika kama kuna matatizo mengine kama ya kimazingira ya ukanda huu wa A. Mashariki ktk maendeleo ya soka, nauliza hivo make ktk soka ni kama tunafanana na km tofauti ipo ni ndg sana. Isije ikawa tunapiga kelele nyingi kumbe kuna sababu nyingine ya mazingira au biolojia ya watu wetu tofauti na watu wa A. Magh na Kask. vp kuhusu UMISETA na UMITASHUMTA mmeangalia kama zina mchango ktk kuibua vipaji vya wachezaji wachanga? Je, zipo shule za vipaji maalum ya soka? Viwanja vya baadhi ya mikoa na wilaya ni vibovu, hali hii pia huchangia ligi za madaraja ya chini kuwa mbovu, mkakati wenu upoje kuhusu viwanja hivi? Nawasilisha!!!!
 
Mi swali langu ni kuhusu uchaguzi wa simba ulivyousimamisha je ni kwa sheria zipi au kwa misingi ipi umeamua kuisimamisha?
Je kutokuwa na kamati ya maadili ni sababu tosha? kama ndio kwann kipindi hiki na sio kipindi cha kabla?
 
Wewe pia umelishwa sumu na waandishi waliohongwa na hao FoS, Malinzi anampenyeza vipi huyo mnayemuhita kipenzi chake acha kubeba maneno ya waandishi walionunuliwa na kuyaleta hapa, hapa tunataka facts.

Atakuwa kahongwa ili kuchafua hali ya hewa.
 
mh rais wa TFF vp tena mkuu mbona huji humu jukwaani? kuna maswali yangu tangu trh 16, na pia ya wadau wengine yapo kwenye huu uzi wako. naamini nia yako ya kuanzisha uzi ilikuwa njema hasa kupokea maoni ya wadau, kujbu maswali ili kuleta maendeleo ya soka letu. kwa heshima tunakuomba uwe unatembelea mara kwa mara huu uzi wako. nadhani na ndio maana uliwaomba mods waweke stick uzi wako.
 

Nakushauri badilisha msimamo wa communication katika JF, humu kuna watu wa aina zote!!!! Be selective to respond.
 
Ndugu Jamal, usiyumbe simamia lile unaloliamini. Ulisema utasimamisha uchaguzi Simba mpaka waunde kamati ya maadili. That was a credit to you maana ulikuwa unasimamia sheria. Umeyumba/umeyu,mbishwa na kubadili lililo la kweli. Nadhani waliokwenda mahakamani watashinda maana kamati ya maadili haipo Simba, katiba imevunjwa. Let us wait and see what the Judge will decide!
 

Jamal Malinzi ni member JF.Njoo utueleze kwa nini hukusimamia maamuzi yako ya awali.Pia kwa nini ulihamisha ofisi za TFF Karume hadi katikati ya jiji? Umefanya maamuzi mengi yasiyo na maana,lakini kwa gharama kubwa.
 
Last edited by a moderator:
Jamal Malinzi ni member JF.Njoo utueleze kwa nini hukusimamia maamuzi yako ya awali.Pia kwa nini ulihamisha ofisi za TFF Karume hadi katikati ya jiji? Umefanya maamuzi mengi yasiyo na maana,lakini kwa gharama kubwa.

Ndio maana nasema ameyumba. Simamia lile unaloliamini ni sahihi na baada ya kufanya utafiti wa kutosha. He is a public figure with all eyes on him!
 
Ndio maana nasema ameyumba. Simamia lile unaloliamini ni sahihi na baada ya kufanya utafiti wa kutosha. He is a public figure with all eyes on him!
sikuona mantiki ya Raisi wa TFF kubadilisha maamuzi yale muhimu, sasa hili swala watu wameenda mahakamani kudai haki zao maana chombo kilichoundwa kuhakikisha haki zinapatikana eti wanatumia busara, busara ambayo inavunja katiba! busara inapotumika basi katiba izingatiwe na kuheshimiwa! Busara inapotumika kuvunja katiba na vipengere hiyo inakuwa si busara tena
 

Muda ukiruhusu tutatoa tathmin ya matokeo ya maboresho ya timu ya Taifa.Kwa kifupi tunao vijana ambao mwalimu Maart kawchukua moja kwa moja timu ya Taifa,wapo ambao wameingia national team under 20 na 23 kwa anili ya olyimpics,wako vijana zaidi ya kumi na moja toka maboresho wamesjilowa vilabu vya ligi kuu kwa msimu ujao.Vumbi likitua tutatoa taarifa kamili ndo utoe judgement kama maboresho yamefanikiwa au la.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…